Konda wa daladala aliniokoa kipindi nachapika na maisha

Konda wa daladala aliniokoa kipindi nachapika na maisha

Pole kwa uliyo pitia na hongera umevuka salama, nimekuelewa sana
Mungu alikupitisha uone maisha jinsi yalivyo na tumaini huwezi dharau mtu wa hali ya chini

Sometimes, nikimua mtu anauza maji, mahindi ya kuchoma na mpa respect sana napenda mwanaume mpambanaji. 👊
 
Niliwahi pia saidiwa na Konda 2015 Goms to Chanika Saa 2.00 usku. Sina hata mia. Nilimueleza shida yangu, jamaa akaniruhusu nipande akaniachia na siti kabisa. Tulifika nikamuomba Na. ya simu akasema haina haja!
dah! mwanetu maisha haya ni fumbo sana
 
Pole kwa uliyo pitia na hongera umevuka salama, nimekuelewa sana
Mungu alikupitisha uone maisha jinsi yalivyo na tumaini huwezi dharau mtu wa hali ya chini

Sometimes, nikimua mtu anauza maji, mahindi ya kuchoma na mpa respect sana napenda mwanaume mpambanaji. 👊
shukrani
 
Sometimes, nikimua mtu anauza maji, mahindi ya kuchoma na mpa respect sana napenda mwanaume mpambanaji. 👊
Sure. Hata mimi nikiwaonaga hawa watu, huwa najiuliza "hivi kama huyu bado ana matumini ya maisha na biashara hii, mimi nina sababu gani ya kukata tamaa na shule ninayo?".
Huwa wananipa kila sababu ya kuzidi kukaza.
 
tuendelee kupambana
 
Based on true story:

Nakumbuka graduation yangu na washkaji zangu ilikua na mvuto sana pale mlimani city hall mwaka 2017 ,niliona baada ya muda mfupi tu basi ningepata mchongo mzuri na ningevuta usafiri unaosomeka crowm new model within the year(s)

Jk alitoa hamasa kwa vijana wakapambane na mtaa either kwa kujiajiri ama kuajiriwa.

muda kidogo badae hakuna rangi niliacha kuona baada ya kuhitimu chuo demu wangu alisepa. ndugu na wajomba walio niahidi kazi wengi niliishia kuramba blueticks whatsapp na kejeli juu baada ya kuwasambazia CV.

nilichapika na maisha balaa nusra kudata, maumivu makubwa ambayo yalikua yakinitesa moyoni mwangu ni kuwa ni lini nitawabeba wazazi wangu kutoka kwenye lindi la umasikini uliokithiri atleast milo miwili homu isiwe tabu tena.

kuna siku nimetoka kutafuta kazi vingunguti viwandani nikakuta formeni anahitaji umtoe chochote kitu ili akuunganishe kazi! nikatoa 9k lakini bado nilikosa kazi siku ilee,changamoto ikaja muda wa kurudi mageto kwa mshikaji niliko kua najiegesha nauli sina.

oya wanangu, nikasogea sogea kwa mguu mpaka buguruni kwa bakhresa kituo cha daladala huku njaa ikinichapa kweli kweli nikamwita konda pembeni (konda nisaidie mwanetu japo buku ama uni link na daladala za mawasiliano sina nauli na ubao unapiga sana) jamaa ile kunitazama tu mwana akazama mfukoni na kuniachia buku mbili .

nafika geto sijakaa sawa napokea simu toka kwa mdogo angu alioko shule kuwa bro naumwa nimeletwa hospitalini na wanafunzi wenzangu malaria imenibana sana kama unasomeka nitumie 12k ambayo wenzangu wamenilipia kwani homu wazazi nao hawapatikani hewani licha ya jitihada kadhaa, aiseeh moyo wangu ulipoteza tumaini siku ile niliona kama kuna mkosi unanisaka mimi na familia yetu .

nisiseme mengi wadau nikaja kupata ajira utawala huu wa mama samia kamwe siwezi sahau changamoto wanazo pitia jobless
Pole kwa uloyopitia na Hongera kwa kupata kazi , hata mimi nilifanya mahafali pale m City 2017 but hali mtaani bado ni ngumu sana naamini ipo siku.
 
Back
Top Bottom