Kuanguka chooni/bafuni na kufa, kuna uhusiano gani?


Mkuu soma post #9 ya Mtimti, hiyo ndio sababu kubwa inayowakumba watu - hakuna cha mashetani/nguvuzagiza au nini sijui!!
 
 
hakuna mahusiano yoyote nishadondoka mara kama 3 hivi kwa haraka haraka na mpaka leo nadundika kama kawa....juzi kati mshua kapiga mweleka chooni nikaenda kumkokota mpaka nje ila mpaka leo bado anadundika kama kawa ila kama angeenda kwa mganga saa hizi kishaibiwa kibao kwa kumtafuta mchawi wake
 
labda ni uoga wao tu..mi nimeanguka mara kadhaa bafuni and am alive and kicking and God is always on my side...ila sikujua there's sth btn kuanguka chooni/bafuni na ushirikina

Mkuu wewe inaonyesha una Imani safi,ukishakuwa na Imani unaweza ukapita Sehemu mbalimbali ambazo ni hatarishi pasipo kudhurika.
 

Sawa sawa mkuu!!,hapo ka-mwanga nimekapata kiasi fulani.
 
Chooni hukaa pepo wachafu wa mauti nlisoma kitabu flani kinaelezea ndo mana wa imani flani hutanguliza mguu wa kushoto kabla ya kuingia. Mi mwenyewe hutokea nimeteleza bafuni au toilet hutoka mzima wa afya naamini blood of Jesus

Damu Ya Yesu ni Mwisho wa Mambo yote mkuu!!,
 
bora usiku ,ukianguka chooni mchana wa saa sita hadi saba lazima uvute. Choo ni sehemu chafu na tundu la choo ni kiza kitupu, pepo hukaa humo. choo huhifadhi mambo mengi ,ikiwemo damu ya hedi,shahawa ,vinyesi, nywele za binadamu na maswala ya kiganga

sumbai hili ndio lilikuwa jibu langu asante sana Msulibasi
 
Last edited by a moderator:

Choo cha shimo lililo wazi moja kwa moja huchukuliwa kama mojawapo ya milango ya kuzimu kwakuwa choo kina sifa kadha zinazoshabihiana na kuzimu kama joto kali giza totoro na chini ya ardhi
Sio vyoo vyote vyaweza kuwa hivyo bali vile ambavyo jiografia ya ulimwengu wa roho inavifanya viwe kwenye mkondo wa kuelekea kuzimu
Kuna baadhi ya vyoo vina hiyo sifa kwahiyo havimalizi mwaka bila tukio kama si mtu kufia huko basi mtoto atatupwa au kuna mnyama atatumbukia na kufa
Vile vyoo ambavyo mtoto anatupwa usiku au mtu anatumbukia kisha anasalimika haviko kwenye hilo kundi
 

Nmefafanya incidence tofaut tofauti..but almost vyoo ilivyotokea ni vya kuflashi..ila tukio la kwanza kulitaja ni cha shimo..pia la huyu jirani ni cha shimo...
Nitashukuru kwa ufafanuzi
 

Kwa sisi waislam, mafundisho yanatuelekeza kwamba chooni ni sehemu hatari sana kwani majini wabaya (mashetani) huwa wanapenda kupitapita au hata kukaa baadhi ya nyakati, na hivyo wakati mwingine huweza kumdhuru mtumiaji wa choo mara anapoingia kufanya mahitaji yake.
Kujiepusha na hayo, waislam tumefundishwa kutangulia kuomba dua kabla ya kuingia chooni, hilo tumesisitizwa sana km vile ni lazima, yaani muislam asiingie chooni bila kuomba dua
nashangaa watu wa siku hizi mtu anathubutu kuweka AC chooni
 

Asante kwa hiyo wanaoanguka maybe ni wale wasio omba dua?
 
majini wabaya hupendelea chooni sasa lazma usome dua ya kujikinga nao wakati wa kuingia na kutoka
 
Asante kwa hiyo wanaoanguka maybe ni wale wasio omba dua?

kwakuwa mpangaji wa kila jambo ni Mwenyezi Mungu, yeye ndie anaepanga nini kita kukuta na ni muda gani, yeye M/Mungu ametuelekeza kwa maombi ya dua huwa akipenda anayabadilisha aliyokupangia, kwa hiyo kwa muislam kuomba dua ni kuomba msaada tu juu ya maamuzi ya mwenyezi mungu, yeye ndie ataamua
 
imewahi toke mara kadhaa hapa Dar mtu kuingia chooni na kukuta joka kubwa ukizingatia ni mjini , sasa wahusika huita wataalm na si kupaparika kulipiga
 
Mimi sio daktari lakini nimeona wengi wakianguka bafuni na si chooni. Nadhani watu huwa tunatembea na magonjwa na hatujui ukianza kuoga kujimwagia maji ni kama msukumo wa damu unaongezeka kwa kasi sasa mtu anaweza kuwa na pressure ndio anaanguka. Au jaribu kumaliza kula halafu ukimbie wa speed lazima uzimie so may be supply ya oksijeni kwenye ubongo inakuwa hakuna na msukumo wa damu unaongezeka kwa speed. Ni vizuri tuwe tunacheki afya zetu.
 

Anamaanisha Choo=kinyesi
 
Hapa lazima utolewa ufafanuzi kwa anaefahamu mambo haya,ni KUANGUKA au KUTELEZA NA KUANGUKA CHOONI?maana kama Kuteleza na Kuanguka Chooni mimi nishateleza na kuanguka chooni/Bafuni hata zaidi ya mara 50 na sijaona tukio lolote baya wala hali tofauti kama unavyoteleza na kuanguka sehemu tofauti na Chooni au Bafuni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…