Kuacha degree ya Human Resources kwenda kusomea Diploma in Forestry

BLACKLIST 12

Senior Member
Joined
Aug 28, 2022
Posts
128
Reaction score
100
Wakuu samahani..

Naomba mnisaidie ushauri.

Inaeza ikawa so mahala pake..

Niko chuo first year

Nachukua bachelor ya human resource

Ila sijapata mkopo

Me ni fresh toka advance.


Sasa nilikuwa nalipiwa kwa michango ya ndugu...ila naona kama inawawia vigumu.

Maana ada,chakula,malazi na mavazi juu ni wao wananisaidia 100%.

Kuna watu wanashauri nirudi nikasome diploma ya misitu.

Sababu...

1.chuo cha misitu kiko karibu na nyumbani so nitakuwa natokea nyumbani kuelekea chuo hivyo basi kupunguza kost za malazi..chakula

Wao watapambania ada.

2.wanahisi course hii ya human resources management haina soko mjini

Kwao itakuwa wame-waiste resources zao afu at the end nirudi kitaa kuhustle tena.


Umri

20 years


Elimu yangu

Form 4

Form 6


Ujuzi

Driving + licence daraja A A2 D

JKT 839


Post za polisi magereza uhamiaji zote huwa na jaribu kuomba....wanaopitia zile nyuzi tunakutana...


Wakubwa naomba mnishauri kushift kwenda io diploma ya misitu ntakuwa nimefanya chaguo sahihi?
 
Umepishana na gari la hela za usaili...
 

Mpnago mzuri HR haina soko
Rudi nyumbani kaa chini na ndugu wanaokusudia waambie wazo lako zen mtafikia muafaka
 
Nenda kasome kozi mojawapo kati ya hizi Chuo cha Bahari.
[1] Basic Technician Certificate (NTA Level 4) in Cargo Tallying and Supply Chain Management (BTCCTSM)
[2]Technician Certificate (NTA Level 5) in Shipping and Logistics Management (TCSLM).

achana na hako ka Human Resource kama hutaki kufa maskini.
 
Fanya haraka sanaaa kuamiaa Tena kesho ashb andika baruaa ,kwa tz hii human resources Ni janga tu Huna konection kubwa utakaa Sana ,naomba kwa unyenyekevu kasome hyo DIPLOMA YA MISITU
 
Fata huu ushaur
 
Fanya haraka sanaaa kuamiaa Tena kesho ashb andika baruaa ,kwa tz hii human resources Ni janga tu Huna konection kubwa utakaa Sana ,naomba kwa unyenyekevu kasome hyo DIPLOMA YA MISITU
Nashukuru jwa ushauri mkuu...
Noted✅
 
Nashkuru mkuu....nitafatilia na uko🙏
 
Achana na stori za vijiweni mkuu.
Changamoto ya uhaba wa ajira nchi hii ipo kwa kozi zote.

Usithubutu kurudi nyuma na kupoteza muda kwenda kuanza diploma.
Endelea kusoma digrii ya HRM hiyohiyo ambayo umeshaianza,
tena isome kwa upendo, juhudi na nia sana.
Na uhakikishe kila ufanyapo U.E unafaulu kwa GPA nzuri ya kuanzia upper second class,
Michongo utaikuta ufikapo uraiani.
 
Nimekuelewa mkuu
✅ noted!
Asante kwa ushauri.
 
Bora ungesoma Animal Resources kuliko yumani resources kwasababu siku hizi hao yumanzi wenyewe ni animals
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…