Kuachiwa Ndege Canada: Lissu, Fatma Karume na Membe muombeni radhi Profesa Kabudi

Kuachiwa Ndege Canada: Lissu, Fatma Karume na Membe muombeni radhi Profesa Kabudi

Narudia tena, mna bahati! Mark my word!!
Hutakaa upate Uongozi kwa Akili hizo maana mungu anapenda uishi miaka mingi akikupa Uongozi utaanza udikiteta na matokeo yake utaishia kufa kwa pressure
 
Hayaaa! nani amemuona tundu hapo nyuma anapata mgawo
Tundu Lssu anaingiaje kwenye hili risasi apigwa kwa order kutoka juu lakini mungu kamuokoa
Sasa munanbebea bango ninti ndio hufa kifo cha kishenzi
 
Ndugu zangu,

Takribani majuma mawili yaliyopita Waziri wa Mambo ya nje Prof.Palamaganda Kabudi aliutaarifu Umma kutokea Dodoma siku ambayo Rais Magufuli alikuwa na kazi ya kikatiba kuwaapisha mabalozi wetu.

Prof.Kabudi alimuelezea rais huku akieleza jinsi ambavyo wananchi wa Tanzania watauchukua ushindi dhidi ya kaburu Stein kwa mara nyingine baada ya ''kumcharaza'' katika mahakama ya Gauteng kule bondeni (Afrika ya kusini).

Aliyekuwa wa kwanza kubeza ni Ndugu Membe huku akiaminisha umma kuwa Prof.Kabudi hatafanikiwa, akishauri kuwa njia pekee ni kumuita mkulima Stein kwenye meza na ''kumlipa chake. Ajizi nyumba ya njaa naye Tundu Lissu na Fatuma Karume wakauvagaa mkenge huku akiwa hawana uzoefu wowote na mashauri katika korti ya kimataifa, walijaribu kuwaapooza wafuasi wao ambao walikuwa wenye hasira nyingi baada ya kushauriwa vibaya kujitoa uchaguzi wa serikali za mitaa.

Bila kuchelewa, wafuasi wa CHADEMA na wanasiasa hao wakaivagaa mitandao huku wakionesha dharau kwa Prof.Kabudi na Watanzania, wakisema Mkulima Stein ni ''kiboko'' wakiowanukuu Lissu,Fatuma na Membe.

Wanasheria wetu wazalendo walinyamaza kimya huku wakiandaa hoja za kumshinda ''Mkulima Stein'' kortini. Kwa hoja zilizotolewa kortini hatimaye siku mbili zilizopita Mahakama ya Canada iliipa Tanzania ushindi kwa mara nyingine tena huku ikiweka ''precedence'' kwa siku zijazo.

Nimalize tu kwa kusema, Hongereni wananchi wazalendo wa Tanzania, Mmeshinda tena!
Ni bilioni ngapi za taifa la wajinga mmelipa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acha ushamba wako ujue watanzania siyo wajinga hakuna asiyejua kuwa chanzo cha hili sakata ni profeselii Kabudi kubuni Mbinu za kumdhulumu mkulima wa kizungu kwa kutengeneza mazingira ya kumfukuza Nchini ili wapate kumdhulumu kirahisi kwa njia haramu, Yaani watengeneze Tatizo wao kwa kisingizio cha uzalendo kisha watake watanzania wenye Akili timamu waone huo ni uzalendo? , acheni dharau kwa watanzania Tambua kuwa watanzania wana Akili nyingi kuliko nyinyi watetezi wa CCM mitandaoni.
Kamanda aibu imewapata

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kamanda, hata SA mlisema hivyo hivyo, tumewazoea kwa kujifariji
Anyway, tuwe wakweli tu. Nakala ya hukumu ya South Africa ilizungushwa kwenye mawasapp na mitandao immediately. Wekeni na hiyo hukumu ya Canada kukata mzizi wa fitna.
 
Kazi ya upinzani ni kuikosoa Serikali kwa kila kitu kidogo kikubwa matukio hawatakiwi kuacha chochote kile popote Nchini, usiwapangie cha kukosoa lazima wapite na mapungufu yote mda wote.
Kosoeni kwa nia ya kujenga sio mpaka mnaonekana watoto wa washirikina.
 
Back
Top Bottom