Labda namna ya kuwasilisha ujumbe ilikuwa si nzuri, kama ni washkaji haswa Yani unajua Kuna ule ushkaji ambao ni kama ndugu wa familia Hadi mnatukanana na Wala hakuna anayemind ndo kwanza vicheko aina hii ya ushkaji ndiyo nzuri ya kurekebisha vitu kama hivyo direct kwamba " hichi kitanda hebu badilisha Mzee, acha ufala Hadi muuza maji anakushinda" then vicheko.
Kuna ule ushkaji wa kufahamiana tu ka mabroo, mmekutana tu mkaanza urafiki ambao uko deep nao ila si wa kindugu ule, Kuna namna ya kutumia lugha kusolve mambo kama hayo ya rafiki yako, kumfikishia ujumbe.
Ukiona huna ule urafiki wa kindugu na mtu basi achana na mambo ya kumshauri directly, kutumia lugha ya Moja Kwa Moja kwenye mambo kama hayo, watu wanapitia changanoto nyingi kwenye maisha labda huyo ana mipango yake mizuri nk, watu wengi wako weak emotional hivyo ni rahisi kuudhika na kukasirika pia,Bora hata ungemwambia bro "Kuna kitanda kinauzwa cha futi sita nk, kama utakitaka nimcheki jamaa, nimekicheki kizuri kinoma, ukikidaka hichi itakuwa unyama bro mana jamaa alinicheki nimtafutie mteja nkaona ngoja nimwambia bro wangu hapa Yani ile lugha za vijana na mbwebwe za maneno kibao ya kijanja ya kuzuga, yy ni mtu mzima ataelewa.