Mwana kinyonga
JF-Expert Member
- Sep 19, 2011
- 377
- 224
Mbona kama sikosei Mzee Slaa tuliambiwa alidondoka chooni akavunja mkono na bado yu hai?
Hata Mkapa kipindi flan akawa anatembelea mkongojo .
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mbona kama sikosei Mzee Slaa tuliambiwa alidondoka chooni akavunja mkono na bado yu hai?
Kwa waislam tunaamini kuwa huko chooni kuna wadudu wabaya saana (mashetan) na maumbo yao yapo tafauti ..mfano mtu akianguka chooni..utamuona mdomo wake ..umekuwa upande
.au mokono haifanyi kazi..alimradi hatokuwa sawaa tu..sasa hao wadudu wanakuwa sura zao kama hizo nolizozitaja..mdomo upande n.k. NDio maana mashekhe zetu kila siku anatwambia tusome dua malaum unapoingia chooni na unapotoka salaama ..ili dua hiyo ikukinge na ballaa hilo..
ukiona mtu kaanguka bafuni au chooni wahi umchane eneo lolote na wembe damu itoke kidogo, baada ya hapo mtoe kwa huduma ya kwanza.
Jamani wana jf.Naamini humu ndani tupo tofauti tofauti na kila mmoja kajaliwa karama pekee na mola wetu.Kwa hivyo basi ujuaji wako ndo karama yako ya ufahamu wako..Sasa back to the topic ni kwamba ni kwamba rafki yangu kafiwa na shangazi yake,chanzo alianguka chooni wakati alipo enda kujisaidia..sasa baada ya kuanguka huyu marehem mama mdomo wake ulikaa upande akapelekwa Hospitali ya Temeke,akalazwa kwa matibabu.Baada ya wk mbili na nusu huyo Mama (marehemu sasa)akafariki.Sasa kinachonifanya niiwasilishe hii thread.,ni kuwa taarifa kama hizi kwangu mimi zishanishawishi niamini mtu akianguka chooni huku town basii huyo ni kifo tuu.Hebu basi wenye ufaham,ushuhuda kama huu na uelewa wa mambo kama haya au yanayohusiana na kuanguka chooni/bafuni baada ya hapo unaugua au kufa,basi tutiririke kuringana na ujuzi,uelewa na ufahamu tulio jaaliwa.Rest in Peace.Shangazi.
hippocratessocrates1gb
Kuanguka chooni itategemea utaitafsiri vipi, mfano kishirikina/kiimani/Kimila/ Kisayansi n.k.
Kishirikina watu huamini, mtu 'amemchawia' mwingine na hivyo kumuadhibu kwa njia hiyo.Hii ipo hadi leo katika jamii yetu.
Kiimani, wengine huamini ni aina ya adhabu kutokana na uovu mtu aliowahi kuufanya na hivyo Mungu kumuadhibu kwa nia hiyo. Au uwepo wa "Majini" kwa wenye kuamini hivyo.
Kisayansi, hali hii inaweza kutokea kwa watu wa aina nyingi lakini Mtu kudondoka Chooni (specifically), hutegemea Jinsia, umri, Kazi, aina ya ugonjwa n.k
Jinsia:
Wanaume- hasa kuanzia umri wa miaka ya 55 kuendelea, zaidi ikiwa kuanzia miaka 65 hadi 70 huwa na ongezeko la ukuaji wa tezi dume (Prostate), hii hufanya kugandamizwa kwa njia ya mkojo na hivyo wakati wa kujisaidia haja ndogo (kukojoa) hutumia nguvu nyingi 'Straining' na kusababisha kuongezeka kwa pressure tumboni ilihali kushuka ghafla kwa msukumo wa damu) na hivyo kuleta kizunguzungu na mtu kudondoka.(same scenario mtu akienda haja kubwa na ku-strain)
Wanawake- Kufikia umri wa miaka 55 na kuendelea(kwa wanawake) hasa ule muda ambao ukomo wa mzunguko/hedhi kukoma wanawake wengi hupatwa na tatizo hili, hasa kutokana na mifupa yako kutokuwa imara.
Pia wanawake wengi waliotunia vidonge vya uzazi wa mpango.
Kazi:
Pili aina ya kazi, wengi wa watu wenye kazi za kuinama...mfano kubeba mizigo, wapishi (hasa migahawa n.k), hupata shida ya pingili za uti wa mgongo, hii huweza kusababisha miguu kukosa nguvu, na mru awapo katika sehemu unayoteleza ni rahisi kuanguka na kuvunjika
Aina ya ugonjwa:
Magonjwa mfano Shinikizo kubwa la damu (Hypertension), na magonjwa mbali mbali ya kifua hutegemea sana uwiano mzuri wa msukumo wa damu na mgandamizo wa hewa, viashiria vya mgandamizo mkubwa (Baroreceptors ) mwilini hutambua endapo kunakuwa na shida hiyo.
Pili, magonjwa ya mifupa kwa aina zake hufanya miguu kutokuwa imara hivyo kazi za kuinama, kuchuchumaa kwa muda mrefu huweza kuwa katika hatari ya kudondoka na kuvunjika .
Hivyo basi the bottomline ni STRAINING activity yeyote yenye kusababisha kubadilika kwa pressure, pamoja na matatizo ya mifupa...na inakuwa chooni, kwa sababu tu ya slippery floor/tiles, straining wakati wa kujisaidia (haja kubwa na haja ndogo).
akikutokea unapiga nae picha halafu unaweka instagram mkuu
Mngojee akutokee kisha upige nae picha Hiram Abiffakikutokea unapiga nae picha halafu unaweka instagram mkuu
Hebu tupate basi uhusiano wa kwenda chooni/Bafuni na STROKE!!!!!!!
Binafsi nalifanyia kazi hilo mkuu ili tupate uhakika. Ni suala la kuvuta subira tutapata uhusiano uliopo.
Very good comment! I second you.
kwa sisi wakristo hakuna haja ya kumchana popote, tunampa damu ya yesu.
Jamani wana jf,
Naamini humu ndani tupo tofauti tofauti na kila mmoja kajaliwa karama pekee na mola wetu.Kwa hivyo basi ujuaji wako ndo karama yako ya ufahamu wako.
Sasa back to the topic ni kwamba ni kwamba rafki yangu kafiwa na shangazi yake,chanzo alianguka chooni wakati alipo enda kujisaidia.
sasa baada ya kuanguka huyu marehem mama mdomo wake ulikaa upande akapelekwa Hospitali ya Temeke,akalazwa kwa matibabu.
Baada ya wk mbili na nusu huyo Mama (marehemu sasa)akafariki.
Sasa kinachonifanya niiwasilishe hii thread.,ni kuwa taarifa kama hizi kwangu mimi zishanishawishi niamini mtu akianguka chooni huku town basii huyo ni kifo tuu.
Hebu basi wenye ufaham,ushuhuda kama huu na uelewa wa mambo kama haya au yanayohusiana na kuanguka chooni/bafuni baada ya hapo unaugua au kufa,basi tutiririke kuringana na ujuzi,uelewa na ufahamu tulio jaaliwa.
Rest in Peace Shangazi.
jamani wana jf,
naamini humu ndani tupo tofauti tofauti na kila mmoja kajaliwa karama pekee na mola wetu.kwa hivyo basi ujuaji wako ndo karama yako ya ufahamu wako.
Sasa back to the topic ni kwamba ni kwamba rafki yangu kafiwa na shangazi yake,chanzo alianguka chooni wakati alipo enda kujisaidia.
Sasa baada ya kuanguka huyu marehem mama mdomo wake ulikaa upande akapelekwa hospitali ya temeke,akalazwa kwa matibabu.
Baada ya wk mbili na nusu huyo mama (marehemu sasa)akafariki.
Sasa kinachonifanya niiwasilishe hii thread.,ni kuwa taarifa kama hizi kwangu mimi zishanishawishi niamini mtu akianguka chooni huku town basii huyo ni kifo tuu.
Hebu basi wenye ufaham,ushuhuda kama huu na uelewa wa mambo kama haya au yanayohusiana na kuanguka chooni/bafuni baada ya hapo unaugua au kufa,basi tutiririke kuringana na ujuzi,uelewa na ufahamu tulio jaaliwa.
Rest in peace shangazi.