Kosa kubwa la Malecela wa NIMR: Rais kaona mbali athari za ZIKA

Suala ni kwamba hajaishirikisha Serikali ili kuipika taarifa na isingetangaza. Mi naona ni vema kujihami hasa kwa magonjwa mapya kumbukeni wenzetu walivyopata EBOLA madaktari wa Dunia nzima walienda kupiga kambi West Africa.
 
Haya nao TWAWEZA tafiti zao pia zipate baraka za serikali!! Hii ipo Tanzania tu
 
pia utafiti wake ulikuwa ni wa awali tuu na haukuwa wa kufanya hitimisho kuwa nchini kuna Zika.
 
ulisikia watafiti wa uganda wamekurupuka kutangaza kwenye media
 
Hivi huyu....nae pia Anna kilango Malecele ni ndugu yake
 
Ni kweli, tunapaswa kujua ili tuchukue tahadhali. Lakini tulipaswa kujua kwa namna ambayo haitaleta image mbaya kwa jamii ya kimataifa.. unadhani ni vizuri uwekewe vikwazo vya kusafiri kwenda nje kwa sababu inch imejulikana kuwa na zika? watalii wote kubadilisha route na kuikacha Tanzania? wawekezaji kuikacha tz kisa zika, wakati imekuwemo siku nyiiiiiiiiiingi na wala haijaleta madhara makubwa? kwa nini wasingetumia njia nzuri kuwaambia watanzania na sio kuleta sintofahamu kwa jumuiya za kimataifa?
 
Mnataka watu wafanye tafiti kisha wasiziseme? Kwa faida ya nani
 
NIMR ni Taasisi ya wapi? Nani ni serikali? Yapi ni majukumu ya NIMR na yapi si majukumu yake Kwa mujibu wa Sheria?

"Think before you act"
 
Kuna tofauti kati ya kutangaza matokeo ya tafiti na kutangaza mlipuko wa ugonjwa.
Alichokifanya yule mama ametangaza matokeo ya utafiti ambao tahasisi yake imefanya....
Nilitegemea Waziri mwenye zamani aje kwa ufafanuzi kama huo mtoa mada ulioutoa...Kwanza wazili akitakiwa kuikubali tafiti then atueleze kuwa imezibitiwa /ipo kwa kiasi kidogo etc
 
wanapewa madaraka ya nini kama hawaruhusiwi kutoa tafiti zake? basi taasisi zote ziongozwe na kurugenzi ya ikulu.
Mbona na ww unakuwa mjinga kiasi hicho jamaa hapo katoa ufafanuzi mzuri kwamba kuna utaratibu unatakiwa kabla ya kutangaza tatizo kama hilo ikiwapo pamoja na kuijulisha serikali na WHO, watz mbona wengine uwezo wa kuelewa ni mdogo sana au unafurahi kuchangia bila hata kutafakari au ndiyo mlioajiriwa kukosoa kila kitu ? Very stupid
 
Mleta mada umepotosha pia.

Dr.Mwele Mallecela alitoa matokeo ya Utafiti uliofanywa na NIMR. Na utafiti ule ulikuwa unataka kujua Uhusiano wa watoto wanaozaliwa na vichwa vidogo hapa Tanzania na maambukizi ya Zika hapa Tanzania. Ambapo matokeo ya utafiti huo kuonyesha kuwa katika sampuli zaidi ya 500 zilizofanyiwa utafiti, Zaidi ya 15% walikuwa na Maambukizi ya Zika. Hitimisho la utafiti ule ni kuwa Homa ya Zika IPO(Endemic) hapa Tanzania na hivyo hatua zaidi zitapaswa kuchukuliwa.

Hakuna mahali popote ambapo Dr.Malecella alitamka kuwa kuna MLIPUKO(Epidemic) wa Zika hapa Tanzania.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…