Kosa kubwa atakalolifanya Makonda ni kutolipiza kisasi

Suzy Elias

JF-Expert Member
Joined
Nov 9, 2021
Posts
1,067
Reaction score
6,200
Kwanza ieleweke, kisasi ni haki!

Kwa namna Paul alivyotengwa na kunangwa, kutwezwa na hata kusilibiwa na mahasimu wake kipindi alipokuwa hana kazi ni wazi kama lipo kosa atalitenda ni kutolipa kisasi kwalo.

Paul, kwanza anapaswa aelewe watesi wake walianza kumtafutia namna ya kummaliza tena tokea waliposikia tetesi ya kurejeshwa kwake.

Paul, pili atambue vita vimhusuzo sasa ni zaidi ya vile vilivyopita hapo nyuma!

Paul, tatu asithubutu kumwamini yeyote awaye baada ya fursa ya kiuongozi aliyoipata kwa mara nyingine.

Mwisho ( na si kwa u-muhimu ), Paul ni lazima alipe kisasi cha haja na kuwatenga mbali watesi wake ili kuwanyima wasaa wanao weza kuutumia kumwangamiza kwa ukaribu alio nao sasa.
 
Aanze na nape ndo aliyehonga pesa ili makonda apelekwe mahakamani kama sio kupotezwa kabisa
 
Asisahau kulipa kisasi Ben Saanane,Lissu......
 
Yaani muhalifu alipe kisasi?
 
Ajaribu aone,nyie mjazeni ujinga tu
 
In politics, there is no permanent enemy...
 
H
Hiyo ni mojawapo ya kanuni za kwenye siasa... ukipata fursa ya kumtandika opponent wako unamtandika kisawa sawa asiweze amka tena. Kama vile Yanga FC ilivyo mtandika Simba FC 5G.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…