Mbalamwezi
JF-Expert Member
- Sep 30, 2007
- 800
- 172
kajenga UDSM
na kukusomesha bure wewe na viongozi walioko sasa madarakani
hiyo ndio inaitwa long term planning (kawasomesha bure badala ya kufanya kazi kwa bidii mnaendelea kuiibia taifa letu)
It is a different ways of viewing things. Mie jambo hili sina tatizo nalo ikiwa tunafanya mambo kwa maslahi ya nchi na watu wake. Bahati mbaya sana hali haiko hivyo ndo maana kwa kila hoja watu wanakuwa na wasiwasi.
Tuna ardhi kubwa kwa muda mrefu. Tumeshindwa kuitumia to our own advantage. Tunaweza kuikodisha ardhi hiyo kwa watakaoitumia na sisi tule rent. Pengine hiki ndiyo kinachotufaa. Ikiwa thinking iko hivyo hawa watu tutawatoza rent ambayo ni commercial. Tuweke kabisa policy ya kukodisha ardhi yetu commercially kwa wanaotaka kuitumia hapa sitakuwa na shida, kwani policy itakuwa debated na hatimaye sheria zitatungwa.
Kwa mfano, mimi nina kieneo changu hapa mjini ambacho nimejenga kibanda changu cha kuishi. Sifanyii biashara yoyote. Eneo lile ni wastani wa meta za mraba 2,600. Kodi kwa mwaka nalipia jumla ya shilingi 26,000 kwa mwaka kama land rent (nenda wizara ya ardhi ukathibitishe). Hii ni kiwango cha karibu shilingi 10 kwa kila meta moja ya mraba.
Sasa kwa hawa watu wa nje (wawe wakorea, waarabu au wazungu) tuwakodishe kwa viwango hivyo hivyo! Eneo hilo linalosemwa yaani kilomita za mraba 1,000 ni sawa na mita za mraba Billion moja kwani kila kilomita ya mraba moja, ina mita za mraba milioni moja (1,000,000). Sasa hawa wakorea tukiwakodisha kwa kiwango sawa na hiki ninacholipa mimi cha karibu shilingi 10 kwa mita moja ya mraba, hapa tumeshapata jumla ya shilingi bilioni 10 kwa mwaka (karibu Dola milioni 8).
Lakini hawa wanaitumia ardhi hii kwa kilimo cha kibiashara. Kwa hiyo kodi yao iwe ni ya kibiashara angalau shilingi 100 tu kwa meta moja ya mraba. Tutapata kiasi cha shilingi bilioni 100 kwa mwaka. Fedha hizi zikiingizwa kwenye subsidies kwa wakulima wa Tanzania (kwenye mbolea, madawa na zana za kilimo) tuna uhakika wa kuwa kilimo chetu kitakuwa kimepona for good.
Tanzania tuna ardhi kubwa inayofaa kwa kilimo, zaidi ya kilomita 250,000 za mraba. Hata tukikodisha kilomita 50,000 tu za mraba tutapata Zaidi ya Dola bilioni nne. Fedha hizi zitatosha kuleta mapinduzi ya kilimo na viwanda tunayoota ndoto kuyapata. Tunahitaji a different way of thinking!
Ikiwa ardhi ina thamani kihivyo, kwa nini tusikodishe tukala rent?? Tatizo tutawapa ardhi bure kwa ahadi kuwa tutaajiriwa mashambani na kukuza uchumi. Hata kodi hizi tunazowakandamiza watanzania WAGENI HAWAZILIPI!!! HILI NDO TATIZO LETU!!
Na kipindi cha Al Haj Mwinyi jee? Nadhani bila shaka utasema barabara, mataa ya kuongoza magari, mataa ya barabarani, ma-parking meters ya uhindini na ustawi wa Waswahili kwa ujumla yooote yalikuwa tambarare kwa mbele hadi alipoingia Mkapa na kuvuruga kila kitu kama kawa...halafu, alhamdulilaaah, kwa nguvu za Mwenyeez Alaah, akaja Kikwete ambaye tena akanyoosha mambo, au siyo?!
Nipeleke kwenye mahakama zilizojaa usanii! Hizo kesi za EPA, Richmond nanga inapaa ufisadi wa Mkapa kujiuzia nyumba za serikali na mawaziri wake na mgodi wa Kiwira bado wanajitahidi kupulizia kadri wanavyoweza. Rostam na utapeli wake wa Richmond/Dowans hadi leo hajaguswa. Utapeli wa kununua rada ya kifisadi na kuna ushahidi wa kutosha kwamba Chenge Vijisenti na Idrissa Rashid walipokea rushwa katika ununuzi ule bado wahusika wanapeta uraiani. Yule Vethlani alikuwa anahojiwa na vyombo vya dola badala ya kumuweka rumande wakati anavisaidia vyombo vya dola katika uchunguzi wao, lakini wakampa upenyo makusudi ili asiwachome vingunge wahusika aliokula nao zile $12 millioni.
Sasa huu ufisadi wa kuingia Ikulu 2005 ndiyo unadhani utashughulikiwa na hizi mahakama za kishkaji!!? Huoni kama hapa kuna pattern ya kuficha kila madhambi yanayowahusu mafisadi!? Au na wewe ni mmoja mafisadi hao huoni dhambi zozote!? Acha hizo za kutaka kuufumbia macho ukweli uliojidhihirisha.
Na atakapoondoka JMK mataa yote yatazima na parking meta kuchakaa unless aje Mswahilina mwengine.
kazi ya kiongozi ni kutumia kodi za wananchi kwa ajili ya maendeleo ya taifa. kama kodi haitoshi anaweza hata kukopa. Akitumia kodi zetu vizuri tunamsifia, akitumia vibaya tunamshutumu...ondoa uwendawazimu wako,hiyo bure pesa katoa mfukoni mwake au ni kodi ya wananchi na madeni tunayoyalipia mpaka leo,
unategemea raisi ajenge shule zake kutokana na hela zake nadhani hii ndio pumbabora zile shule angewaachia hao wakoloni waziendeshe wenyewe na ajenge za kwake ndio uongee hizo pumba zako!
Laiti ungallijuwa history ya UDSM, usingesema hayo.
Wakati mimi nasoma kulikuwa na ada ya Shillingi 33 kwa mwaka au Shillingi 11 kwa term (primary), baada ya hapo nikaenda kusoma nje ya Tanzania, si kwa fedha za Serikali. Kumbuka, enzi hizo za ubepari (Kabla ya Azimio la Arusha), kama ilivyo tena sasa, ilikuwa ni sifa kwa watu wa Dar Es Salaam kupeleka watoto wao Ulaya kwenda kupata masomo zaidi, kama vile ilivyokuwa kwa nyinyi wa bara kuletwa hapa Dar.
Waliosomeshwa bure na Nyerere nadhani unawajuwa, kwa kuchaguliwa na vigezo vya kuchaguliwa nadhani unavijuwa.
....ushaanza mambo yako tena. Leo hii tunaongelea Wakorea, hawa watu hawana dini za kishabiki shabiki tulizozoea sisi mkuu!! Ardhi ya Watanzania kwanza, mambo ya Imani baadae!
Sawa, nikubaliane nawe kuwa Mwl. aliondoa taa mabarabarani, kunyofoa parking meters na kuziba mifereji. Maana hayupo hapa kuweza kujitetea. Lakini kuvirudisha vitu kama hivi inahitaji miaka mingapi, 20, 30, au?!!
Mapato tu pekee ya pale stand ya mabasi ubungo kama yangelikuwa yanasimamiwa ipasavyo na kwenda kwenye mfuko wa halmashauri, leo hii tungelikuwa na maUDA na hizo parking meters zingelikuwa operational mpaka Kawe Tangini. Lakini cha kushangaza hao unaowataja kama visionaries wa jiji, wengi wako implicated kwenye scandals kubwa za ufisadi. Na kwa pale Ubungo, hata ripoti ya CAG inasema kuna ubadhirifu.
Kingine unachosahau ni vita vya NDULI. Bila jitihada za wanabara na jemedari Nyerere leo hii hapo Kigamboni huchelewi kukuta watu wangelikuwa wanaongea Kiganda kama lugha ya Taifa. Backing ya Shekh Gadaffi kwa Nduli ndiyo uilaumu, kwani gharama za kumwondoa Nduli na kuhakikisha hela yetu inabakia stable iliongezeka. Bila yeye mpambano usingechukua muda mrefu. Sasa hapa ni mambo ya priority. Je, ungelipendelea lipi - Kulazimishwa kuongea Kiganda na Nduli na kuacha kuongea Kizaramo? Kuhakikisha ukabila unasambaratishwa kwa kufanya Kiswahili kuwa lugha ya Taifa au kuwa na parking meters?!
Nipeleke kwenye mahakama zilizojaa usanii! Hizo kesi za EPA, Richmond nanga inapaa ufisadi wa Mkapa kujiuzia nyumba za serikali na mawaziri wake na mgodi wa Kiwira bado wanajitahidi kupulizia kadri wanavyoweza. Rostam na utapeli wake wa Richmond/Dowans hadi leo hajaguswa. Utapeli wa kununua rada ya kifisadi na kuna ushahidi wa kutosha kwamba Chenge Vijisenti na Idrissa Rashid walipokea rushwa katika ununuzi ule bado wahusika wanapeta uraiani. Yule Vethlani alikuwa anahojiwa na vyombo vya dola badala ya kumuweka rumande wakati anavisaidia vyombo vya dola katika uchunguzi wao, lakini wakampa upenyo makusudi ili asiwachome vingunge wahusika aliokula nao zile $12 millioni.
Sasa huu ufisadi wa kuingia Ikulu 2005 ndiyo unadhani utashughulikiwa na hizi mahakama za kishkaji!!? Huoni kama hapa kuna pattern ya kuficha kila madhambi yanayowahusu mafisadi!? Au na wewe ni mmoja mafisadi hao huoni dhambi zozote!? Acha hizo za kutaka kuufumbia macho ukweli uliojidhihirisha.
Kuna mahakama za Rushwa za kimataifa kama za Tanzania huziamini, unangoja nini?
Niambie, Tanzania tulikuwa na Nyerere miaka 30, tumepigana vita ngapi na niambie miaka 30 kabla ya Nyerere tumepigana vita ngapi na miaka 30 baada ya Nyerere tumepigana vita ngapi?
QUOTE]
unajua kuhesabu kweli? halafu Tanzania miaka 30 kabla ya Nyerere ni Tanzania ya watu gani hiyo? Na kweli ungetaka turudishe tulivyokuwa miaka 30 kabla ya Nyerere?
Nyerere, aliikuta Dar Es Salaam nzuri kama mtoto, na kama ilivyo.Hakuna alichokiongeza wala kuwa na nadharia ya kuongeza. Uozo wa Dar Es Salaam wa hivi sasa unatokana na huko nyuma (Kwa Nyerere). Na Dar Es Salaam ilianza kuharibika wakati wa Nyerere. Tuulize sisi tuliozaliwa na kukulia hapa tukueleze! Hakuna muundo mbinu mpaya wowote alioufanya Nyerere Dar Es Salaam utaozidi asilimia moja ya aliyoyakuta.
Mag3,Labda ni wewe huijui historia ya Dar Es Salaam. Ukiacha sehemu zilizojulikana kama Uzunguni ama Uhindini, sehemu kubwa ya iliyojulikana kama Uswahilini wakati nchi inapata uhuru mwaka 1961, Ilala, Magomeni, Mwananyamala na kwingineko zilisheheni nyumba za makuti na hazikuwa na barabara za lami.
Mwaka mmoja tu baada ya nchi yetu kupata uhuru, Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) lilianzishwa ili kusaidia upatikanaji wa nyumba bora za makazi, hasa mijini. Baada tu ya Shirika kuanzishwa, Serikali ilikuwa inatoa ruzuku kwa Shirika ili kuliwezesha kujenga nyumba nyingi kadri ilivyowezekana. Kwa kutumia ruzuku hiyo, Shirika liliweza kuondoa nyumba za makuti (slum clearance), hasa jijini Dar es Salaam na kujenga nyumba za saruji na kuezekwa kwa mabati.
Hivyo ndivyo zilivyojengwa nyumba za Ilala, Magomeni, Mwananyamala. Ujenzi kama huo ulienea pia kwenye miji yote ya mikoa na wilaya nchini. Ni wakati huo huo wa "operation makuti" barabara zote katika sehemu hizo (Ilala, Magomeni na Mwananyamala) ziliwekewa lami. Kabla ya hapo sura ya jiji la Dar es Salama na hasa zile sehemu za uswahilini hazikuwa tofauti na yale mabanda tunayoyashuhudia hadi leo sehemu nyingi za mkoa wa pwani.
Koba,Nafikiri huyu Governor wao ana make sense kidogo,lakini ukweli kilimo cha peasant hakiwezi kuondoa umaskini,nafikiri kilimo kwa TZ kina weza kuondoa umaskini zaidi ya utalii na madini lakini lazima kuwatumia watu wanaojua kilimo,Zimbabwe ilikuwa haina kitu zaidi ya hawa commercial farmers ambao walikuwa ndio wanaendesha uchumi wa nchi na kwa waliofika harare kabla ya Mugabe kuiharibu atakubali jamaa walikuwa tofauti na nchi zilizoendelea/states...tuna ardhi nzuri sana mikoa ya kusini ya kuweza kuondoa njaa na kuweza kuuza nje na kutoa ajira kwa mamilioni lakini lazima kama tuna taka tushirikiane na serious investors sio blah blah za kina Richmond!
Mag3,
Uongo huumbuliwa na ukweli. Huyu Darisalama chuki zake kwa Nyerere ndizo zinazomwongoza kusukumiza uwongo na kubadilisha ukweli. Kuna thread aliongopa kuwa msikiti wa Butiama ulijengwa baada ya kifo cha Nyerere wakati mimi niliuona nilipokwenda kule kwa mazishi Oktoba 1999.
Jamani tusipofushwe na chuki.
Mag3,
Uongo huumbuliwa na ukweli. Huyu Darisalama chuki zake kwa Nyerere ndizo zinazomwongoza kusukumiza uwongo na kubadilisha ukweli. Kuna thread aliongopa kuwa msikiti wa Butiama ulijengwa baada ya kifo cha Nyerere wakati mimi niliuona nilipokwenda kule kwa mazishi Oktoba 1999.
Jamani tusipofushwe na chuki.
Niambie, Tanzania tulikuwa na Nyerere miaka 30, tumepigana vita ngapi na niambie miaka 30 kabla ya Nyerere tumepigana vita ngapi na miaka 30 baada ya Nyerere tumepigana vita ngapi?
QUOTE]
unajua kuhesabu kweli? halafu Tanzania miaka 30 kabla ya Nyerere ni Tanzania ya watu gani hiyo? Na kweli ungetaka turudishe tulivyokuwa miaka 30 kabla ya Nyerere?
Of course, utakapopata jibu ndio utajuwa speed iliyomchukuwa kuimaliza nchi