Kuachia wahalifu kwa muda mfupi ni hatari inayokuja nchini

Kuachia wahalifu kwa muda mfupi ni hatari inayokuja nchini

MchunguZI

JF-Expert Member
Joined
Jun 14, 2008
Posts
4,011
Reaction score
2,185
Ni katika kipindi cha siku 100 madarakani, Rais anaachia wahalifu kwa sababu anazozijua. Baadhi ya wahalifu wamekuwa mahabusu tangu awamu ya 4 ya Kikwete wakati Rais Samia akiwa ni waziri tu!

Je, ni kweli katika siku 100 ameweza kugundua watu hawa walionewa? Kweli rais wetu anaamini serikali zote zilizopita hazikufahamu undani wa watu hawa isipokuwa yeye?

Rais Samia, hakika unatuponza! baadhi ya watu hawa tunawafahamu mikasa yao huku mitaani. Huku Bara (Tanganyika) ndo huwa kituo cha uhalifu wa watu hawa. Hawa watu muda hautapita mitaani watatuumiza na tutaomba utueleze unakotupeleka ni wapi?
 
Hata kama wametenda ndio ichukue miaka 9 bado hakuna ushahidi?(UHAMSHO) ,ichukue miaka minne hakuna ushaidi(escrow)? Kama wamekosa na uthibitisho upo wapewe hukumu kama imechukua miaka yote bila ushahidi ni bora walivyoaachiwa siku wakipata ushahidi wawakamate tena.
 
Angekuwa ameachiwa dingi yako ungelalamika? mwacheni Rais afanye kazi yake kwa uhuru, hakuna taifa limeendelea kwa kujaza watu ndani bila sababu za msingi.
Hizo hasira ni kama unaona wanakuharibia dili lijalo?
 
Angekuwa ameachiwa dingi yako ungelalamika? mwacheni Rais afanye kazi yake kwa uhuru, hakuna taifa limeendelea kwa kujaza watu ndani bila sababu za msingi.
Mbona wezi wa kuku hatuoni wakitolewa?

Je wale wafungwa waliokuwa wanasemwa na kina Lema kwamba wamejazana magerezani bila hukumu ndio hao wanaotoka?
 
Back
Top Bottom