Korogwe: Bodaboda wadaiwa kuchoma basi la Saibaba baada ya mwenzao kugongwa

Ikithibika kwamba bodaboda ndio waliochoma hilo basi nashauri vijiwe vya boda vilivyopo karibu na eneo la tukio wajipe likizo au watafute pahala pengine pa kufanyia shughuli zao kwa muda.

Sent from my SM-A042F using JamiiForums mobile app
Sio likizo tu wahame ila haitowasaidia watakamatwa kama kuku
 
daaahhh,mbona boda mmefika mbali sana
 
Kwakua ,Masikini Hana Haki katika mahakama zetu, sana sana Mmliki wa Bus Hilo bado angetafuta kunyonya Ndugu wa marehem, yaaan umegonga, umeuua, na Bado ulipwe fidia wewe.



Niwapongeze Bodaboda Kwa Hatua hii nzurii na ushirikiani wao Hadi kufanikisha Kuchomwa na kuteketea teketeke Kwa Bus hili


Ndiooo masikini tuna Roho mbayaπŸ˜…πŸ‘Œ


Pumzika Kwa Aman Degree Holder, ulosomeshwa, Ajira hamna, ukaamua kujiajiri na sasa umeondoka.
 
Maua upewe
 
Sawa hao bodaboda wamekosea kuchoma hilo basi ila madereva wa mabasi ni washenzi sana yaani wanacheza rafu barabarani hatari. mimi nikiona basi naweka chombo yangu pembeni namuachia njia nyeupe.
kweli kabisa, wana vurugu za speed bila kuangalia wako wapi
 
oya ilishatokea kigamboni jamaa aligongwa na bonda taa za nyuma zikapasuka alikua na crown boda akataka kusepa jamaa akampelekea ngoma basi boda wakaanza kumkimbiza alikua anawafuta anakimbiza anawasubiri wakitaka kumpita anawapeleka mtaroni tukio lilikua usiku road ya kutoka mikadi mpka mji mwema kile kipande watu walilazwa sana mtaroni ....
jamaa wa crown alitoa sadaka maana kagongwa akaona bora apeleke moto nilikua naenda ferry tukio lilikua kama movie ilibidi niingie lembeni ya barabara kupisha maana nilikua naona toka mbali wanavyopigwa pembeni
 
Wakikamatwa wakalipe watauziwa hadi viwanja vya babu zao
 
jamaa mwingine alitaka kusababisha ajali lakini haikutokea akashuka akaomba msamaha boda wakaona wanamuweza wakazuia gari yake jamaa akaona hakuna tena amani gari imeanza kupigwa bodi inagongwa gongwa akafungua kioo akapiga ngoma juu mbili tu boda walitawanyika nilicheka sana siku hiyo japo jamaa alikua msataarabu ila boda wakaona sio kweli hatimaye wakatawanywa πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

kuchukua sheria mkononi kwa boda ni kawaida sana wanahasira za ghafla wanaona kama kundi linaloonewa sana inabidi serikali wairasimishe hii kazi na waweke misingi ya kuwabana vituko ni vingi na wengi wanaishia kuumia hata kwenye sheria bado wanaumia...


unakuta boda kakugonga hata leseni hana hiyo bima ndio hajui inarangi gani mambo ni mengi ila serikali iache kuwatumia kipindi cha uchagizi wawarasimishe watu wafanye kazi
 
Haki ikikosekana mahakamani, yanayofuata ni haya.
 
Kwahiyo hapa abiria wakashuka wakala pembeni wakishudia Maafisa Ubashiri wakifanya Yao, mpaka wanashusha mizigo hakuna hata alieonyesha juhudi ya kuita polisi maana pale Msambiazi ni hatua chache toka Korogwe stand wangeweka road block Kwa boda zote zinazotoka Msambiazi labda kama waamue kwenda Mombo nako wangekamatwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…