Sikubaliani na kanisa kuhalalisha dhambi badala ya kukema dhambi.
Kuanzia leo mimi si Mkatoliki tena, ninamkataa shetani na kazi zake zote.
Wasinizike wala kunipa huduma zozote wanazodhani ni za kiroho.
Sitahamia kanisa lolote, bali nitaendelea kumuabudu Mungu katika roho na kweli
Waefeso 5:11-17
[11]Wala msishirikiane na matendo yasiyozaa ya giza, bali myakemee;
And have no fellowship with the unfruitful works of darkness, but rather reprove them.
[12]kwa kuwa yanayotendeka kwao kwa siri, ni aibu hata kuyanena.
For it is a shame even to speak of those things which are done of them in secret.
[13]Lakini yote yaliyokemewa hudhihirishwa na nuru maana kila kilichodhihirika ni nuru.
But all things that are reproved are made manifest by the light: for whatsoever doth make manifest is light.
[14]Hivyo husema,
Amka, wewe usinziaye,
Ufufuke katika wafu,
Na Kristo atakuangaza.
Wherefore he saith, Awake thou that sleepest, and arise from the dead, and Christ shall give thee light.
[15]Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima;
See then that ye walk circumspectly, not as fools, but as wise,
[16]mkiukomboa wakati kwa maana zamani hizi ni za uovu.
Redeeming the time, because the days are evil.
[17]Kwa sababu hiyo msiwe wajinga, bali mfahamu ni nini yaliyo mapenzi ya Bwana.
Wherefore be ye not unwise, but understanding what the will of the Lord is.
watu wengi sana wanapoteza uelekeo wa kiimani kwa kukosa uelewa na ufahamu wa kutosha juu ya masuala mbalimbali, mathalani hili la ushoga...
Maeneo mbalimbali duniani, jamii hii ovu imetengwa si tu kiutu bali pia kihuduma na inaangamia kwa mateso makali sana kama vile kukosa huduma za kimwili yaani afya na tiba juu ya maradhi mbalimbali yanayowakumba mfano ukimwi,saratani, malaria, magonjwa ya moyo, ngozi n.k
Lakini pia kukosa huduma za kiroho kama vile Neno la Mungu, kitubio na ekaristi takatifu, kubariki rozali wanazotumia kusali n.k
Anachomaanisha Papa ikiwa padre ameenda hospitali mathalani ocean road kutoa baraka kwa wagonjwa akiwakuta mashoga wagonjwa , nao pia awabariki na kuwapa upako wa wagonjwa....
Ikiwa watu mbalimbali wameenda kanisani mathalani kutaka kitubio na ekaristi takatifu, kubariki Rozali au magari yao, miongoni mwao wakiwemo mashoga nao wabarikiwe... wapewe huduma za kiroho kama wakristo wengineo.
Wasitengwe kama huko kwenye jamii
Kanisa linatoa huduma za afya,
Ikiwa wakristo na wasio wakristo wameenda kupata baraka hiyo ya afya ya mwili kwenye mahospitali ya kanisa, miongoni mwao wakiwemo mashoga nao wapewe baraka hiyo bila kubaguliwa...
Hicho wengi wanachodhani eti kubariki ndoa za kishoga, hakitawahi kutokea ktk kanisa katoliki..
Msimamo wa kanisa katoliki ni mkali sana, ndoa ni sharti iwe ya mtu mume na mtu mke....
Kanisa linahitaji mapadre, masista na waamini. Na waamini wa kanisa katoliki ni sharti wazaliane tena bila uzazi wa mpango....
Ndoa za jinsia moja mtasibiri sana kanisa katoliki...
Mashoga hawazai na wala hawazaliani, yaani kanisa haliwezi kuwa na uovu huu kabisaa...