Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Majini ni viumbe kam bindamu walioumbwa kbal ya binadamu wanaishi kama
tunavyoishi sisi. Wako Majini wazuri na Majini Mabaya kama tulivyo sisi Binadamu tupo binadamu wazuri na wapo
binadamu wabaya tunawaita ni Mashetani wa kibinadamu ukiwa wewe ni muuwaji basi wewe ni shetani wa kibindamu,na pia wapo majini wa kishetani .Shetani ni yule muovu hata binadamu akiwa ni muovu tunamwita ni shetani
mkuu. Kuna Viumbe aliowaumba Mungu sisi binadamu hatuwezi kuwaona kwa macho yetu kam hao majini na malaika ukiwa unaamıni kuna viumbe wanaoitwa malaika basi itakuwa ni rahisi pia kuamini kuwa kuna viumbe wanaoitwa Majini.
SHEITANI MTU NI NANI?
Sheitanimtu anaweza kuwa jamaa yako, ndugu yako, rafiki yako au wewe mwenyewe. Sheitanimtu ni kila anayeweza kumpoteza mtu akatenda jambo ovu kama vile kuiba, kuzini, kunywa pombe, kuvuta bangi na kutumia madawa ya kulevya au kukupandikiza chuki baina yako na mwengine.
Sheitanimtu kila siku unatembea naye, unakula naye lakini huwezi kumgundua kwa urahisi wakati wote unapokuwa nae hujifanya anaushari, busara na hekima upande wako kiasi kwamba wewe mwenyewe humpenda na kumwamini kwa kumuamini na kumthamini kwako basi anajenga katika akili yako mizizi ya tabia na mwenendo wake na hivyo kukufanya uwe miongoni mwa tawi lake.
Ewe ndugu yangu sheitanimtu hafanyi mambo yake kwa siri bali hufanya kwa uwazi ili wewe uyaone na uweze kushawishika. Anaweza kunywa pombe mbele yako kutumia madawa ya kulevya, kuvuta bangi na anaweza kukusimulia jambo lolote kama uzinzi n.k vitendo na masimulizi hayo yote ni kukuvuta wewe kutoka tabia nzuri kukupeleka katika tabia mbaya.
Rafiki yangu mpendwa huyo sheitanimtu yuko tayari kutumia hata gharama ilimradi tu akupoteze. Anaweza kununua vitu vya gharama ili akupe wewe akitaka uwe tu pamoja naye katika maovu. Hapa siyo kwa jinsi yako tu, msichana anaweza kugharamiwa na mvulana au mvulana anaweza kugharamiwa na msichana kwa ajili ya kufanya uovu. Jambo hili ewe ndugu yangu ni hatari sana kwani wewe unajua fedha ni fedheha.
Ewe ndugu yangu, wewe unaakili timamu na unajua ukweli wa mambo unajua yenye manufaa na hasara katika maisha ya kila siku. Kutokana na akili uliyokuwa nayo huna budi kuwa makini na kutafakari wakati unapopewa ushauri na huyo ambaye unasema rafiki yako. Tafadhali sana usipende kusema ndiyo au hapana bila kufikiria faida au madhara ya hiyo NDIO AU HAPANA yako.
Bila shaka wewe unapenda kuisha kwa amani na furaha karibu kila siku kwa hiyo huna budi kuwa makini katika ,maisha yako. Umakini ambao ninakuambia ni KUFIKIRI KABLA YA KUTENDA suala hili la kufikiri kabla ya kutenda litakufanya uweze kugundua mbinu na ujanja anaotumia huyo sheitanimtu na hivyo kujiepusha naye mimi sipendi kuona wewe rafiki yangu ukiwa katika huzuni na majuto ndio maana nina kupa mwanga katika maisha yako.
Ndugu yangu, sheitanimtu katika maisha yako ujitahidi kamuogopa kama ukoma jiepushe nae na asikuzoe nakukutawala katika akili yako na kukufanya wewe kuwa mtu usiyekuwa na kauli ya kusema HAPANA katika kila jambo la uovu.
Wewe ni rafiki na ni ndugu yangu, ninakupa mwanga huu kwa manufaa yako mwenyewe na sio kwa manufaa yangu. Nijukumu lako kutumia akili na hekima alizo kupa Mungu ili uweze kuepukana na sheitanimtu, nawe utaifanya akili yako ifanye kazi kama inavyo takiwa. Kama ulikwisha potenzwa siyo ukate tamaa bali tumia muda huu kujuta na kujirekebisha mara moja.
Mtakuja ku wauwa watu nyie ,shauri zenu
Acheni kwanza kuingiza imani za kishirikina;
Kuna wakati nilimsikiliza dakatari mmoja wa magonjwa ya moyo, na alilielezea hili (ilikuwa siku nyingi kidogo) kwamba inawatokea sana wale wenye matatizo ya presha, magonjwa ya moyo. Kubwa ni kwamba, inaweza kuwa ni kutokana na mstuko wa moyo/presha pale ambapo nguvu kubwa inatumika kusukuma "gogo" na hivyo kuchangia mstuko kwenye mishipa inayopeleka damu kwenye moyo.
Kuna maelezo zaidi kuhusu hili ila kumbukumbu imenipita kidogo. Labda tuwaite wataalamu wetu kwanza (wa tiba za kisasa) kabla ya kuingia kwenye majini.
CC: Riwa, Mupirocin
inamana haipo kisayansi ya darasani,ipo sayansi ya kiswahilihata wakichunguza hao ma-profesa wenu hawawezi kuona kitu huko chooni. Kuna shetani mbaya kila anaye anguka mwisho wake anapatwa na ugonjwa wa kupooza stroke na asipojishughulikia kujitibia basi mwisho wa huo ugonjwa aliopata ni kifo tu hakuna kitu kingine zaidi ya hicho kifo tujihadhari tunapokwenda chooni.
Haipo Kisayansi ya darasani hiyo ipo Sayansi ya kiafrika kuna mambo mengine huwezi kupata kwenye Shule za kizungu unapata Kwenye Shule za kienyeji tu.Hakuna hata Professor yoyote yule anayejuwa hayo mambo ya Sayansi ya Kiafrika.inamana haipo kisayansi ya darasani,ipo sayansi ya kiswahili
Hata vitabu vya dini vinakubali kuna majini na shetani. ila tunawahususha vibaya na maisha yetu. watu wanatelezaga tu bafuni kwa kuwa kuna sabuni na hupelekea kujigonga vichwa kuvuja damu nyiingi ana kupasua mishipa ya fahamu. hakuna uchawi bafuni. amkeni
Hahahahaha watu mna mambo nyie. Mbona bibi yangu alianguka chooni wakati anaumwa ila alipona tu?
Nani alifanikiwa kumpiga huyu jini picha, inaonekana jini aliweka kabisa pozi mmh/=
Mbona kama sikosei Mzee Slaa tuliambiwa alidondoka chooni akavunja mkono na bado yu hai?
Tatizo ni masturbation...hawa wazee hufanya huo mchezo bafuni au chooni...kwavile nguvu za kujizuia zinakuwa zimewaishia huishia kuangukia kichwa...
We bibi yako atakua na kizizi
Acheni kwanza kuingiza imani za kishirikina;
Kuna wakati nilimsikiliza dakatari mmoja wa magonjwa ya moyo, na alilielezea hili (ilikuwa siku nyingi kidogo) kwamba inawatokea sana wale wenye matatizo ya presha, magonjwa ya moyo. Kubwa ni kwamba, inaweza kuwa ni kutokana na mstuko wa moyo/presha pale ambapo nguvu kubwa inatumika kusukuma "gogo" na hivyo kuchangia mstuko kwenye mishipa inayopeleka damu kwenye moyo.
Kuna maelezo zaidi kuhusu hili ila kumbukumbu imenipita kidogo. Labda tuwaite wataalamu wetu kwanza (wa tiba za kisasa) kabla ya kuingia kwenye majini.
CC: Riwa, Mupirocin
Hakuna mashetani wala Majini. Hio mi naona inakuwa ni Pressure kali inayoendana na paralysis. hata mtu akipatwa na kiharusi midomo hupinda na either mkono au mguu au vyote hupooza.