Uchaguzi 2020 Kuamini kwamba Lissu alisafiri angani kutumia helikopta bila kibali cha TCAA ni kujidanganya sana!

Uchaguzi 2020 Kuamini kwamba Lissu alisafiri angani kutumia helikopta bila kibali cha TCAA ni kujidanganya sana!

Naheshimu mawazo yako.
Nafikiri tuna mtazamo tofauti ktk hili ngoja tukubali kutofautiana.
Hata hivyo Kuna hoja kuu mbili kwenye mada yangu.

Mmoja ni kusema uongo, na ya pili ni kuwa waangalifu tusichochee na kujenga tabia mpya ya kutoheshimu taratibu, sheria na kanuni halali hasa kama zinahusu kukwepa kuhatarisha maisha ya watu wengine.
Mkuu Kiranga nisome hapo juu
Unaji contradict kwenye hoja yako ya kuwashutumu CHADEMA kuhamasisha watu kutotii sheria.

Ukikubali sehemu halali ya civil disobedience, then CHADEMA si tu wana haki, bali wana wajibu wa kuhamasisha wananchi kutotii sheria dhalimu.

Ukiwashutumu CHADEMA kwa kuhamasisha wananchi kutotii sheria, bila qualification, then hukubali sehemu halali ya civil disobedience katika demokrasia.

You can't have it both ways.
 
Viongozi wa CHADEMA angalieni maisha baada ya uchaguzi.

Kukaa kimya bila kukemea au kukanusha uongo ulioenezwa LISSU alisafiri kutoka KIA Hadi Kawe Dar kwa helikopta bila kupata kibali toka mamlaka ya anga ni Jambo la hatari Sana kwa LISSU na CHADEMA yenyewe.

Inajulikana hakuna mahali duniani unaweza kurusha helikopta au ndege angani bila kibali toka mamlaka ya anga ya nchi husika.
Rubani angerusha ndege kibabe hivyo ingemgharimu yeye binafsi na mmiliki wa helikopta.
Madhara ya uongo huu ni makubwa kuliko faida.

Mosi: CHADEMA na LISSU mtaonekana au mnaelekea kuhamasisha watu kutotii au kufuata sheria kama mnavyotaka MAGUFULI afanye. Mkichukua dola mtatawala nchi yenye vurugu za kutotii Sheria maana watu watamuiga kiongozi wao kupinga kila taratibu zilizopo kisheria au kikanuni.

Pili: Kwa watu ambao waelewa na waliwaamini watakosa imani nanyi siku zijazo.

Watu wenye kutafakari tunajiuliza hivi kweli LISSU yupo kujenga Tanzania au ana Jambo lake binafsi kiasi Cha kutumia njia hii ya uongo wa kitoto? Anamkosoa Magufuli kwa uongo huku nayeye akisema uongo?

CC: joka kuu
Mkuu, kama ni suala la uongo, hata mgombea aliyeko madarakani ameshasema uongo mara nyingi sana hadi ninaelekea kuamini kuwa hakuna mwanasiasa asiyekuwa mwongo
 
Back
Top Bottom