Mtu anayekufa siku zote huwa hajui. Ccm inakufa na haijui. Mwaka 2014, K/ mwenezi alikuwa Nape na Katibu mkuu Kinana.
Kinana alitaja orodha ya mawaziri mizigo zaidi ya saba, mmojawapo Prof. Maghembe na awamu ya tano pamoja na kutajwa ndiye aliyekuwa Waziri wa utalii wa kwanza wa JPM.
Ukichanganyikiwa unaweza fanya chochote, kwani huyu mama aliyekuwepo alikuwa na vigezo gani vya kupewa hiyo nafasi? Ni kweli ccm ilijiridhisha kuwa Mh.Mjema anaweza hiyo nafasi!! Sasa hawa waliompa Makonda ndio hao hao wanasema Makonda anafaa. Makonda hana tofauti na Muimba taarabu, na ushahidi ni alivyoanza leo. Yaani target yake kubwa ni Mbowe Wala siyo Chadema.
Makonda siyo mwanasiasa anachoweza ni utawala tena wa mabavu na kusaidiwa, kama alivyosaidiwa na Magufuli kwa kupewa majambazi wa kutembea naye,maana haingii akilini na hatutaki kuamini kuwa wale aliongozana nao kwenda cloud kufutilia flash ya umbea ni askari wetu kweli!!
Bila Magufuli Makonda alipata wapi mamlaka ya kumtishia/kumuamrisha IGP Siro!! Kwamba leo usikue Chalamila anamfokea Wambura!! Bila Samia kuwa nyuma yake!!
Tunachoomba mama Samia asivuruge utawala wa sheria na haki kwa kuiga mambo ya mtangulizi wake japo aliwahi kusema wao na Magu ni kitu kimoja.