Daaaa! Nakumbuka miaka ya 2000 mwanzoni krismasi ndio inafika, mimi ni muajiriwa mahali fulani kipindi hicho. Halafu ndani naishi na mwanamke japo si wa ndoa na tuna mtoto mmoja. Sikukuu inafika sina kitu mfukoni na kazini hatujalipwa.
Sasa wife anasisitiza tununue chochote hata ikiwezekana tukope. Nikiangalia sioni shehemu ya kukopa. Nikamwambia wife kakope kwa mangi maharagwe tu leo tutakula tusubiri sikukuu ya mwaka mpya nitajipanga. Wife Kagoma hadi ikawa kelele ndani. Mara karopoka leo sili (mimi) na wala hapiki chochote.
Kumbe bwana mama mwenye nyumba alikuwa anasikiliza tu. Nilikuwa nimepanga nyumba tunaishi na mwenye nyumba nyumba moja kasoro vyumba tu, si unajua uswahilini.
Nikachukulia mzaha nikatulia ndani nacheki TV chaneli kama zote nabadili tu, sina ramani kabisa ya kutoka siku hiyo. Basi bwana mama mwenye nyumba kwa huruma zake kumbe kapika na ziada. Mida ya saa nane mchana nasikia anamwita wife. Hapo ni kwamba dogo (mtoto wetu) kakotogewa uji mchache asubuhi na mimi hata sikutaka kuuonja. Ndani kuna unga, mchele, viazi mviringo dagaa na mafuta ya kupikia. Mkaa upo na gesi tulikuwa nayo, kwa hiyo ilikuwa ni maamuzi tu ya wife kupika.
Wife katoka kwenda chumba cha mama mwenye nyumba, sikujua kaitiwa nini. Masikio hayana pazia bwana. Nikasikia akamwambia wife: NILISIKIA MABISHANO YENU NA MUMEO. KWA BAHATI MIMI NINA NAFASI KIDOGO NIMEAMUA NIONGEZE CHAKULA ILI NA NYIE MPATE JAPO SIKUKUU IENDE VIZIRI. LETA VYOMBO UPAKUE CHAKUALA HIKI HAPO KAMA UNAVYOONA.
Mara wife yuko ndani anachukua hotpot na mabakuli. Kaelekea kwa mwenye nyumba na baada ya mda karudi na pilau kuku, ndizi za kupika na kachumbari. Kaweka mezani wala hakunusemesha. Nami nikachuna tu. Kamwita dogo akasogea kampakulia chakuala, mimi nimekomaa na TV kama kipofu vile.
Kwa kweli nilijisikia aibu sana sana. Kuzuga nikajifanya naenda dukani kununua soda (nilichukua matupu manne). Sikupita kwa mangi nikala chocho nikatikeza mtaa wa pili. Nikaelekea kwa mshikaji wangu, yeye alikuwa bachela, hajaoa. Bahati nikamkuta nae kachili tu. Nikampa stori nzima.
Mwanangu akasononeka sana. Kaanza kunikumbusha mambo ya longi mara ooooo, huyo demu wako usingezaa nae tulukwambia sio wife material unaona sasa... Tukapiga stori pale za kutosha. Kumbe mwenzangu asubuhi kapiga zake supu hana shida.
Ikabidi nijikaze kiume, tena ukizingatia niko na mwana. Nikampa live sina hata jero na kazini hatujalipwa, tena sijala. Mwana akanielewa. Akasema kuhusu wife shauri yake... Akanitoa tukaenda kupiga kitimoto choma bwana... Baada ya hapo gambe likaanza hadi saa tano usiku nakumbuka nyumbani. Hapo simu nilizima ttka mchana. Kurudi home wife kafungua mlango mimi direct kitandani hakuna neno hata moja. Kesho yake wife anaomba msamaha. Nikaona isiwe tabu ni maisha tu nikammsamehe.