Kuagiza Gari nje ya nchi vs Kununua Yard

Kuagiza Gari nje ya nchi vs Kununua Yard

Ni bora angezisema hizo yard zilizomfanyia mchezo huo kuliko kuzihukumu yard zote maana siyo kweli kuwa gari za kuagiza mwenyewe ni bora kuliko za yard kuna sababu nyingi zinapelekea mteja kuamua kununua yard badala ya kuagiza mwenyewe moja kwa moja
Kwani za yard zinatoka wapi hadi ziwe bora kuliko za kuagiza direct? Nadhani yard nyingi zinafanya huu ujanja ujanja aliousema mleta mada!!
 
Wale madalali wanaopanga magari uwanjani/pembezoni mwa barabara ndo hatari zaidi maana sidhan hata Kama wanalipa kodi
 
Yaah hii ndo sababu tunaagiza nje, mi naokoa hadi 3.5m kwa gari husika kulinganisha na bei ya Japan
Unapotaka kununua gari befoward au sbt Japanese wanapunguzo lolote au ndio wanakomaa Bei Ile Ile waliyoandika. Naomba nieleweshwe.
 
Unapotaka kununua gari befoward au sbt Japanese wanapunguzo lolote au ndio wanakomaa Bei Ile Ile waliyoandika. Naomba nieleweshwe.
Unapunguziwa lakini kidogo sana ukilia lia...mi Kuna gari moja nilijiliza hadi mikamasi eti wakatoa $100..[emoji849]
 
Back
Top Bottom