Komodo dragon ndio mnyama hatari zaidi kuliko Black mamba (koboko), Simba, Mamba, Tiger na wanyama wengine wa aina hiyo

Ni mnyama coward na mviziaji. Anachofanya anavizia ukiwa huna hili wala lile, anakung'ata halafu anakimbia kama kafumaniwa usije mdhuru, anakuacha akisubiri sumu isambae mwilini udondoke aanze kunusa nusa ulipopita ndo ale nyama ya mwili wako. Hata hivyo huwa anamuavoid binadamu.
 

Niliwahi mkuta kichakani nikamkimbiza huku mkononi nimeshika ndala moja alitoka baru hadi akaingia shimoni
 
Blank mamba ndio hatari ndani ya dakika umeshapotea
 
Ni bora wawe hukouko Asia, Ni wanyama hatari sana na hizi kampeni za utalii wa ndani kuna baadhi ya maeneo viongozi wanahamasisha tu watu kwenda kwenda kutazama mapori nawezajikuta unavagaa balaa hilo!
Hahahaha unaambiwa huko walipo huuwa viumbe mbali mbali vibaya sana. Ila ndo hivyo hakuna namna kwa sababu bado nchi hizo zinawatumia wanyama hawa kwa utalii.
 
Wanasema mdomoni mwake ana bacteria wengi hatari sana kama akikung'ata huwez kupona hata hakuwahishe hospital unapata septic shock baada ya mda kidogo.
Huyu nafikiri kaumbwa kwa ajili ya kuuwa tu viumbe wengine wakiwemo wanyama, ndege na binadamu. So kwahiyo akishakutia jino tu basi hakuna namna ya kuendelea kuishi au kupata muda wa kuandika usia kwa watoto.
 
huyu kenge mwenye jina la kizungu ndio unaemfagilia namna hii!?
Mkuu, Nakuomba ukafanye marejeo usije ukatupoteza bila kukusudia!.
Kenge kwa kizungu anaitwa lizard, huyu anaitwa Komodo dragon.

Kwahiyo ni vitu viwili tofauti. Ni mfano umwite Tiger, Leopard au Cheetah (chui) paka eti kwa vile wanafanana muonekano wao. Hili dubwasha limeshindwa kupewa heshima na wazungu kwa sababu halikuwahi kuishi huko kwao ulaya. Hili lidubwasha lingekuwa linapatikana ulaya na Afrika basi lisingekosa kuwekwa katika wale tano bora ya wanyama hatari duniani. Kama chui ambae ni mchumba tu amewekwa kwenye list vipi hili dubwasha lenye uwezo wa kuangamiza kiumbe chochote hapa duniani anyimwe heshima hiyo ya tano bora?
 
Shukran mkuu kwa kuongeza baadhi ya mtazamo.
 
Kiufupi binadamu tumependelewa sana wala haijatokea bahati mbaya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…