Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu wenye vyeo vya mabegani ndiyo maofisa. Hao uliowataja vyeo vyao ni vya mikononi.Kwasababu jeshi lina maofisa wengi hivyo halitaki tena maofisa linataka nguvu kazi ndio maana hupendelea la saba maana hawa wengi wanaishia kua ma private au vyeo vya mabegani basi ( koplo,meja,sajenti ,rcm,nk)
Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Yeah nimechanganya ni vyeo vya mkononi pamoja na wavaa saaMkuu wenye vyeo vya mabegani ndiyo maofisa. Hao uliowataja vyeo vyao ni vya mikononi.
Pole pia mkuu yaan hapa vijiwe ni pasua bichwa kazi tembo malipo sisimiz[emoji1787][emoji1787]tuko pamoja mkuu.. napiga vijiwe hadi nachanganyikiwa. Kumbe inawezekana chaka langu liko jeshini
Sijaona wanyonyaji Tz kama wamiliki vijiwe.. bora nafasi za Jeshi zitoke tukajaribu maisha hukoPole pia mkuu yaan hapa vijiwe ni pasua bichwa kazi tembo malipo sisimiz
Atakuwa taahira kama luteni UrioYani mtu asome urubani akasotee jeshi
ivi ukiingia jeshini kwani huwezi kuacha kaziKweli kabisa mimi nina jamaa zangu watatu wana degree ya Computer Science, wameishia usajent,wana wengine sasa hivi Maluteni, sijui walifanya nini ,ila jeshini kama huna NIDHAMU na UADILIFU issues ndogo tu utakaa benchi mpaka unastaafu,haijalishi una level gani ya kielimu au umesomea kozi gani.
Kazi yeyote ya kuajiriwa unaweza achaivi ukiingia jeshini kwani huwezi kuacha kazi
Ivi ni kwanini utakuta mtu bado kijana na nguvu zake halafu anakuambia mie nimeshastaafu,je umri wao kwa vyeo vya chini ni miaka 45 amaKazi yeyote ya kuajiriwa unaweza acha
Akina Tata Mura, vita ni vita mura [emoji3][emoji3][emoji3] siku hizi makabila yote yapo kwa uwiano mzuri ingekuwa hivyo kilugha chochote ukikijua tuu ungepeta kiulaini. Sasa mambo ni tofauti.Ukitaka kujiunga na jeshi lolote Tanzania jifunze kuongea KIKURYA
Samahani Mkuu, BMS kirefu chake ni nini?Kijana yoyote yule ilimradi ni mtanzania anachukuliwa bila kujali course gani amesoma. Ila kwa kipindi hiki JWTZ imewekeza zaidi kwenye course ya BMS
Sasa wanajeshi wote wawe na vyeo nani atamheshimu mwenzake.Jeshi la kielimu kwa afrika litakuja kuwa la hovyo maana watu wanakwenda jeshini kutafuta maisha safi.wakati nidhamu ni elimu bora kuliko chochote jeshini.Yote kwa yote akili zao zisiwaze sana vyeo bali majukumu yalio mbele yao, bila kusahau wanatakiwa kuwa na nidhamu na uadilifu wa hali ya juu, vinginevyo hivyo vyeo mtavisikia pamoja na master yako.
watu hawajui tu Jeshini hasa JWTZ ndio sehemu ambayo kuna kila taaluma iliyo nchi hii.Kule kuna ma proffesor,dar degree za kwanza ni za kumwaga na mainjinia ndio usiseme.Jiulizeni Muhimbili walivyogoma ni kina nani walikwenda kukamata usukani,waongoza ndege walivyo goma nani walikwenda kamata usukani.Wapo mpaka maprofesa jeshini kijana, ni kawaida tuu. Jeshi limekuwa la kisasa linaenda na wakati.
usikate tamaa unaweza kwenda kuwa ofisa uhusiano wa kati ya jamii na jeshi lilipoNimehuzunika sana kusoma huu uzi nimesoma kozi ya community development na jeshi nalipenda
Na waliosomea mifugo vip?Natumai mu wazima wa afya. Pole kwa wanaoumwa, Mungu awajaalie mkapate afya njema.
Nimeona niwashauri kuhusu kozi na taaluma za kuwa nazo, vijana wetu wenye lengo la kwenda kujitolea JKT ili baadae waje kupata nafasi ya kuandikishwa JWTZ kwa urahisi.
Kijana, kama una nia ya kuja kulitumikia taifa letu hili pendwa la Tanzania kupitia kuwa mwanajeshi JWTZ, soma kozi hizi ili ukienda kujitolea JKT ikuwie rahisi kuandikishwa kufanya kozi ya jeshi la wananchi JWTZ.
1. Kozi zote za afya. Udaktari, unesi, ufamasia, radiographia n.k pata certificate, diploma, degree, masters mpaka PhD ya taaluma za afya, hutajutia.
2. Urubani. Ukisoma kozi hii, hata JKT unaweza usipite, ila sasa hakikisha kwenu muwe mna hela ya kutosha sio ya kubababisha maana urubani si mchezo, mpaka milioni 200 +.
Hizi ndio kozi za uhakika, ukiwa na hizo fani, ukaenda JKT, siku JWTZ wakija kuwafanyia usaili hutakosa kupata nafasi kwenda kuvaa bakabaka.
Mbali na hapo, jiandae kutoboa mkataba na kurudi nyumbani, au ujiandae kwenda polisi, Magereza, uhamiaji au wanyamapori (ukibahatika).
Ni hayo tuu kwa leo, nakaribisha michango ya wengine. Muwe na muda mwema sana
Kwamba kuna Rubani anaelipwa laki 3 kama dereva wa Land Cruiser au sio. Hebu jishikilie we jamaa.Hapo no. 2. Hapana , rubani.mshahara wake mdogo Sana nchi za wengine rubani wanaacha kazi kusomea IT, rubani Hana tofauti na dereva wa gari tofauti wewe unapita chini yeye juu. Hata darasa la saba kama unajua kusoma naa kuandika unaweza jifunza urubani. Siyo ngumu sana, utachukuwa muda kujifunza katika takeoff na landing. Ni sifa tu kuwa rubani lakini mfukoni hakuna kitu zero kabisa.