Kuanguka chooni/bafuni na kufa, kuna uhusiano gani?

Kuanguka chooni/bafuni na kufa, kuna uhusiano gani?

mzee meghji nae alifia choonií-½í¹†
 
Mimi sio daktari lakini nimeona wengi wakianguka bafuni na si chooni. Nadhani watu huwa tunatembea na magonjwa na hatujui ukianza kuoga kujimwagia maji ni kama msukumo wa damu unaongezeka kwa kasi sasa mtu anaweza kuwa na pressure ndio anaanguka. Au jaribu kumaliza kula halafu ukimbie wa speed lazima uzimie so may be supply ya oksijeni kwenye ubongo inakuwa hakuna na msukumo wa damu unaongezeka kwa speed. Ni vizuri tuwe tunacheki afya zetu.

Asante sana kwa ufafanuz
 
chooni au bafuni ni miongoni mwa madirisha ya kuzimu, sasa kama hao majini wapo katka shughul zao then ukawabughuzi wanakulapua kofi ILA inategemeana na kinga zako za mwli i.e za mungu kwa waumini au kama umejzndka kwa witch dokta...
 
We jamaa unainekana unapenda ushirikina!!!!!!!
 
Nimekuwa nikishangazwa na hii kitu, nimekuwa shuhuda mara ya tatu sasa watu wangu wa karibu na majirani kila wanapoteleza bafuni basi kama cyo kupoteza maisha ni kuwa mlemavu, nisaidieni bafuni huwa kuna mkosi gani jamani????
 
Kifo ni mpango wa Mungu na kila kifo huwa kina sababu hata kama siku zako zimefika lazima kuwe na chanzo.
 
mi nilidhani kuanguka tu bila sababu, sasa kama wanaanguka kwa kutekeza usitafute mchawi hapo, kama mmeweka tiles(marumaru) basi mzitoe maana hawajazizoea, kama ni sementi tu chini basi muwe mnapiga deki(mop) vizuri kwa kusugua na brashi, na kama yote hayo sio suluhisho basi wekeni zege bafuni ndio iwe sakafu ili wasiteleze tena.
 
Kuna HUBUTH NA HABAITH,,..Kabla hujafanya jambo lolote mtangulize M/MUNGU kwanza...Hayo ni mashetani yanayoishi sehemu hizo..Kila muislam wa kweli Duniani Wanamuomba mungu awaepushe na mashetani hayo mawili tajwa hapo juu..Hayo nikwamujibu wa mafundisho ya mtume (s.a.w)...
 
Kama ni muislam kabla ya kuingia bafuni au msalani basi unatakiwa kuomba dua sehem hizo mapepo wachafu hupenda kukaa huko mwenyezimungu atakulinda Insha'Allah.
 
Pressure, wanapata stroke,hakuna mkosi wala nini.
jitahidi ndugu zako wawe wanajua hali zao za afya, wajiupeshe kwenda kuoga maji baridi pressure ikiwa juu na kujisaidia haja kubwa hasa kwenye choo za kujipinda na kuongeza stress kwenye mishipa.

Pole sana na RIP kwa ndugu zako

Hicho choo cha kujipinda ndiyo kipi mkuu? Ufafanuzi tafadhali.
 
My father survived from this kind of attack, it was in 2013. Nilikuwa likizo, nikaenda naye bush kumsalimia bibi....Uzuri vyoo vya kule ni vya udongo. Namshukuru Mungu, hakuumia na ni mzima mpaka leo. Alianguka alipoingia chooni; When I checked his pressure after the incident it was low & he was hypoglycaemic too. Hii ni kwa sababu alikuwa anasumbuliwa na tumbo tulipofika kule. So, vitu vingi vinachangia yaweza kuwa ni presha ya kupanda au kushuka ghafula mtu atahisi kizunguzungu na kuanguka, Au sukari kushuka pia kunaweza kumsababisha mtu kuanguka. Akianguka vibaya km choo au bafu ni modern wengi huumia ama kupoteza maisha. Ni nadra mtu kuumia if choo/bafu ni cha udongo. Otherwise factors za kiimani zaweza pia included....!
 
NKWESA MAKAMBO UR RIGHT-my DADDY DIED BAFUNI ALISIKIA JOTO AKAOMBA MAJI YA BARAFU AKAWA ANAJIMWAGIA KICHWANI MPAKA AKAANGUKA
 
Kifo ni mpango wa Mungu na kila kifo huwa kina sababu hata kama siku zako zimefika lazima kuwe na chanzo.

Si vifo vyote ni mpango wa Mungu.Unaweza kukataa roho ya mauti na ikakutoka hasa kama roho hiyo ya mauti inasababishwa na uchawi na roho ambazo ziko kinyume na Mungu.Ukiikemea inaondoka na huta kufa kama ujafikia umri wa kufa.Kuna watu wengi hasa vijana na watoto ambao mna zika magogo tu na wenyewe wakiwa bado wanatumika kwenye ulimwengu mwingine kufanya kazi zilizo kinyume na Mungu.Watu hao huja kufa uzeeni baadaye.Ishi maisha ya kumpendeza Mungu na utaona vifo vya ghafla vinatokea kwenye jamii uako mtaishi maisha yaliyojaa heri na fanaka.Na Mungu uwajulisha waja wake kabla kifo akijatokea na kujiandaa na kuaga hata wapendwa wao na huwa hawafi vifi vya gafla wala mateso.Ishi maisha ya usafi ya kumpendeza Mungu bila kujali wewe unaitikadi gani ya dini.
 
Nimekuwa nikishangazwa na hii kitu, nimekuwa shuhuda mara ya tatu sasa watu wangu wa karibu na majirani kila wanapoteleza bafuni basi kama cyo kupoteza maisha ni kuwa mlemavu, nisaidieni bafuni huwa kuna mkosi gani jamani????

Kuanguka bafuni mara nyingi sana huwa ni kuteleza na hasa kwenye mabafu yenye beseni la kuogea. Tatizo ni kwamba mtu aliyesimama huanguka ghafula na kwa kasi ya ajabu kwa kuwa anakuwa amekanyaga sehemu inayoteleza ikisaidiwa na povu la sabuni. Kuumia vibaya au kufa kunasababishwa na sehemu ulipoangukia na kujigonga.

Katika moja ya tukio, nikiwa Monterey, California, USA, asubuhi moja bafuni kwangu nilianguka kwa utelezi huo huo. Mshindo, kasi ya kuanguka na nilipojigonga vilisababisha nikae dakika moja nzima bila kupumua. Ni bahati tu kuwa nilijigonga sehemu ya chini kidogo ya mbavu za kushoto.

Nilikuja kupumua kwa taabu sana baada ya dakika moja na sehemu na kwa siku kadhaa nilibaki na kichomi kikali. Nilipaka vicks kali kwa muda huo.

Hadi leo huwa najiuliza iwapo ningejiginga mbavu zenyewe au ningepiga kichwa au sehemu mbaya zaidi ingekuwaje. Katika maisha yangu sikuwahi kuwa na shinikizo la damu. Hiyo ni moja ya experience kutoka kwangu mwenyewe niliyewahi kuanguka bafuni katika mazingira yasiyosababishwa na ugonjwa wala imani za kishirikina.

Ni bahati pia kuwa nilikuwa Mtanzania pekee yangu na chumba cha pekee yangu. Kama ningeumia sana au kufa ningekuja kugundulika baada ya siku kadhaa na pengine kungekuwa na hadithi nyingi za majumuisho zisizo na ukweli.
 
Ni kweli wengi huanguka bafuni na kufa, kupoteza fahamu au kuumia vibaya ila sio uchawi au nguvu za giza

Athari za kuanguka bafuni hutokana na hali halisi ya bafuni kwenyewe mara nyingi kuna teleza, eneo dogo na mzunguko mdogo wa hewa in some cases hivyo ikitokea mtu kaanguka ni likely akaanguka kwa speed na kuangukia pabaya ukizingatia nyumba za siku hizi marumaru kila kona hadi bafuni.

Wengi wa watu wanaoanguka huwa wana either pressure au kisukari au condition fulani inayokuwa triggered na temp ya maji au chochote wawapo bafuni, kwa kukosa msaada wa haraka huishia kuumia vibaya au kupoteza maisha
 
chooni au bafuni ni miongoni mwa madirisha ya kuzimu, sasa kama hao majini wapo katka shughul zao then ukawabughuzi wanakulapua kofi ILA inategemeana na kinga zako za mwli i.e za mungu kwa waumini au kama umejzndka kwa witch dokta...

Duuuh! We ni wakala wa VIGAGULA. Maaana!
 
Back
Top Bottom