Kuacha degree ya Human Resources kwenda kusomea Diploma in Forestry

Kuacha degree ya Human Resources kwenda kusomea Diploma in Forestry

Wakuu samahani..

Naomba mnisaidie ushauri.

Inaeza ikawa so mahala pake..

Niko chuo first year

Nachukua bachelor ya human resource

Ila sijapata mkopo

Me ni fresh toka advance.


Sasa nilikuwa nalipiwa kwa michango ya ndugu...ila naona kama inawawia vigumu.

Maana ada,chakula,malazi na mavazi juu ni wao wananisaidia 100%.

Kuna watu wanashauri nirudi nikasome diploma ya misitu.

Sababu...

1.chuo cha misitu kiko karibu na nyumbani so nitakuwa natokea nyumbani kuelekea chuo hivyo basi kupunguza kost za malazi..chakula

Wao watapambania ada.

2.wanahisi course hii ya human resources management haina soko mjini

Kwao itakuwa wame-waiste resources zao afu at the end nirudi kitaa kuhustle tena.


Umri

20 years


Elimu yangu

Form 4

Form 6


Ujuzi

Driving + licence daraja A A2 D

JKT 839


Post za polisi magereza uhamiaji zote huwa na jaribu kuomba....wanaopitia zile nyuzi tunakutana...


Wakubwa naomba mnishauri kushift kwenda io diploma ya misitu ntakuwa nimefanya chaguo sahihi?
Tulia wewe. Endelea na kozi hiyo
 
Kama hutajitambua hata ukisoma kozi yoyote hamna kitu sababu akili yako imekaa kuajiliwa tu
 
Human resources kozi Haina Dili Kwa sasa wamejaa kama kumbikumbi.

Hio forestry ni nzuri.

Kama uweza fanya haraka hamia huko.

Then kwenye bachelor kama ipo hapa bongo piga au nenda kasomee wanyama au kilimo.
 
Nimefanikiwa kupata forest braza kwa level ya NTA level 5.
Kupitia cheti cha six.

Tunakaza sasa na masomo
mungu amulike tu🙏
 
Nenda kasome kozi mojawapo kati ya hizi Chuo cha Bahari.
[1] Basic Technician Certificate (NTA Level 4) in Cargo Tallying and Supply Chain Management (BTCCTSM)
[2]Technician Certificate (NTA Level 5) in Shipping and Logistics Management (TCSLM).

achana na hako ka Human Resource kama hutaki kufa maskini.
Hizi zinatolewa NIT au wap?
 
Back
Top Bottom