Korea yanunua ardhi "kwa mkopo" Tanzania, Serikali yasita kuthibitisha


Tazara, sijui hata kama Tanzania tulitowa senti tano yetu kuijenga. Labda wewe unafaham. Lakini naomba kaitazame hali ilivyozorota halafu ndio utajuwa, kama tuliitolea fedha yetu au la. Kama kweli tumeitolea fedha basi tu mapunguwani kwa kupoteza fedha nyingi halafu tunashindwa kukiendesha kitu tulichokigharamikia.
 

Hapa nakuunga mkono mia kwa mia, na hawa wa Korea tutaona jinsi ardhi hiyo hiyo inayotushinda sisi kulima na ku-export mazao yawe ghafi au yameshasindikwa watakavyofanya. Na naomba waje na tupate fursa ya kujifunza kwa vitendo. Tusikae domo kaya tu.
 

Mosi, nakushangaaa kwa kuona kupigwa ''vita sana na nchi za magharibi'' kuwa ni sifa.

Pili, unaemataja hapo juu ni Mwinyi huyu anaesemekana kuwa ni ''ambaye aliongoza serikali ya awamu ya pili iliyoruhusu mabadiliko makubwa ya kisiasa, kijamii na kiuchumi kiasi cha kupewa jina la Mzee Ruksa" Au unaongelea Mwinyi yupi?

Tatu, nakubaliana nawe kwa hili "Mwalimu hakuwa perfect alifanya makosa yake''

Nne, sikubaliani na wewe katika hili "makosa yake ni madogo sana ukilinganisha na mazuri mengi aliyoyafanya alipokuwa madarakani" nijuavyo mimi ni kuwa alikuwa na makosa mengi tena makubwa kuliko Rais wa Awamu yeyote Tanzania. From experience, na namshukuru Allah, kuniwezesha kuziona awamu zote nne zilizoshika madaraka Tanzania na kabla ya kuwa Tanzania, nilikuwepo wakati wa Nyerere toka alivyokuwa waziri mkuu mpaka alivyong'atuka, hadi hii leo (Alhamdullillah). Sijaona, ''mazuri'' yaliyopita ''mabaya'' aliyoyafanya Nyerere kuwashinda viongozi waliokuja baada yake, never. Kweli, tumwacheni awepo apapendapo kumuweka Mungu, na aliyochuma akiwa hai, alipwe kwa kipimo chake, huko aliko, bila kuzidishiwa wala kupunguziwa.
 

Wazazi wangu walikuwa na uwezo wa kula na kulala bila matatizo na wakiishi Kariakoo na waliweza kweli kunipeleka nje kwenda kusoma, namshukuru Allah kwa hilo, wala halina ubishi.

Hawakuwa wazito kama utakavyo + sina chuki na Nyerere kama Nyerere binafsi bali nnachuki ya kutokuwa kiongozi makini na kutuharibia nchi yetu. Nashangaa sana kuona watu wengine humu, nadhani wengi wao wakati wake, ya ama hawakuwepo au walikuwa bado vikinda, wanampa sifa ambazo hakuwa nazo.

Wazazi wangu hawakuwa na ugomvi na Nyerere, na by the way, ofisi ya kwanza ya TANU na kabla ya hapo TAA iko ubavuni wa iliyokuwa nyumbani kwetu hapo Mtaa wa Lumumba. Na wazee wangu wakijuana sana na Nyerere, kabla na baada ya kuukwaa ukuu. Kama kuna sifa yoyote inayobidi nimpe, ni kuwa, mara kwa mara (kila apatapo nafasi), alipokuwa akija ofisi ya TANU alikuwa akipita pale kwetu kuwasalimia wazee japo dakika mbili tatu, hilo moja lake nilijuwalo.
 

Ni wewe ambae huziamini si mimi.
 

Unajuwa mwaka mmoja baada ya Uhuru bajeti ilikuwa ikitoka wapi? au unajisemea tu? na mpaka hii leo zaidi ya asilimia 30 ya bajeti unajuwa inatoka wapi?
 

Labda huo msikiti uliokuta ulikuwepo kabla, nenda kauone alijengwa baada ya kufa Nyerere halafu uulize umejengwa na nani? halafu njoo ubishane.
 

Tazama huyu mwingine, kuezekwa nyumba bati anaona ni maendeleo, wakati wa mkoloni alikuwa akijenga nyumba za mabati kwa ajili ya kukaa manamba, na maofisa walikuwa na nyumba za vigae.

Sisi, tuliopo pwani tulikuwa tukiezeka kwa makuti, tusiwe kama manamba wanaowekwa nyumba za full suit, juu bati pembeni bati.

Na raha yake nyumba za makuti ni kuwa, hazina joto. Na mpaka hii leo ukiona mahoteli ya kifahari Mengi tu Tanzania, ambayo si ya ghorofa yanaezekwa kwa makuti. Its simple, cheap comfort. Usifikiri kuezeka mabati ndio kuendelea. Katazame nchi zilizoendelea uone kama wanaezeka kwa bati. Sasa limbukeni wewe au mimi aonae kuwa nyumba ya bati ni maendeleo?

"Thatching is the craft of building a [ame="http://en.wikipedia.org/wiki/Roof"]roof[/ame] with dry vegetation such as [ame="http://en.wikipedia.org/wiki/Straw"]straw[/ame], [ame="http://en.wikipedia.org/wiki/Phragmites"]water reed[/ame], [ame="http://en.wikipedia.org/wiki/Cyperaceae"]sedge[/ame], [ame="http://en.wikipedia.org/wiki/Juncus"]rushes[/ame] and [ame="http://en.wikipedia.org/wiki/Calluna"]heather[/ame], layering the vegetation so as to shed water away from the inner roof. It is a very old roofing method and has been used in both tropical and temperate climates. Thatch is still employed by builders in developing countries, usually with low-cost, local vegetation. By contrast in some developed countries it is now the choice of well-to-do people who want their home to have a rustic look."

source:[ame]http://en.wikipedia.org/wiki/Thatching[/ame]
 
Mbona mashamba ya Nafco wameuziwa wakenya na ngano yote inakwenda huko, mbona hamlalamiki? Watanzania wengi tu walijitokeza kuomba mashamba ya ngano Katesh lakini hakuna hata mmoja aliye pata, wakenya wakamwaga kitu kidogo sasa mashamba ni yao.
 
mkuu Dar Es Salaam una hoja nzito sana!
kwa uzoefu wangu mdogo sidhani kama nastahili ku-argue na wewe
 
Kuna mahakama za Rushwa za kimataifa kama za Tanzania huziamini, unangoja nini?

Nina shaka na hiyo shule unayodai ulipelekwa na wazazi wako! Kuna mahakama gani ya rushwa ya kimataifa? Nitajie moja tu ambayo ipo kwa ajili ya kusikiliza kesi za rushwa. Msipende kudai usomi halafu maandishi yenu yakawashushua!

Amandla.....
 
Last edited:

Tatizo letu wengi hatujui maana ya neno ukoloni hivi jamamani tunaweza pata mtu akazungumzia defination ya ukoloni in very simple language labda watu wataelewa.

Watu wanadhania ukoloni ni bendera ya mkoloni ipepee kila mahali, wengine wanadhania ni magwanda na makofia ya PC na DC na au office attendant kuitwa messenger, wengine wanadhania ni kodi ya kichwa na baiskeli, lakini majority hawajui hii concept ya ukoloni.

Naomba mdau mmoja atueleze maana ya ukoloni
 

Well, nnachojifunza hapo ni kwamba uwezo wako wa kufikiri ni mdogo sana ukilinganishwa na wa Nyerere. Au ni hii pia unakataa?
 
Mbona mashamba ya Nafco wameuziwa wakenya na ngano yote inakwenda huko, mbona hamlalamiki? Watanzania wengi tu walijitokeza kuomba mashamba ya ngano Katesh lakini hakuna hata mmoja aliye pata, wakenya wakamwaga kitu kidogo sasa mashamba ni yao.

Nadhani tuanze kuangalia ni jinsi gani tunareposses hayo mashamba kupewa wakenya mashamba hayo isiwe sababu ya sisi kuendelea kutoa mashamba kwa wakorea, waarabu na watu wengine wasio na ardhi wanaokuja kutunyang'anya sisi.

Kama walipewa kwa kutoa kitu kidogo basi hii ni sababu tosha ya kutengua mkataba uliofunikwa na rushwa. Kinachofuata ni kutoa taarifa PCCB ili wafuatilie kama wanavyofanya kwenye kesi ya Liyumba wakishindwa basi tuchukue hatua nyingine za kulazimisha upelelezi uendelee.
 


ukoloni kama mfumo wa kueneza himaya na kulinda maslahi unakuja na sura tofauti, nchi moja yenye nguvu kiuchumi na kisiasa kuinyonya nchi masikini

zamani ilikuwa mkoloni anaitawala nchi nyingine katika kila nyanja, lakini enzi hizo zilishapita. kwasasa ukoloni umejikita kukomba maliasili za nchi kama Tanzania.

Tanzania ni mfano mzuri jinsi ukoloni wa kisasa unavyotumika kuwanyonya masikini, viongozi wetu wanabisha hilo - akili zao zimelewa moshi wa madaraka na fedha.

tukumbuke kuwa hata wakati wa kupigania uhuru miaka 50 na 60, wapo waafrika waliwaunga mkono na kushirikiana na wazungu kuwakandamiza waafrika.

nadhani ushamsikia Kikwete akisema bila wawekezaji wa kigeni Tanzania haiwezi kuendelea. maana yake ni kwamba yuko radhi awafungulie milango wachukue kila wanachokitaka, kuliko kulinda maliasili zetu. angalia madini yanavyochotwa, angalia ardhi inavyouzwa, vitalu vya uwindaji wanagawiana waarabu.
 
Prime Minister Pinda should come clean on this, atwambie anajua nini kuhusu huu mradi.Na yeye alipokua Korea walizungumza nini na hao wenyeji wake kuhusu swala la ardhi. Vinginevyo hii kitu ni swala muda tu, watakuja watafanya wanavyotaka na tutanyamaza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…