Kozi zitakazokuwezesha kujiunga kirahisi na JWTZ

Tatizo humu kila mtu anaongea lake

Jeshini nako siku hizi connection kama hauna refa tena mwenye cheo kikubwa kule utasota sana hata uwe na masters ya aeronautical engineering

Nina ndugu yangu ana diploma ya sociology aliingia jeshini kwa connection na ndani ya miaka mitano tu akawa tayari ni lieutenant anakula maisha wakati kuna mtu na degree yake hiyo miaka mitano bado ni private anakimbizana na kuruta na kulima mashamba kila siku

Sent from my SM-G973F using JamiiForums mobile app
 
JKT wanakwenda baada ya kumaliza form six, udaktari, unesi, urubani wataupata muda gani?
 
Usome urubani kwa milioni 200 halafu uajiriwe JWTZ?
 
Nakumbuka miaka ya nyuma wakati nipo jkt walikuja kufanya usahili wa kuchukua vijana waliosoma science yani PCM, PGM, na PCB na walivyo na akili walikuja wakati wa (six week) kipindi hicho mtu akikwambia tukuandikishe ili badae uende jwtz ukapige kozi ilikuwa ni ngumu sana kukushawishi kutokana na mateso yale ya jkt afu ukateseke tena jwtz Hapana! Nakumbuka waliambulia vijana wachache tena kwa kulazimisha akiwemo rafiki yangu mmoja ambae alikuwa doja mzuri tu na mvivu wa kazi za shamba. Baada ya kumaliza mafunzo ya jkt tulienda chuo tukiwa mwaka wa kwanza rafiki yangu akapigiwa simu kuwa anahitajika kambi ya abdallah twalipo 95kj nadhani kama sijakosea akafanye usahili wa kuingia jeshin, nakumbuka tulimcheka sana nakumsihi asiende uko maana ataumia vibaya kwa mateso ila mwisho alienda na nikapoteza mawasiliano nae.

Siku moja katika harakati zangu za maisha wakati huo sina ajira na chuo nishamaliza
nilienda benki kumlipia mdogo wangu ada ya shule, wakati nimefoleni kwenye mstari kusubiri huduma nilishaanga kumuona askari polisi(FFU) nakusaruti kijeshi ile kutaamaki namuona jamaa yangu kavaa full kombati za kijeshi na ana cheo cha luten nyota mbili daaha roho iliniuma na nilijiona mjinga sana
Anyway wadogo zangu hiyo nafasi ukiipata usichezee kabisa
 
Vipi kozi za kilimo na mifugo, na zile za uhandisi...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…