Kosa gani la kifedha au kiuchumi ulilifanya ukajutia?

Kosa gani la kifedha au kiuchumi ulilifanya ukajutia?

Ushauri wa bure.

Ukipata hela nyingi ambazo hukuwahi kuzishika, weka kwenye fixed kama miezi sita hivi ukitafakari nini chakufanya.

Inahitaji hesabu kali sana kukopa bank na kujenga nyumba ya kuishi.

Usiende bar kwenye starehe na hela nyingi mfukoni, kadi ya bank na Salio kwenye Mpesa.
 
Naamini kwenye hizi bar na hawa madada wakwenye starehe huwa kuna uchawi mwingi sana, TUWE MAKINI SANA.

Ngoja nitafakari kama ninaweza kuweka kisa fulani cha kufundisha watu.

MUHIMU: USIENDE BAR UKIWA NA HELA NYINGI.
 
Kutumia 70m kwa miezi miwili tu, ikaniacha nimeongezeka uzito. Najutia sasa nina kazi ya kupunguza uzito usiotoka kirahisi kama ulivyoingia 🥲🥲🥲🥲🥲 na hela inaniuma nimepoteza pia.
☕️
 
Pole sana watu kama nyinyi humu mpo. So kama wewe huna ndiyo kila mtu hana, sikulazimishi kuamini. Ila wanaonijua nje ya JF humu wako wengi watakuona hater tu. Mmezoea kudanganya unajua kila mtu anadanganya.

Bob naishi maisha halisi, ningekuwekea na bank statement kama ingekuwa salama hapa. Punguza wivu kijana siyo kosa langu wewe kukosa pesa. Pole...
 
Ukichukua mkopo miaka 5-8 maaana yake riba ni 70-80%

Piga hesabu nyumba ya mil 100 utashangaa imekucost mil 200-250

Bora uanze kujenga mdogo mdogo ukope kumalizia mkopo usiozidi 3 yrs
 
ndio nina mkopo wa milioni 80 na bado hiyo nyumba nayojenga sasa hivi haijaisha ila hela imeisha, yaani presha na kisukari huwa vinakutana katikati ya kitovu.
Hii comment imeniacha hoii eti kisukari na pressure vinakutana katikati ya kitovu
 
ndio nina mkopo wa milioni 80 na bado hiyo nyumba nayojenga sasa hivi haijaisha ila hela imeisha, yaani presha na kisukari huwa vinakutana katikati ya kitovu.
Huku jua cost kabla ya kukopa mkuu au ulichepusha km kawaida yetu?
 
Nilipochukuwa mkopo wa milioni kumi na kutakiwa kurudisha milioni kumi na sita ndani ya miezi sita.
Hebu weka nyama Mkuu 😂ulisaini mwenyewe au ulisainiwa fomu?
 
Back
Top Bottom