Ku-file kupitia mfumo mpya wa iDRAS vipengele vimekuwa vingi

Ku-file kupitia mfumo mpya wa iDRAS vipengele vimekuwa vingi

Vien

JF-Expert Member
Joined
Mar 6, 2020
Posts
8,508
Reaction score
15,276
Wakuu salaam.

Naomba nichangie jambo ambalo naamini wengi wetu wafanyabiashara na wahasibu tunapitia kwa sasa - ku-file returns kupitia mfumo mpya wa iDRAS wa Tanzania Revenue Authority.

Zamani mambo yalikuwa relatively straightforward. Unaingia, una-file, unamaliza. Lakini sasa mchakato umeongezewa vipengele vingi kiasi kwamba kwa mtu ambaye hana accountant wa kudumu inaweza kuwa changamoto kubwa.

Changamoto nilizokutana nazo:

1. Mfumo wa “Create Batch” kwanza

Sasa kabla hata huja-upload return, lazima u-create batch. Kwa mtu ambaye alikuwa amezoea direct filing, hii ni hatua ya ziada inayochanganya mwanzoni.

2. Excel Template yenye structure ngumu

•Huwezi kufuta column
•Huwezi kubadilisha sheet
•Kuna Tanzania Bara na Zanzibar hata kama huna shughuli Zanzibar
Ukikosea kidogo tu validation inakataa.

3. Validation Errors zisizoeleweka kirahisi

Wakati mwingine system inarudisha error message isiyoeleza moja kwa moja tatizo liko wapi. Inakulazimu kupitia cell moja moja kutafuta kosa.

4. NIL Return nayo ni mchakato mrefu

Hata kama huna mfanyakazi (PAYE = 0), bado unatakiwa:

•Create batch
•Upload Excel
•Validate
•Submit

Kwa biashara ndogo isiyo na wafanyakazi, huu mchakato unaonekana mzito ukilinganisha na nature ya return yenyewe.

5. Bara na Zanzibar confusion

Template inakuja na pande zote mbili hata kama biashara ipo upande mmoja tu. Wengi wanajiuliza wafute au waache blank - na ukikosea structure system inakataa.

Sina pingamizi na maboresho ya kidigitali, lakini naamini bado kuna nafasi ya kufanya mfumo uwe rafiki zaidi kwa small businesses.

Je, wenzangu mmekutana na changamoto gani kwenye iDRAS?
Au kuna mbinu mmegundua zinazorahisisha filing?

Karibuni kwa mjadala.
 
Ukiona mambo yanafanywa kuwa magumu ujue ni mazingira ya "chai" yanatengenezwa
 
Yeah ni kweli filing returns leo imenisumbua kidogo, Ila naamini ukiuzoea utakua poa
 
Nafikiri Lengo la TRA ni kwenda Paperless na Kuwa Transparent.

Issue ya Batch Creation lengo nafikiri nikumaintain Payrol workflow.Inakulazimisha Upitie mchakato kamili wa kuandaa Payrol.Ni kweli kwa kampuni ambayo ni changa na aina ya wafanyakazi ni kipengele ila ikizoeleka haitakuwa shida.Any way tuendelee kuutazama na kutoa maoni ya maboresho ila kwa kiasi fulani tumepiga hatua kutoka mfumo wa zamani.

Shida ninayoona ni Support ya TRA online yaani handling yao ya queries ndani ya mfumo bado ipo slow san.Inakuwa inakera wanapochukua muda kufanyia kazi issue za ndani ya mfumo inabidi waongeze bidii kwenye utaratibu wao wa ndani kuhakikisha Mtu anapotuma issue inakuwa responded ndani ya muda mfupi maximu 24 hrs.Sio issue inakuwa unresolved kwa siku 2-7 as if hakuna watu kazini.
 
Back
Top Bottom