dorahndauka
Member
- Dec 7, 2013
- 7
- 1
Ila jaman vitu vingine ni hatar
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Jamani wana jf,
Naamini humu ndani tupo tofauti tofauti na kila mmoja kajaliwa karama pekee na mola wetu.Kwa hivyo basi ujuaji wako ndo karama yako ya ufahamu wako.
Sasa back to the topic ni kwamba ni kwamba rafki yangu kafiwa na shangazi yake,chanzo alianguka chooni wakati alipo enda kujisaidia.
sasa baada ya kuanguka huyu marehem mama mdomo wake ulikaa upande akapelekwa Hospitali ya Temeke,akalazwa kwa matibabu.
Baada ya wk mbili na nusu huyo Mama (marehemu sasa)akafariki.
Sasa kinachonifanya niiwasilishe hii thread.,ni kuwa taarifa kama hizi kwangu mimi zishanishawishi niamini mtu akianguka chooni huku town basii huyo ni kifo tuu.
Hebu basi wenye ufaham,ushuhuda kama huu na uelewa wa mambo kama haya au yanayohusiana na kuanguka chooni/bafuni baada ya hapo unaugua au kufa,basi tutiririke kuringana na ujuzi,uelewa na ufahamu tulio jaaliwa.
Rest in Peace Shangazi.
Kwa waislam tunaamini kuwa huko chooni kuna wadudu wabaya saana (mashetan) na maumbo yao yapo tafauti ..mfano mtu akianguka chooni..utamuona mdomo wake ..umekuwa upande
.au mokono haifanyi kazi..alimradi hatokuwa sawaa tu..sasa hao wadudu wanakuwa sura zao kama hizo nolizozitaja..mdomo upande n.k. NDio maana mashekhe zetu kila siku anatwambia tusome dua malaum unapoingia chooni na unapotoka salaama ..ili dua hiyo ikukinge na ballaa hilo..
Nashukuru Mungu my dad alipona ye alianguka alikuwa anaoga,japo aliumia sana kwenye maeneo ya nyusi,ni mzima hadi leo,more than 10 yrs,hii kitu nishaisikia sana pia,inahusishwa na nguvu za giza
Hujaumwa wewe na kuanguka chooni na wala usiombe yakukute wewe nenda makaburini kawaulize waliozikwa makaburini walipenda kukaa huko makaburini? kama huyajuwi uliza wenzio wewe mwenyewe. Waswahili wanasema Adhabu ya kaburi aijuaye ni maiti hutaweza kujuwa matatizo ya mashetani mpaka yakukute wewe ndio utayajuwa kama kweli mashetani yapo au hayapo usiombe yakukute utaipata kazi kwako.Mkuu acha mawazo ya kishirikina. Nani aliyechora hizo picha? Mbona walioanguka hawajawahi simulia kuziona au kuona hayo mafudu?
Mimi mwenyewe nilipokua form 5 niliumwaga sana kwa mda mrefu, nilipoenda chooni, sikumbuki kilitokea nini, nilijikuta nipo sakafuni na ni mda mrefu ulipita, ila sikumbuki kuona hayo makitu.
Mimi sipotoshihahahahaha Mtumeeeee, CC. Bujibuji CC. Ilonga Msalabani
Kweli watu wangu wanapotea kwa kukosa ILIM sisi wakristu tunaita elimu.
Mzizi Mkavu kuna mambo unapotosha kila kitu unaweka majini.
Kuna mdau kaelezea vizuri sana hapo juu kuwa ni stroke nothing more nothing less ila hajaelezea namna ya kuiepuka hio stroke ya bafuni na chooni.
Ukiamka asubuhi kitandani au mchana ukiwa umelala, aamka then kaa kwa dakika 5, the shuka kitandani jinyooshe/do some stretching for next 5 minutes. Ukiweza kunywa maji glass moja ambayo ni room temperature. Then nenda bafuni.
kosa kubwa watu wanalofanya ni kukurupuka gafla na kukimbilia bafuni na kuanguka kwa shambulio la moyo. Kuna wengine wanapata Palimonary Emblelism au tiny blood cloting ambazo zina block valvu za moyo.
Sio wote wanaoanguka bafuni hufa mbona Dr. Slaa alianguka na kuvunjika mkono ila alipona?
Hakunaga nguvu za giza au uchawi mkuu, grow up.