Kuajiriwa ni utumwa

Kuajiriwa ni utumwa

Hemedy Jr Junior

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2023
Posts
915
Reaction score
1,082
Kuna kijana kaniuliza kwani we uliyejiajiri unaingiza zaidi ya 5M au upo chini ya hapo.
Na mjibu kama ifuatavyo 👇

Tatizo sio kuingiza kiasi gani we utakuwa mbumbu na unatetea upuuzi bora kuingiza buku yangu kuliko kutumia akili yangu kumuingizia million mwajiri wangu.

Hapa kinachozungumziwa ni utumwa wa kifikra sio kuingiza kiasi fulani cha pesa. Kuna watu wako na hela Ila hawana amani ya moyo.

Ni sawa na kumiliki pesa za majini zinakuendesha we unaona mtu yuko bomba kumbe anateseka. Kuajiriwa ni utumwa. Me sijali hata kama unamiliki kiwango gani cha pesa we kama umeajiriwa nakuona kama mwanamke aliyeolewa au anayedanga maana bila danga hapati mikwanja ila mimi naingiza buku binafsi haina kelele situmikishwi. We endelea kupambana.
 
Jamaa mbona unahangaika Sana?

We si umejiajiri sasa kwann unahangaika Sana na waliojiriwa? We endelea na hizo buku zako unazopata kwa kujiajiri achana na wanaoingiza 5m kwa kumtumikia mtu mwingine.

Mbona unatapatapa Sana? Kuna mtu kakuvuta mkono ukaajiriwe? We ishi maisha yako achana na machaguo ya watu wengine

Unakera manyuzi meeeeengi utadhani unashindana na mtu.
 
Hata sioni ni kwa nini unatumia nguvu nyingi hivi kujadili kitu ambacho wala sioni kama kina mantiki yo yote. Watu wengi wameajiriwa na pia wana vibiashara vyao na maisha yanasonga.

Halafu ujue kuwa watu ni lazima waajiriwe. Tunahitaji wanajeshi, walimu, watumishi wa afya, wahasibu, mapolisi na watumishi wengine. Hawa ndiyo wanashikilia jamii ili hata wewe uliyejiajiri ukiumwa ukatibiwe na ukivamiwa na majambazi polisi waje kukusaidia.

Na sioni ni namna gani daktari aliyeko zamu ni mtumwa wakati akimaliza zamu yake anakwenda nyumbani.

Wewe unayeshinda dukani kwako kila siku siyo mtumwa? Tena ni lazima ufungue kila siku maana usipofungua unakula hasara...uko huku na huko ukihangaika biashara yako isiyumbe...Huo siyo utumwa?

Ni utumwa upi unazungumzia?

Utaachana na utumwa tu pale biashara yako imekua inajiendesha yenyewe na wewe kugeuka mwangalizi tu. Ila hata hapa bado unaweza usiwe huru kivile. Ndiyo maana akina Elon Musk na akina Warren Buffet bado wanafanya kazi zaidi ya masaa 10 kwa siku. Bado ni watumwa ama?
 
Jamaa mbona unahangaika Sana?

We si umejiajiri sasa kwann unahangaika Sana na waliojirowa? We endelea na hizo buku zako unazopata kwa kujiajiri achana na wanaoingiza 5m kwa kumtumikia mtu mwingine...
Mkiambiwa ukweli wabongo manakaza mafuvu. Ukweli ndo huo tuache roho mbaya kuna watu wanajifuta kitu kupitia hoja hizi we ambaye unaziona zinaufinyu wa maarifa
 
Sasa kwanini unalalamikia kitu usichokijua?

Unawezaje ku compare vitu 2 wakati kitu kingine hujawahi fanya na wala hukijui?
Sasa kwanini unalalamikia kitu usichokijua?

Unawezaje ku compare vitu 2 wakati kitu kingine hujawahi fanya na wala hukijui?
Sio kila msanii anachokiimba kimemkuta acha kukaza fuvu
 
Hata sioni ni kwa nini unatumia nguvu nyingi hivi kujadili kitu ambacho wala sioni kama kina mantiki yo yote. Watu wengi wameajiriwa na pia wana vibiashara vyao na maisha yanasonga...
Nadhani we utumwa ninao uzungumzia ujauelewa. Mfano mdogo unaishi kwa ndugu unalala kwa godoro, unakula chakula chake lakini masimango kibao si bora ulale chini lakini kwa amani.

Utumwa wa amani ya moyo. Sijasema utumwa wa kufanya kazi. Me hata nikalala saa 10 usiku najua ni kazi yangu sio kazi ya mwaajiri tuelewane
 
Kuna kijana kaniuliza kwani we uliyejiajiri unaingiza zaidi ya 5M au upo chini ya hapo.
Na mjibu kama ifuatavyo...
We utakuwa mlokole,unaejipa moyo,

"Mambo yote ni upotovu na kujilisha upepo"pale unapoona wenzio wapo kwenye ndinga Kali,vogue,land cruiser,bmw,na kwenye majumba ya kifahari.

Watu wasio nacho,huwa wajinga sana, wakiwa kwenye daladala wamesimama,jasho,joto,wakiona mtu yupo kwenye ndinga yake full kiyoyozi, wao huwaza, aaah tulikuja watupu tutaludi watupu.

Yaani kuuza mahindi ukapata buku yako kwa siku,ni Bora kuliko kuajiliwa ukalipwa laki kwa siku?kisa eti ajira ni utumwa? Akili za hovyo sana hizi.
 
We utakuwa mlokole,unaejipa moyo,
"Mambo yote ni upotovu na kujilisha upepo"pale unapoona wenzio wapo kwenye ndinga Kali,vogue,land cruiser,bmw,na kwenye majumba ya kifahari...
Endelea kuajiriwa kijana ujakatazwa na sio kila aliyejiajiri anauza mahindi. Serikali yenyewe inakupa mshahara kwa sababu ya sisi walipa kodi
 
We utakuwa mlokole,unaejipa moyo,
"Mambo yote ni upotovu na kujilisha upepo"pale unapoona wenzio wapo kwenye ndinga Kali,vogue,land cruiser,bmw,na kwenye majumba ya kifahari.
Watu wasio nacho,huwa wajinga sana,wakiwa kwenye daladala wamesimama,jasho,joto,wakiona mtu yupo kwenye ndinga yake full kiyoyozi,wao huwaza,aaah tulikuja watupu tutaludi watupu,
Yaani kuuza mahindi ukapata buku yako kwa siku,ni Bora kuliko kuajiliwa ukalipwa laki kwa siku?kisa eti ajira ni utumwa?akili za hovyo sana hz
Sisi tuliojiajiri ndio wenye uwezo wa kununua hizo ndinga cash.

Waajiriwa wengi mnatembelea mabakuli mliopewa kwa mikopo kutoka ujira wenu.

Ndiga zenu ni vits,passo,ist,raum,corolla,carina,noha na kidogo kwa bahati mbaya rav 4. Tena unakuwa na kagari kamoja kama uniform ya shule ya msingi
 
Back
Top Bottom