Kongwa sirudi tena, kuna vumbi na funza miguuni nimepatia huku

Kongwa sirudi tena, kuna vumbi na funza miguuni nimepatia huku

Wakuu,

Huku hata iweje sitorudi tena pana funza za hatari, vumbi nikama linazaliwa huku yaani hapaeleweki kamwe naapa sitorudi tena huku hata iweje.

Huku hapafai kuishi maji ni tatizo sugu yaani palifaa watu wasikae kabisa maana pabaya sijawahi kuona.

Huku hapana hapana.
hahahaha mkuu kongwa ya wapi hiyo mkuu pole Sana!
Je Ni zoisa,makawa,mageseni,songambele,au? Yaani huko hutakiwi kuvua viatu mchana na soksi usiku.
 
Mkuu
Mtoa maada akumbushwe kwamba Dodoma yote ipo hivyo..., jaribu kwenda Mpwapwa huko utashangaa
Mpwapwa kuna shida ya maji sanaaa lakini HAKUNA finza.Ila sehemu zote hizo barabara ni shidaaaaa yaani Ni Kama hakuna viongozi kabisaaaaaaaa
 
Mpwapwa HAKUNA funza Mkuu. Funza wapo kongwa kaskazin Ni nouma yaani ukifika usiku kesho asubuhi tayari miguu inawasha funza washa kuingia!!
Mimi nazungumzia vumbi..pako hovyo mnoo.
 
Ni kweli kongwa pabaya na pana sifa nyingi mbovu lakini funza wa miguuni ni uchafu wako.

Mimi nimefanya kibarua kongwa miaka miwili sijawahi kua na funza wala magaga

Vumbi la kongwa ni kama la Mbinga vijijini
Vumbi la kongwa lina afadhali kuliko la kasulu
Chumvi kwenye maji ya Kongwa ni afadhali kuliko udom
Mbeya mjini ni Dust City(lile vumbi kongwa inasubiri) na kwa msimu wa mvua ni mud City, tukuyu pekeake ndo Green City.
Hivi lile vumbi la Moshi mjini hulijui? Lile vumbi ukikanyaga chini linaruka linafunika kiatu chote, ile ni poda kabisa

Ukiwa mchafu, hata ukiishi Mwanza (Mwanza ni Pasafi) funza utawapata tuu.
Kongwa hapana tusidanganyane dom ni pabovu generally!!! Utatumia nguvu nyingi bure kijitetea
 
Jifunze kusoma kwa kuelewa, sio kusoma ili ujibu. Maana usipoelewa ndo unajibu uwele kama huu. Soma tena kuanzia mwanzo.

Nasisitiza, uchafu ni sumu, ukiwa mchafu hata uishi ulaya utapata funza tuu.
Mkuu kongwa HAKUNA Cha uchafu Kuna mifunza kutokana na udongo wake tifutifu yaani ukifika huko usivue socks au viatu
 
Back
Top Bottom