Kuanzia kazi kijijini kunaweza kuwa nafasi bingo ya maisha

Kuanzia kazi kijijini kunaweza kuwa nafasi bingo ya maisha

Mkuu Sky Eclat uko sahihi kabisa.

Mimi ni mtumishi wa umma ninayeishi kijijini, ambaye kama ningekuwa naishi mjini na changamoto hizi za kutopanda daraja kwa wakati na no salary increment kwa consecutively 5 years sasa sijui hali yangu ingekuwaje tu.

Imekuwaje kufanya kazi huku kijijini limekuwa jambo jema kwangu? Iko hivi:

1.Kabla sijajenga nyumba yangu nilianza maisha kwa kupanga nyumba nzuri (umeme,kisima, vyumba 2,sebule,stoo,choo na bafu) kwa sh.50,000/= tu kwa mwezi. Ingekuwa ni town pango la nyumba ya aina ile lingekuwa si chini 130,000/= kwa mwezi.

Landlord wangu alikuwa ni Daktari anayefanya kazi na shirika moja ambalo liko affiliated na Johns Hopkins, na jamaa huyu alijenga nyumba hii kijijini kwao kama sehemu ya kukilinda kiwanja chao cha urithi.

2.Nyumba niliyokuja kujenga iko kando kando ya Ziwa Victoria. Hivyo,imenipa fursa ya kuendesha kilimo cha bustani kwa kumwagilia. Si mnamkumbuka kuna miezi fulani hapa nyanya ziliadimika sana?Basi mwenzenu nimepiga pesa nzuri tu kipindi hicho.

3.Kuhusu mlo ndo usiseme!very cheap. Kwakuwa ninaishi karibu na Ziwa napata samaki na dagaa kwa bei ya kutupa. Najua utastaajabu nikikwambia kuwa samaki wa sh.2,000/= (aina ya sangara) huwa tunawala kwa siku 2, kwenye familia yenye watu 4. Kwa ufupi, sh.7,000/= inatosha kwa matumizi ya siku;ugali/wali/ndizi, samaki na matunda.

4.Hizi mvua zilizonyesha (November - hadi sasa May) mmeziona? Basis mimi nimevuna mpunga wa kutosha huku kijijini. Sasa gunia linauzwa huku kwa sh.60,000/= na Mimi sitayauza magunia yangu kwa bei hiyo,ila ninataka niukoboe mpunga wangu na nikauuze town kwa mzani, nimeambiwa Mwanza mchele unauzwa sh.1,000/= au 1,200/= kwa bei ya mashineni. Nikienda kuuza kwa bei hii bado itanilipa tu.

Halafu two weeks ahead nataka kupanda mpunga mwingine wa kumwagilia, mbegu nitakayotumia ni SARO 5, na nataka magunia machache tu, 80 tu yatanitosha.

5.Ninajipanga baada ya corona kuisha nianze kusafirisha dagaa, kutoka huku kijijini (kando ya Ziwa) kwenda Dar es Salaam.Bado naendelea na utafiti kuhusu soko, ila dagaa huku ni wengi sana.

Hii awamu ya 5 isifikiri imenikomesha kwa kutonipandisha daraja na kuninyima nyongeza ya mshahara. Maisha bado nayasongesha. Na pamoja na yote hapo juu,lazima nidai haki zangu za kiutumishi. Pumbavu sana!
Safi

Waache wanaokariri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom