Duh hakika jamiiforums ni wide forum,tunae hadi Mrusi humu ndani!.?Ndio hivyo tena, majimbo tushachukua kwanguvu na hamuwezi kufanya kitu na wambieni hao wapuuzi wenu wasogeze pua waone kitakachowapata
Unatakiwa ujue kuwa hao Wayahudi unaowaona miungu watu wako neutral kwenye mgogoro huu. Israel ina maslahi na Urusi kuliko Ukraine na Israel ndio bingwa wa kufanya annexation na Urusi yuko balaza la Usalama la UN akiwa na Veto power. Israel sio mambwiga kununua ugomvi huu, the same na China ambao wanaangalia uwezekano wa kuzichukua Hong Kong na Taiwan.Dunia inaangalia mchango wako ni upi. Substance ya kwako ni ipi. Myahudi anao mchango kuanzia masuala ya teknolojia mpaka yale ya muziki.
Kulialia tu na kulalamika ni sifa ya mwafrika, ambaye siku zote anahisi kuwa anaonewa, ukiwa na mchango katika uhai hutalia kuonewa, unachokichangia ndio kitakachokupa heshima.
Crimea ilikuwaje ?Ukraine ni nchi huru it is a sovereign state, halitakwenda Russia kirahisi tu.
Ukraine ni nchi huru ukumbuke hilo usilinganishe na masuala ya Golan Heights za Syria. Israel alizichukua baada ya kuchokozwa. Mukraine hana uwezo wa kuvamia na kuteka eneo la nchi nyingine.Unatakiwa ujue kuwa hao Wayahudi unaowaona miungu watu wako neutral kwenye mgogoro huu. Israel ina maslahi na Urusi kuliko Ukraine na Israel ndio bingwa wa kufanya annexation na Urusi yuko balaza la Usalama la UN akiwa na Veto power. Israel sio mambwiga kununua ugomvi huu, the same na China ambao wanaangalia uwezekano wa kuzichukua Hong Kong na Taiwan.
Alichofanya Russia kina tofauti gani na Israel kuchukua Gola Heights za Syria, Eastern Jerusalem na maeneo ya Jordan? Na ujue Russia ina Wayahudi wengi kama ilivyo Ukraine, sasa sijui kwanini unamuona Zelenskiy kama special
Hongereni sana.Sisi hao [emoji23][emoji119] walete chokochoko waone
Mimi wala siamini kama tatizo la Putin ni Ukraine. US wanapolia kuwa Russia inaingilia chaguzi zao ni kupitia njia kama hizi.
Uwezo mkubwa wa Putin kiakili na uzoefu wa kijasusi ni tishio kwa ustawi wa US.
Last time i checked crimea was part of ukraine.
Ila huyuhuyu Putin aliichukua na Us wakaingia mitini.
Mmeshachukua majimbo sio😂😂😂.
Mkuu Amagedon hiyoWanasiasa hufanya makosa mengi sana wakiwa madarakani. Wanapoyafanya huwa hawana uwezo wa kupima ukubwa na madhara ya wanachokusudia kukifanya. Ni pale wanapokuwa wanapokea lawama nyingi ndio hujisumbua kuangalia kwa kina namna ambavyo wangeweza kuzuia kile walichokifanya, wangefanya hivi na wakafanya vile ndio huwa ni wazo lililochelewa wakati wake. Wanapokuwa wakiamua kufanya maamuzi yanayoongozwa na upofu au ulevi wa madaraka huwa wamezungukwa na wapambe wanaosema kitu wanachotaka kukisikia. Wao kuwa na maamuzi ya mwisho wakati mwingine huwanyima ile busara ya kuwa mawazo yao sio kila wakati huwa ndio ya kutekelezwa na yakaja na jibu lililokusudiwa na lenye faida.
Rais wa Russia Vladmir Putin anataka kufanya kosa litakalompa umaarufu mbovu kama ule aliokuwa nao Adolph Hitler mwaka 1939. Putin anataka kufanya kosa kama lile alilolifanya Idd Amin mwaka 1978 kwa kuivamia sehemu ya mkoa wa Kagera, kipigo alichokipata kilimpoteza kabisa miongoni mwa viongozi wa mataifa waliostahili heshima kila walipokatiza. Putin ameiangalia Ukraine katika udogo wake kwa kuilinganisha na Russia hivyo anaamini kwamba anaweza kufanya lolote na dunia ya sasa ikatulia tu na kumtazama. Kitakachompata kitakuwa ni fedheha kama ile iliyomkuta Hitler ambaye aliishia kujinyonga baada ya vita kumalizika akiwa ameshindwa vibaya.
Anatakiwa kukumbushwa kuwa Volodymyr Zelensky licha ya kuwa ni rais wa Ukraine taifa huru lenye maamuzi huru kama ilivyo Russia pia ni myahudi. Kwa asili ya wayahudi huwa ni watu wenye mtandao ulio hai na makini siku zote. Wayahudi wanajuana popote walipo, na mwanasiasa ambaye hata kama upande wa Mama ndio wayahudi huwa wanamchukulia kama ni mtoto wao. Wayahudi wanalinda ushawishi walionao duniani kote. Na ni rahisi kwao kumpachika jina la 'anti semitic' yoyote yule anayekwenda kinyume na falsafa zao au anayewakejeli.
Sembuse maamuzi ya Putin kuivamia nchi huru ya Ukraine inayoongozwa na myahudi mwenzao!!. Putin anakosa washauri wenye kutazama mbali, wenye ushawishi wa kidunia. Atumie busara sana kwani anachofikiria dhidi ya Ukraine kinaweza kumpoteza kabisa na yale yote aliyokwisha kuyafanya tangu 1999 alipoanza kuongoza Russia yakafunikwa na huu 'ujinga' anaouwazia kwa sauti ya juu.
Ulimwengu wa 1939 wakati Hitler akiivamia Austria sio huu wa 2022. Zimetungwa sheria nyingi za kimataifa zinazolinda uhuru wa kila taifa. Wamezaliwa wanasiasa wenye maarifa mazito ya kuongoza. Sayansi haijabaki nyuma zimeundwa silaha za hatari zenye kuweza kuangamiza kila kilichopo juu ya uso wa dunia ndani ya saa chache tu. Anaumizwa sana na ushawishi wa USA kwa jirani yake wa karibu, lakini nguvu nyingi hutumiwa na mwenye maarifa madogo ya uongozi.
Sasa Syria, Jordan na Lebanon ambako Israel imechukua maeneo yao sio nchi huru? Egypt ambayo Israel iliinyang'anya Sinai peninsula na wakapigana ikarudi kuwa mikononi mwa Egypt sio nchi huru? Au Palestinians sio ethnicity inayojitegemea, mbona Israel haiwatambui makazi yao.Ukraine ni nchi huru ukumbuke hilo usilinganishe na masuala ya Golan Heights za Syria. Israel alizichukua baada ya kuchokozwa. Mukraine hana uwezo wa kuvamia na kuteka eneo la nchi nyingine.
Putin hana nguvu ya hoja, hana watu wenye kuweza kufanya mawasiliano na wakaeleweka.
Wajue mustakabali wa nchi yao unapoishia ndipo mstakabali wa nchi nyingine unapoanzia...Ukraine waachiwe waamue mustakabali wa nchi yao bila kuzongwa-zongwa na Urusi au Marekani.
Bado kidogo 😆😆Mkuu Amagedon hiyo
Eti Atlantic organization inataka kujitanua hadi mpakani mwa Russia!Huwezi Ruhusu Ukraine iwe chini ya NATO ,ukijua NATO ni maadui wako na Kwamba ulichukua jimbo La Crimea kinguvu .
[emoji23][emoji16]Alifanya ivo Georgia, amefanya Crimea, akafanya Moldova, na atafanya UKRAINE.....Putin anajua anachofanya na NATO haitafanya kitu.
Huwezi Ruhusu Ukraine iwe chini ya NATO ,ukijua NATO ni maadui wako na Kwamba ulichukua jimbo La Crimea kinguvu .
What if Ukraine chin ya NATO wakataka kurudisha Jimbo la Crimea kinguv?? Maana yake V.Putin atapambana na NATO.
Kipi bora?? Kuwazuia waukraine wakiwa nje ya NATO au Usubiri Ukraine wawe ndan ya NATO??
Naungana na Warusi wote Dunia nzima, waichabange Ukraine.
Ukraine ikiachiwa ijiamulie mambo yake kama ambavyo unasema, itarejea katika ambitions zake za kujiunga na EU kuimarisha mahusiano ya kiuchumi, kisha watapeleka maombi ya kujiunga NATO kwa mara nyingine kama jinsi ambavyo nchi za ukanda wa Baltiki zilifanya. Baada ya hapo, tutarejea 'square one' tukijadili mgogoro huu...mimi siungi mkono Urusi au Marekani ktk mzozo huu.
..wote wako kwa maslahi ya nchi zao na sio maslahi ya Ukraine.
..Ukraine waachiwe waamue mustakabali wa nchi yao bila kuzongwa-zongwa na Urusi au Marekani.