Kuanzia kazi kijijini kunaweza kuwa nafasi bingo ya maisha

Kuanzia kazi kijijini kunaweza kuwa nafasi bingo ya maisha

Elimu uliyopata itakusaidia kupambana na hali. Unapokwenda kuchukua mshahara unatafuta na soko la mazao yako huko huko. Kwakua unaajira itakua na smart phone na hela ya bundle, unaweza kuulizia hata JF soko zuri la nyanya linapatikana wapi.
wEWE kuna vijiji huvijui. Hebu siku moja fanya ziara kidogo ufike Handeni ndani ndani huko kwa wazigua, Morogoro ndani kwa wamasai ukajionee.

Kuna vijiji mpaka unajiuliza ni kwanini watu hasa wanaishi huku ?
 
kuna demu alikuwa ticha chimbo fulani ndani ndani kabisa, kila akiamka asubuhi kwanza anakuwa ametoka kwenye usingizi mzito na kaloweshwa sana sehemu zake za siri.[emoji24][emoji24][emoji24]
alikimbia kazi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vijana wengi wamekimbia kazi serikalini (hasa ualimu) kwa changamoto walizokutana nazo vijijini.
Unakuta kijana maisha yake yote yalikua mjini, baadae anakuja kuajiriwa na kupangiwa kituo cha kazi vijijini kabisa tena mbali na kwao. Kijiji hakina huduma za msingi za kijamii. Hakuna maji safi, barabara mbovu, hakuna huduma bora za afya achilia mbali huo umeme. Hapo kijana hakai. Anaacha kila kitu na kusahau suala la ualimu. Anatoka nduki.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Embu tuo mfano wa vijiji vyenye nyumba maji na umeme kama si unaadika kma huijui Tanzania vizur , watu wanapangwa vijiji vya kusini mwa Tanzania yetu hii huduma za kijamii ni mbovu had wengine wanakufa kwa malaria kisa kukosa huduma kwa wakati.

Sent using Jamii Forums mobile app
Jimbo la BUSEGA la dr Raphael Chegeni Kati ya vijiji 59 56 vina umeme
 
Kijijini kuwa Bora au kuwa jau inategemea NDOTO yako kubwa nini kwenye maisha na umeipangilia vipi kuifikia.

Period, mimi nikiajiliwa kijijini nitaomba uhamisho wa DSM na ikishindikana nitafanya kazi kwamuda kwa kukusanya Mtaji then napiga chini hiyo kazi fasta.

Malengo yangu ya maisha nikuwekeza vitega uchumi vyangu vyote DSM na nitakuwa na vitega uchumi sichini ya vitano (5) ambavyo vinahitaji commitment yangu kubwa sana...mikoani (kijijini) nitaenda kwaajili ya kilimo biashara tu ambacho ni njia ya kukuza Mtaji mkubwa basi.

Portfolio | 2020
Inategemea tafsiri yankijiji Mm balaa Dar na fanya Ufugaji na kilimo na Biashara MIKOA MITATU na ni rural Tanga. Arusha Njombe na Niko Dar toka 2012 ila nimekuja mtu mzima Dar
 
Kuanzia kazi kijijini kunaweza kuwa nafasi bingo ya maisha, vijana wengi hawapendi kuanzia kazi vijinini. Hii ni kutokana na miundo mbinu kuwa mibovu zaidi huko vijijini

Fikiria unaanza kazi kama tabibu, nesi, mwalimu, bwana kilimo kijijini. Unakuta kuna nyumba yenye maji na umeme, japo utakatwa katika mshahara pesa ya pango kwakua nyumba ni ya serikali lakini itskupunguzia upungufu.

Ukishazoea mazingira ni rahisi kupata ardhi na kuanza kilimo huku ukiwa mfanyakazi wa serikali. Kilimo kikileta ziada ya mapato unaweza kuanza ujenzi wa nyumba. Ikitokea unahamishwa nyumba unauza au kuipangisha.

Tatizo la kuanza maisha kijijini na unakuta kijiji chote kina nyumba za nyasi na matope. Haya ndiyo matatizo yanayowakayisha tamas vijana kuanzia ajira vijijini.

Mwisho wa mwezi kuufuata mshahara unasafiri siku nzima tena kwa malori ya mkaa.
Kijijini changamoto ni nyingi kuliko mjini, kijijini unakua locked na unakopi maisha ya watu wake kisha hamna utakachofanya, zaidi unajikuta umeangukia Pombe za kienyeji na hata hicho kilimo mbacho ndio fursa pekee inaweza kushindikana vilevile. Mjini kuna fursa nyingi za kila aina kama; biashara, Elimu, networking na Kiu ya mafanikio.
 
Hapa umenena mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Weee nilivyojuwa kusini Kuna vijiji unapita nyumba zote za udongo nikawa nawaza hivi walimu na tabibu wanaishije hapa.Jioni wamekaa barabarani wanapiga stori na wandewa wa vijijini
 
Mkuu Sky Eclat uko sahihi kabisa.

Mimi ni mtumishi wa umma ninayeishi kijijini, ambaye kama ningekuwa naishi mjini na changamoto hizi za kutopanda daraja kwa wakati na no salary increment kwa consecutively 5 years sasa sijui hali yangu ingekuwaje tu.

Imekuwaje kufanya kazi huku kijijini limekuwa jambo jema kwangu? Iko hivi:

1.Kabla sijajenga nyumba yangu nilianza maisha kwa kupanga nyumba nzuri (umeme,kisima, vyumba 2,sebule,stoo,choo na bafu) kwa sh.50,000/= tu kwa mwezi. Ingekuwa ni town pango la nyumba ya aina ile lingekuwa si chini 130,000/= kwa mwezi.

Landlord wangu alikuwa ni Daktari anayefanya kazi na shirika moja ambalo liko affiliated na Johns Hopkins, na jamaa huyu alijenga nyumba hii kijijini kwao kama sehemu ya kukilinda kiwanja chao cha urithi.

2.Nyumba niliyokuja kujenga iko kando kando ya Ziwa Victoria. Hivyo,imenipa fursa ya kuendesha kilimo cha bustani kwa kumwagilia. Si mnamkumbuka kuna miezi fulani hapa nyanya ziliadimika sana?Basi mwenzenu nimepiga pesa nzuri tu kipindi hicho.

3.Kuhusu mlo ndo usiseme!very cheap. Kwakuwa ninaishi karibu na Ziwa napata samaki na dagaa kwa bei ya kutupa. Najua utastaajabu nikikwambia kuwa samaki wa sh.2,000/= (aina ya sangara) huwa tunawala kwa siku 2, kwenye familia yenye watu 4. Kwa ufupi, sh.7,000/= inatosha kwa matumizi ya siku;ugali/wali/ndizi, samaki na matunda.

4.Hizi mvua zilizonyesha (November - hadi sasa May) mmeziona? Basis mimi nimevuna mpunga wa kutosha huku kijijini. Sasa gunia linauzwa huku kwa sh.60,000/= na Mimi sitayauza magunia yangu kwa bei hiyo,ila ninataka niukoboe mpunga wangu na nikauuze town kwa mzani, nimeambiwa Mwanza mchele unauzwa sh.1,000/= au 1,200/= kwa bei ya mashineni. Nikienda kuuza kwa bei hii bado itanilipa tu.

Halafu two weeks ahead nataka kupanda mpunga mwingine wa kumwagilia, mbegu nitakayotumia ni SARO 5, na nataka magunia machache tu, 80 tu yatanitosha.

5.Ninajipanga baada ya corona kuisha nianze kusafirisha dagaa, kutoka huku kijijini (kando ya Ziwa) kwenda Dar es Salaam.Bado naendelea na utafiti kuhusu soko, ila dagaa huku ni wengi sana.

Hii awamu ya 5 isifikiri imenikomesha kwa kutonipandisha daraja na kuninyima nyongeza ya mshahara. Maisha bado nayasongesha. Na pamoja na yote hapo juu,lazima nidai haki zangu za kiutumishi. Pumbavu sana!
 
Safi sana mkuu,hapo umenitamanisha sangara nawakubali mno.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inategemea hasa wewe upo Kijijini lkini kuna Fursa na kimsingi kwa maelezo yako upo mwambao wa Ziwa Victoria kama ni Mwanza au vp apo we lazima Ukijijini wa hapo uwe tofauti na mazingira kame
Nimekuelewa mkuu.Kuna sehemu kwakweli ni balaa tupu.Kwa mfano: kijiji cha Mwanhuzi,mkoani Shinyanga. Ukienda kufanya kazi huko utakula mboga za majani hadi kuta za utumbo wako zibadilike rangi ziwe za kijani.
 
Aisee ndo hivo ndugu inategemea sana na eneo mdau huyu yupo Mwambao wa ziwa sasa hapa yeye ana fursa lazima apende kukaa hapo.
 
Unavoenda kuanza kazi kijijini uwe na mume au mke kabisa vinginevyo upweke utakupelekea kuingia ndoa ya majuto maana hakunaga option cycle ya watu ni ndogo,..Pili vijiji vingi havina umeme Wala network Wala lami hyo nguvu ya kusafirisha mazao utatoa wapi? Acha waliozoea kijijin wakae ila kama hujawahi kanyaga bush utataabika,utachakaa na utapoteza tumaini ndo wale watumishi wanaoishia ulevini
 
Ulichokisema mtoa mada ni kweli japokuwa inategemeana na kijiji ulichopo. Mfano:

Niliajiriwa kijijini sana hakuna maji wala umeme network shida, wenyeji kilugha tupu na wabaguzi kinoma. Kiukweli mara ya kwanza nilipofika nililaani sana na kujiapiza siwezi kumaliza mwaka niwe nimehama, bahati mbaya mishe za kuhama zilibuma ikabidi nitulie. Ila nashukuru kuishi kwangu hapo, kuna kijiji cha jirani ambacho tulikuwa tunanunua mahitaji yetu ya nyumban yaaani ndio sokoni kwetu, maduka ya jumla, sheli ipo na network iko vizuri kiukweli nikavutiwa napo na nikaiona fursa ya kulima mbogamboga.

Nikajiongeza nikatafuta nyumba nikapata nimepanga nyumba ina vyumba 3 sebule na choo maji na umeme full, nalipa elfu 60 tu, pia nalima mboga mboga na mahindi na kufuga sinunui mahindi labda Mchele tu, kwahiyo kuna nnachosave kwenye bajeti ya kununua chakula. Japokuwa changamoto ilikuwa umbali kutoka kile kijiji ambacho ninaishi na kile nnachofanyia kazi. Nilianza kwenda na baiskeli kazini aisee nilipata tabu kwakuwa kuna vilima. Mungu si Athumani, nikanunua kapikipiki kangu kwa mtu. Nafika na kuondoka kazini kwa wakati ni umbali wa dk 20 tu kiukweli nafurahia maisha yangu nimeshaanza kuinua kakibanda changu kwa mshahara na mishe zangu za kilimo na sina mpango wa kuhama kwasasahivi.

Upande wa pili;
Kuna jamaa yangu tuliajiriwa wote yeye alipelekwa mbali kidogo ni kijijini haswa kutoka hapo mpk halmashauri ni elfu 12. Alifanya mishe mpk kuhonga pesa ahame imeshindikana, jamaa kawa mlevi hafai akienda kufata mshahara anakaa hata siku 5 mjini anakunywa, anapiga vizinga balaa mpk namkwepa.

Hitimisho; kuanzia kazi kijijini unaweza kutoboa ila inategemea upo kwenye kijiji kipi? Mjini changamoto nyingi ila kama utaweza kujizuia na anasa na ukatulia kutoboa kuna wezekana.

#StaySafe,CoronaIsReal.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom