Ni kipi ambacho sisi hatuwezi kukifanya kati ya hivyo na kwanini hatuwezi?
Mkuu MM,
Heshima kwako mkuu!
Kwa muda mrefu sana, pengine tokea tupate uhuru, hilo ndilo swali ambalo limekuwa likitushinda kujibu. Ni ama hatutaki kujishughulisha nalo, au ni kweli tumeamua kushindwa kuitumia ardhi na maji mengi tuliyonayo ipasavyo.
Ardhi na maji tele, vimeshindwa kutumika kupunguza umasikini na kukuza uchumi kwa taifa ambalo 80% ya watu wake wako vijijini. Kwa nini, wakati huu ambapo teknolojia ya kilimo ipo kila mahali?
Watanzania ni watu wenye character ya pekee mno inapokuja kwenye ujenzi wa uchumi. Tunapenda njia za mkato, maneno mengi, na kulaumu wale wanaoonekana kutuzidi au kutaka kutuzidi.
Wenzetu wakitumia advantage ya kuwa jirani na Mlima Kilimanjaro, tunalalamika, wakati sisi hatuitangazii dunia ije kuupanda.
Wakati upatikanaji wa nishati ya umeme ni mzozo, Ngeleja anasema "hatuwezi kuangalia uranium kwa sasa kwa kuwa mahitaji yetu ni madogo mno kuweza kuhitaji umeme wa uranium..." hii statement inatioka kwa waziri. Hii ina maana kuwa, wala hafikirii kuuza umeme wa ziada, hadi hapo Kenya au Uganda itakapotaka kutuuzia umeme wa Uranium yao kama itakuwepo.
Watanzania wengi hatupendi kusoma na kupata maarifa mapya, ila huwa tunatafuta njia za mkato za kujitajirisha, na ndiyo maana wengi tunaangukia kwenye utapeli, tunaghushi vyeti, tunauza kura zetu, na hatupendi kufikiria na kujaribu kutumia nafasi zilizopo kujijengea uwezo. Ndiyo maana ukianzisha biashara ya maandazi leo hapa, kesho kutakuwa na wenzio watatu wanauza maandazi.
Nahisi tumekuwa so obsessed na mafaniko ya wenzetu kiasi kwamba tunasahau kuwa hata wao walianzia pagumu sana kufikia hapo walipo.
Kwa hali ilivyo, mimi bado ninaamini kuwa matumizi bora ya ardhi ndiyo suluhisho la nguvu la kuweza kubadilisha hali ya uchumi wa taifa hili...japo kuna wenzangu wanaosema kuuwa ni service industry ndiyo inayoweza kufanya hili. Kilimo bado hakina ushindani mkali duniani, hususan kwa soko la Afrika.
Nilikuwa Antwerp mwaka juzi, nikaona ndizi mbichi, nyanya na mananasi yanashushwa toka melini toka West Africa...nilihuzunika sana kuona hata hili sisi hatuwezi, na tumeshindwa kwa miongo kadhaa iliyopita. Kwa nini tumeshindwa? Kwa nini hatuwezi kutumia maji ya mto Ruvu, Ruaha, Rufiji Malagarasi, Ziwa Victoria kupata mazao, hadi wageni watake kufanya hivyo?