Yupo jamaa hapa Dar kwa jina Masawe Kuna siku alikua Hana hata unga wa kukorogea uji. Basi akamfuata jamaa yake town, na jamaa akamuambia usihofu, njoo ofisini kwangu saa tatu asubuhi kesho nitakua nimeshatoka benki.
Basi jamaa yangu Masawe mwenye njaa asubuhi na mapema akaanza mdogo mdogo kwa mguu mpaka posta akitokea Mwananyamala alikopanga . Kufika ofisini kwa tajir akaambiwa boss amekusubiri Sana wewe hutokei, amesema Kama unahitaji kumuona umfuate Uwanja wa ndege maana leo Kuna mzigo anausubiri huko eapoti.
Mwenye njaa Masawe Mia mfukoni Hana, huku ana njaa na jua ndio limeanza kuwaka. Mwenye njaa akapiga moyo konde na njaa yake na kiu akaianza safari ya kumfuata boss Uwanja wa ndege. Ile njia haina shortcut Wala kivuli. Ilibidi Sasa asitembee polepole maana Kama atamkosa boss Uwanja wa ndege ingebidi arudi Mwananyamala kwa mguu huku ana njaa na kiu.
Dogo alipiga moyo konde Ile kufika airport Ni saa Saba, akaambiwa boss Yuko lunch nje ya Uwanja , kumbuka mshkaji alikua Hana simu maana enzi zile wenye simu Ni wachache kuliko wenye magari.
Alisubiri Hadi saa nane ndipo tajiri alipotokea na kumkabidhi ule mkopo. Mwenye njaa baada ya kuagana na tajir alipanda daladala Hadi buguruni sokoni. Alinunua papai laini kwanza maana kwa zaidi ya masaa 24 alikua hajatia kitu tumboni.
Baada ya hapo akachukua mchuma wa Mwananyamala.