Kosa langu nini ni Vannesa?

Kosa langu nini ni Vannesa?

KOSA LANGU NINI NI VANNESSA [emoji174] [emoji3590] [emoji3590]

SEHEMU YA 9

Wiki mbili za mama yake kuwa Tanga tulizitumia vizuri sana maana alihamia kwangu mazima . Kasoro pekee ya Vannesa ni kwenye mapishi zaidi ya kupika wali tena kibishi vingine vilimzingua . Mimi nilimzidi hapo kwenye mapishi sio utani nipo vizuri , napika wali , pilau , ndizi, ugali, tambi , mtori , kiburu ngararimo , mtango na vinginevyo. Maisha ya zile wiki mbili yalinizamisha sana kwenye mapenzi kuliko kawaida tulizurura ma club mengi bar na kila sehemu tulipoona pamechangamka na kwa kiasi kikubwa zaidi hela yake ndio ilihusika .

Baada ya wiki mbili zile alirudi kwao mama yake alikuwa arudi siku inayofuata. Alivyoondoka tu nilianza kuhisi upweke wa hali ya juu nilikaa kinyonge isivyo kawaida nikawa angalau tuna chart mpaka usiku ila ilikuwa ngumu sana kuzoea ile hali ya kulala mwenyewe na kuwa mwenyewe getto.
Umbali ulizidi zaidi baada ya kumaliza semister ya kwanza likizo ile muda mwingi alikuwa kariakoo na walirudi wote na mimi nilienda kukaa kwa uncle msakuzi tukawa tumepumzika hivi maana tulikuwa moto sana penzi letu lilikuwa stori ya mtaa pale . Pisi niliyomiliki ilikuwa sio ya kitoto anayeimiliki lazima awe na kaumaarufu flani .

Sasa siku mbili kabla ya kwenda kuianza semister ya pili si nikawa nimerudi kwenye getto langu . Akagoma kwenda kazini na mama yake akaja getto aisee hiyo siku tulizini kama hatutakaa tuzini tena tulifanya mapenzi kwa kasi sana alikuwa anaizungushia mauno utadhani siku hiyo alikula cha arusha mimi mwenyewe siku hiyo siku poa nilirusha mabomu kuhakikisha navunja safu ya ulinzi. Nilishambulia kama sitakaa nipate tena nafasi hiyo . Mpaka tunamaliza kila mmoja alikuwa hoi tukawa tunaangaliana tunacheka kwa tulichokifanya . Siku hiyo tulishinda wote akarudi home kesho akaja tena kama kawaida


Kosa langu lipo wapi?


Final inakuja . Utaniambia nilikosea wapi basi. Saa 4 kamili
 
Bado hujasema… malizia hiyo episode tufahamu ulikosea wapi.
 
KOSA LANGU NINI NI VANNESSA [emoji174] [emoji3590]

SEHEMU YA 10 FINAL...
.
MWISHO USIACHE KUNIAMBIA LABDA KUNA SEHEMU NILIKOSEA ALAFU MIMI SIJASHTUKA [emoji3531]

Tuendelee

Mahusiano yetu yaliendelea mara kadhaa tukiishi wote mpaka alivyomaliza diploma ila kabla hajamaliza . alianza kubadilika na kuwa mtu wa huzuni . Sio yule Vannesa niliyemzoea baadae nilijagundua ni mjamzito nilishtuka sana . Maana sikutarajia kwa ujanja alionao angezembea abebe mimba . Akawa mtu wa kulia sana . Nilimbembeleza nikimwaminisha hakuna kitakachobadilika lakini hakuna jibu nililopewaga na mpaka leo sijui na siamini kama ni mimba kuwa inamliza

mwezi mzima nilipewa mara mbili na Nilipewa kinyonge sana nakuondoka . Nilijiuliza sana sana tatizo nini ila nilikuwa nauchosha ubongo bure sikupata majibu. Mimi mwenyewe nilipoteza furaha kabisa. Nikawa kama nimeganda hivi sio kwa sababu ya mimba hapana kwa sababu ya kupoteza kabisa utani tabasamu mazoea na uchangamfu aliokuwa ananiletea Vanne... hapa tu tayari nilianza kuonja maumivu ya kumpoteza kipenzi changu.

Sasa baada ya kama mwezi siku moja akiwa ashamaliza diploma ( nilisahau kuwaambia mrembo alikuwa anaitafuta diploma )alikuja ghafla getto . Alikuja analia mfululizo alivyofika tu akanirukia na kulala kifuani kwangu nikafunga mlango kwa mguu nikasogea nae mpaka kwenye sofa na kujaribu kumbembeleza huku nikimwomba aniambie kinacho msibu akawa ananiangalia usoni tu na kuongeza kulia .

Nilijikuta nikilia pia [emoji24][emoji24] tena machozi yakitoka kwa kasi ajabu nikihisi labda mimi ndio sababu ya yeye kuwa kwenye hali ile akawa ananifuta machozi nikamuuliza kosa langu nini ni Vannesa hakunijibu. Nilimkumbatia nikizidi kumuuliza lakini wapi mpaka leo sijawahi kujua kwanini alibadilika vile . Nikajaribu kumtajia ni mimba akatikisa kichwa kuashiria hapana na kuongeza kulia kwa kweli nilijikuta nalia pia kama nimefiwa .
Baada ya muda aliinuka ghafla . Akiwa amenyamaza akataka kutoka kufika mlangoni . Akaanza kuniambia nakupenda sana . Wewe ni mwanaume wapekee niliyekupenda kwenye maisha yangu. Akanikumbatia . Akaniambia najua unanipenda sana pia ila hakuna namna .

Moyo wangu ulihisi jambo baya machozi yalianza kutoka mpaka leo hii sijawahi tokwa na machozi hivyo. Akajitoa kwenye kukumbatiana akanipiga kibao cha wastani tu akiwa ashafuta machozi yake na nikawaida yake akitaka umakini. nilikuwa nishamzoea akarudia kingine kikali cha kuuma kabisa akaniambia unaweza kuishi bila mimi jitahidi kujipenda na kujilinda usiwe malaya sawa . Hapo tayari machozi yalianza kumlenga nataka kumkumbatia ili nimuulize tena shida nini akarudi nyuma na kuanza kukimbia nilimfuata mpaka nje ya geti nikilia sana . Akanigeukia tu uso wake ukiwa umefunikwa na machozi huwezi kuamini kama ni yeye . mimi nilikuwa nimemzoea usoni mda mwingi ni kutabasamu tu ila leo sura yake ili funikwa kwa machozi na huzuni tele alibadilika rangi na kuwa mwekundu . Hata mwili wake ulikuwa umepungua sana ndani ya mwezi ambao kuwa simwelewi.

Basi ndio sura iliyobaki kwenye akili yangu mwishoni akilia machozi yakishuka kinoma akanipungia mkono wa kwaheri na kusepa. sikuweza kumfuata zaidi kwani nilitoka peku sikufunga mlango na ile hali ya kulia ilibidi nilirudi tu ndani nisionekane na kadamnasi. Nilibaki Nikiumia na kuwaza mengi sana nikaanza kuwaza labda amepima ukimwi nini kakutwa nao na kaona nitamlaumu yeye au. Nilijiuliza sana nikaamua kwenda kupima . Majibu yakawa hakuna. Na angekuwa nao ningepata tu kama kuwa hatumii dawa na match za kibabe zisizo na fair play lazima ingekuwa balaa . Siku hiyo nilikosa usingizi kabisa kuwa sielewi nini kinaendelea

Sasa asubuhi na mapema kesho yake . Nilikuta meseji imetumwa saa nane usiku. Alituma Vanne. Inasema " Nitakuwa mbali ,mbali sana naomba usijitese kabisa endelea na maisha jiamini hakuna mwanamke wa kukukataa wewe naomba naomba sana uendelee na maisha. Jana nilitaka ulie ili nikiondoka usilie tena naomba iwe hivyo usilie wala kuwa na huzuni "
Daah sijui aliwaza nini meseji ndio kwanza ilinipa kilio acha nikiri tu nililia sana
Hiyo ndio meseji ilikuwa ya mwisho kabisa laini aliitelekeza mpaka ikafungiwa na account zake za social media alifuta zote mpaka email. Kwao nyumba ili uzwa usiku alionitumia meseji ndio kuwa wanaondoka hivyo sijui walipo sina fununu zozote nimefuatilia mpaka singida , Tanga nimefeli

meseji yangu ya mwisho kwake ilikuwa kosa langu nini ni Vannesa?. Kwanini unataka kuniacha mwenyewe. Kosa langu nini?.

Mpaka leo hii sijibiwi?.
Akaniacha mpweke zaidi ya mpweke mkiwa zaidi ya mkiwa nilichanganyikiwa balaa .

Chuo nilienda kinyonge sana kila nikipitaga hiyo njia kumbukumbu zinanijia nilivyokuwa natembea nipo nae. Nikawa na mwona kwa mawenge niliyokuwa nayo nilipoenda jengo tulilokutana sana mgahawa tuliokuwa tunakula ulikuwa ni mtihani sana .

Kila siku najiuliza kosa langu nini ?
Nimiaka miezi siku kibao zimepita hata kunitafuta mara moja tu hanitafuti . Hata nijue tu kosa langu haniambii.
Naumia sana .

Kwanini basi ulinifundisha kupenda ?
Kwanini ulinionjesha penzi nikiwa kwenye kilele cha furaha ukanitelekeza ?

Kiukweli nilichelewa sana kununua nguo kwani wakati wote tulikuwa pamoja karibu miaka miwili sikununua nguo bila yeye na yeye ndio alikuwa ananichagulia kila nilipotakaga kununua nguo nilishindwa kabisa kujiamini kama hiyo nguo itanipendeza . Mwaka na miezi nane ilipita bila mimi kunua nguo mpya zaidi ya kudandia za wadogo zangu wawili ambao tunalingana kabisa kimo na unene ukituona utadhani mapacha nilitaka kujirudisha alikonitoa kuvaa ovyo . Au kiheshima sana kujaribu kumsahau lakini wapi ikawa kama kukimbia kivuli changu mwenyewe.

Kiukweli baada yake nilishalazimisha mahusiano kadhaa lakini wa kumfikia hata robo Vannesa wangu hakuna .

Miaka inaenda naogopa kuoa mwanamke ambaye moyo wangu haumpendi licha ya kuwa anatabia njema na sura nzuri. Na kadata sana kwangu. Na kumwacha a move on namwonea huruma na sioni mbadala wake yupo vizuri tu

Hebu nishaurini kwa hili la kuoa huyu mrembo ambaye anaingia kwenye maisha yangu ila moyo wangu katoweka nao mrembo Vannesa . Nimwoe hivyo hivyo au niendelee kumsubiri Vannesa


Swali la pili . Ile mimba naamini ni yangu je atakuwa alienda kutoa au mtoto yupo? Na kama yupo kwanini hamleti ?

Swali la mwisho kwa ulivyosoma
KOSA LANGU NINI?

[emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]
 
1st of all, kwann hukumuuliza kama mimba ni yako?? Au uli assume tuu itakuwa yangu??

2nd, mwanaume kuulizauliza kila mara "kosa langu nini" bila kujibiwa ni udhaifu, ukishamuuliza mwanamke "kosa langu ni nini" usipojibiwa bac jua wewe huna kosa, kuulizauliza kila mara inakera.
 
Dah pole sana Mkuu…
Umeandika ukiwa na maumivu bado. Kisa chako kinagusa sana.

Binafsi nakushauri usahau maana huna jinsi, huwezi kusubiri kitu ambacho hakipo mikononi mwako.

Wengi tumepoteza warembo tunaowakubali bila sababu kuwekwa wazi na tukachagua kumove on tukivinjari na mafungu mengine tuliyopangiwa.

Hili nalo litapita.
 
dah hii episode ya mwisho nimelia sana
why Vanessa why 😭
 
anyway Vanessa yuko uarabuni kaolewa na mwarabu kwa sababu ya tamaa zake mwenyewe wewe huna kosa lolote ni ivo tu umekuwa replaced as always nikushauri tu oa uyo mwanamke msahau vanessa
 
Aisee,ushauri wangu..kubali ukweli na uoe huyo mwanamke
 
1st of all, kwann hukumuuliza kama mimba ni yako?? Au uli assume tuu itakuwa yangu??

2nd, mwanaume kuulizauliza kila mara "kosa langu nini" bila kujibiwa ni udhaifu, ukishamuuliza mwanamke "kosa langu ni nini" usipojibiwa bac jua wewe huna kosa, kuulizauliza kila mara inakera.
Niliamini mimba itakuwa yangu. Nilimuuliza tatizo ni mimba ? Akatikisa kichwa kuashiria kukataa. Ni ngumu sana mimba kuwa ya mwingine maana mda mwingi tulikuwa wote tukiwa mbali tunachat
 
Dah pole sana Mkuu…
Umeandika ukiwa na maumivu bado. Kisa chako kinagusa sana.

Binafsi nakushauri usahau maana huna jinsi, huwezi kusubiri kitu ambacho hakipo mikononi mwako.

Wengi tumepoteza warembo tunaowakubali bila sababu kuwekwa wazi na tukachagua kumove on tukivinjari na mafungu mengine tuliyopangiwa.

Hili nalo litapita.
Unanishaurije ni mwoe tu . Huyu niliyenaye ananipenda sana uzuri anao tabia ndio kabisaa inambeba ila ndio hivyo moyo wangu aliondoka nao Vanne ..
 
Mkuu Mashaurijr Kwanza nikushukuru kwa darsa lako la mahaba hakika usiku wa leo nimefanya kufuru kwa mengi niliyosoma kwako ,sidhani Kama huyu dada hatakuja kuniacha tena .

Ila kuhusu Vanessa ndugu kubali kumove on penzi haliwezi kuwepo tena na likiwepo si Kama lile la mwanzo kubali kuanza upya ,achana na huyo Vanessa .

Kwa kumalizia nasema tena ahsante sana kwa darsa ,sidhani Kama kelele za kuwa Sina nguvu za kiume zitaendelea hapa ofisini maana nimejua kumkomoa nesi
 
Mkuu Mashaurijr Kwanza nikushukuru kwa darsa lako la mahaba hakika usiku wa leo nimefanya kufuru kwa mengi niliyosoma kwako ,sidhani Kama huyu dada hatakuja kuniacha tena .

Ila kuhusu Vanessa ndugu kubali kumove on penzi haliwezi kuwepo tena na likiwepo si Kama lile la mwanzo kubali kuanza upya ,achana na huyo Vanessa .

Kwa kumalizia nasema tena ahsante sana kwa darsa ,sidhani Kama kelele za kuwa Sina nguvu za kiume zitaendelea hapa ofisini maana nimejua kumkomoa nesi
Nitajitahidi mkuu
 
Niliamini mimba itakuwa yangu. Nilimuuliza tatizo ni mimba ? Akatikisa kichwa kuashiria kukataa. Ni ngumu sana mimba kuwa ya mwingine maana mda mwingi tulikuwa wote tukiwa mbali tunachat
Unaamini ni yako we ndo uliibeba?

Mkuu unamwamini mwanamke??
Stop that shit
 
Back
Top Bottom