SoC04 Kosa Litakaloliangamiza Taifa Miaka Mitano ijayo

SoC04 Kosa Litakaloliangamiza Taifa Miaka Mitano ijayo

Tanzania Tuitakayo competition threads

Sam Darfur

New Member
Joined
Sep 28, 2021
Posts
1
Reaction score
0
Mashuhuda wa ajali wanasema kwamba, eneo ajali ilipotokea ni hatari na huenda kukawa na jini ambaye anasababisha ajali zitokee mara kwa mara. Wanadai kwamba, inawezekana jini huyo ndio sababu ya kutokea kwa ajali hii kubwa na hatari, ajari iliyoondoa roho za watu 65 huku watoto chini ya miaka 18 wakiwa ni 20 na watu wazima wakiwa ni 45 huku majeruhi wakiwa ni watano ambao wamevunjika baadhi ya viungo vyao na kuwa vilema. Ajari hii mbaya itasimuliwa visasi na visasi kwa sababu hata waliopona hawana tena furaha na dunia, sio abiria wala Dereva pamoja na Kondakta wake, walipoteza maisha, wote walifanya Taifa lipeperushe bendera nusu mlingoti. Je, huyo jini aliyesababisha ajali hii ni nani?


May 05, 2024, asubuhi ya saa saa tano, hali ya hewa ilikuwa imetulia huku joto likichukua nafasi yake. Maeneo ya kituo cha Mabasi Cha Msamvu, Morogoro. Dereva Mwakilaki Yohana Mwarombo, aliwasha gari yake huku akiwa na wasiwasi juu ya safari yake. Alikuwa amechoka kwa sababu usiku wa jana alikuwa na safari kutoka Dar es salaam mpaka Morogoro na sasa anatakiwa kutoka Morogoro kurudi Dar es salaam huku akiwa na abiria. Idadi kamili ya abiria ilikuwa ni 50 huku yeye pamoja na watumishi wake wanne wangefanya Basi hili kuwa na abiria 55 ambao wangefika Dar es salaam masaa kadhaa mbele.


Mwanaume mwenye umri wa miaka 43, aliianza safari yake rasmi pasi hata kutazama chombo chake kama ni salama ama la? Kwakuwa kilitoka safari usiku wa jana basi aliimani huenda hata siku hii kingemfikisha salama. Kwa mwendo aliouzoea aliendesha gari lakini safari yake ilisimama baada ya Askari wa usalama barabarani (trafric) kupiga tochi Basi hili. Mwakilaki, alihisi huenda hii ndio ingekuwa siku yake mbaya kuliko zote katika maisha yake. Mkosi wa asubuhi asubuhi wa kupigwa tochi ulimkera na alipomtazama Askari, aliona uso wake umeanza kuwa na furaha mara baada ya Basi kusimama. Askari aligeuka na kuwatazama wenzake walioko katika kibanda, wenzake walimuonesha ishara kwa kumkonyeza. Askari alipiga hatua hadi sehemu gari lilipo. Alifanya ukaguzi wa nje kwa dakika kama tano huku akiwa anaandika kwenye kijitabu chake kidogo ni wazi kuwa, kulikuwa na makosa ambayo aliyapata kutoka katika Basi.

Basi linaonekana kuchoka na kama sio halikupata muda wa kupumzika kwa sababu muda wote lilitema harufu kali ya injini. Askari alizidi kuandika katika kitabu chake kisha alipiga hatua hadi karibu na dereva, wawili hawa waliingia katika mazungumzo ya usiri kwa muda kidogo kisha Askari alipanda ndani ya Basi na kuwasalimu abiria wote huku akiwatakia safari njema huko waendako wafike salama. Alieataka Abiria wote kufunga mkanda, nao walifanya hivyo. Askari alishuka katika Basi na kurudi kuzungumza na Dereva.

Dereva kwa macho ya mtu mwenye majuto, alijaribu kujitetea huku akionesha ishara ya kuomba na kunyenyekea, alifanya hivyo kwa zaidi ya dakika 10 huku akionesha ishara ya vidole vitatu. Maongezi yalishika hatamu, mmoja wa Askari ambaye alikuwa katika kibanda, alisogea karibu yao. Wanazungumza kwa lugha moja, Dereva alionekana kuwa muungwana hana shida yoyote na Askari huyu, naye anamtazama Kondakta wake mwenye suti iliyochoka ikiwa na nembo ya kampuni yao, kisha anamuonesha ishara ya vidole vitatu kutoka katika mkono wake wa kulia. Ishara hii kwake alijua inarenga jambo gani? Alishuka katika gari na kwenda nyuma ya buti, alijifanya kama anafungua na kufunga vyema. Noti tatu za rangi nyekundu alizidondosha chini kisha anamtaarifu Dereva waanze safari huku akimthibitishia kuwa kila kitu kipo sawa.


Kila kitu kipo sawa kwao pamoja na kwa Askari ambaye alikwenda nyuma ya gari, anaangalia kushoto na kulia. Aliliruhusu gari kuondoka kisha aliimana na kuokota noti tatu. Uso wake uliweka tabasamu, hakuonekana kama alikuwa mkali kabla ya kuipata pesa hii. Kichwa chake kilipanga mipango mingi ya kutumia pesa pamoja na kutoa taarifa kwa Askari wengine katika vituo vinavyofuata, akiwataka kutosimamisha gari yenye usajili fulani kwa sababu tayari amekwishalifanyia ukaguzi wa kutosha.


Ukaguzi wa kutosha ulimlevya Dereva ambaye alijawa na manung’uniko akilalamika kwa kile kilichotokea.
“Jamaa wakiona hawajapata mshahara kwa wakati tu, basi wanasimamisha balaa” aling’ununika Dereva na Kondakta akaunga.
“Unaambiwa Sembule juzi imemtoka 80 kama masiara, jamaa sa’ivi wana njaa balaa” Kondakta alichangia. Mada yao ikawa ni tukio lililotokea muda mfupi uliopita. Walilalamika sana wakilaani juu ya kufinywa kwao, mwisho Dereva alikubali yote, alikubali kuendeleza safari yake na sasa mwendo kasi akauajiri katika Basi lake. Vibao vilivyomtaka kutembea kwa mwendo wa kawaida, hakuvijali. Nani wakumhofia ikiwa amepewa ruksa kwa kuinunia? Hakuna. Umakini ukawa mkubwa katika kujua analipita gari gani lililokuwa mbele yake ili afidie muda ambao aliupoteza wakati aliposimamishwa. Hakujali usalama wake, usalama wa wasaidizi wake wala wa abiria lengo lilikuwa ni kufika Jijini Dar es salaam kwa wakati.

Abiria walistuka, kwanini mwendo kasi umezidi? Mmoja alinyanyuka na kwenda kwa Konda, anamtahadharisha na kumuambia
“Konda, najua wewe una akili timamu, hizi ulizobeba ni roho za watu, tunategemewa na ndani ya Basi kuna watoto zaidi ya 20 ambao ndio Taifa la kesho kama hilo halitoshi, watoto hao wanatakiwa kuwahi shule wakiwa wazima wa afya. Nasi pia ni wazazi, familia inatutegemea”
“Usijali Mr, gari haiwezi kuvuka speed limit iliyowekewa na Mamlaka. Dereva anajua hilo na huu mwendo ni wakawaida kabisa. Ondoa shaka” Kondakta anafanikiwa kumshawishi Abiria ambaye alirudi katika siti yake, akaketi lakini bado moyoni mwake mlikuwa na hofu kubwa juu ya mwendokasi wa gari.


Mwendokasi wa gari unafanya Dereva azidi kujiamini, nini akitake ikiwa tayari anauhuru alioununua? Kondakta wake anampatia ujumbe aliopewa na abiria. Ujumbe aliopewa Dereva kwake haukufanya kazi, badala ya kupunguza mwendo, dereva alibadilisha ‘Flash’ katika redio yake kutoka ya flash yenye maigizo na filamu za kupigana hadi yenye muziki wa kisasa. Wimbo wa kwanza ulipomvutia, aliongeza sauti. Mkono wake wa kulia ulishika chupa ya juice, alikunywa. Dakika mbili mbele jasho lilianza kumtoka.


Jasho lilianza kumtoka kwa wingi utadhani alikuwa anafanya mazoezi hata kiyoyozi cha ndani ya gari hakikufanya kazi kwake, alionekana kama ametumia kinywaji kikali. Ndio, ilikuwa ni pombe kali ambayo alichanganya katika juice ili kuzuga Abiria wake wasimfahamu kama anatumia pombe. Pombe ilimlevya Dereva, mwendo kasi ukamkolea huku akiwa na shauku ya kutaka kufika kwa haraka. Watu walipolalamika kuwa mwendo mkali, hakusikia. Muziki uliziba masikio yake huku akifurahia kile alichokuwa akikisikiliza.

Kituo kilichofuata kilikuwa na abiria ambao hawakuwa wamekata tiketi lakini walihitaji kufika Dar es Salaam. Watumishi wa Basi wakapiga hesabu juu ya kiasi walichokipoteza na watakachokipata kama wakikubali kuwabeba abiria wale, licha ya siti zote kujaa lakini waliona bora wawapakize kwa bei ya chini. Dereva aliruhusu hili, abiria nao bila kujali usalama wao. Waliingia katika Basi huku wakipunguziwa Nauli, hatimaye idadi ya Abiria ikaongezeka, kutoka abiria 55 mpaka 70. Basi iligeuka kuwa daladala na dereva hakuwa na wasiwasi kwa sababu tayari alikuwa amenunua uhuru hapo awali.

Uhuru ulizidi kuvuka mipaka hadi walipokaribia Chalinze, Injini ya gari ilianza kuchoka, taratibu moto ulishika katika injini. Dereva hakujua hilo, aliendelea kuendesha gari huku akivuta mwendo, sauti ya muziki ikimsahaulisha kila kitu. Lakini ghafla, gari lilisimama, mbele haliendi wala nyuma halirudi. Nini kimetokea? Dereva alitahamaki. Wakati akitaka kujua, moto mkubwa ulilipua gari na hakukuwa na abiria ambaaye alitoka salama. Moto uliteketeza Abiria pamoja na Basi lenyewe.

Abiria watano ndio waliokapona kwa juhudi zao binafsi za kutokea madirishani lakini tayari moto ulikuwa umewakula kwa kiasi kikubwa. Abiria wengine walipoteza maisha kwa uzembe wa Askari ambaye alijali pesa kuliko kuangalia usalama wa raia. Walipoteza maisha kwa sababu ya uzembe na ubinafsi wa dereva wa kutoa hongo ikiwa anajua gari halikuwa na uwezo wa kwenda popote. Familia zaidi ya 65 tano zilipoteza wapendwa wao kwa uzembe ambao ungeweza kuepukika na maisha yakasongea. Kosa moja lilisababisha uchumi kwa Taifa kupotea, kuwa duni na kuangamua. Doto za vijana kupotea pamoja na kuongezeka kwa wajane na yatima.

Maadili ya hadithi hii:

  • Dereva jaribu chombo chako kabla ya kuingia barabarani.
  • Kosa moja linaweza kusababisha dunia nzima ikalia kwa kudharau kanuni na sheria za barabarani.
  • Dereva, mwendo kasi sio salama kwako na kwa abiria pia.
  • Udereva ni zaidi ya kuendesha gari, linda roho za watu.
  • Dereva usichezee speed limit
  • Ewe Askari weka haki mbele na sio rushwa ili kulinda usalama na afsa za wengine.
  • Ukiona gari lipo mwendo kasi paza sauti.
  • Dereva usiendeshe gari huku ukiwa umelewa, unasikiliza muziki n.k


Kwa pamoja tunaweza kutokomeza ajali za barabarani. Usalama wako unaanza na wewe.
 
Upvote 0
Back
Top Bottom