Kuanzia Sasa Namuomba Mungu Anipe Moyo Mgumu Wa kutokusaidia Binadamu😭

Kwanza amekuhurumia sana hata hapo kwako inaonekana hakuona tu cha kuiba. Wewe sio kwamba eti una moyo wa huruma bali huna reasoning ya kujua ni angle ipi mtu anahitaji msaada na mipaka yake. Kama umeoa au kuolewa jiangalie utakuwa unaibiwa kirahisi sana.
 
Mimi ni mtu ambaye kila mara nilijtahidi kwa kadri ya uwezo wangu kumsaidia mtu yeyote aliyehitaji msaada wangu uwe wa muda, mawazo au ata fedha.

Lakini kwa hili lililonikuta naomba Mungu aondoe spirit hii ndani yangu
Juzi nimekaa ofisin kwangu alikuja jamaa mmoja simfahamu yule jamaa nilidhan anahitaji huduma nilimpokea kwa furaha.

Kumbe hakuhitaji huduma yoyote Bali alihitaji msaada wa Tsh 10k hii ni baada ya yeye kuibiwa kiasi Cha fedha alizokuwa nazo na sehemu aliyokuwa anaenda alikuwa bado hajafika na kwa bahati mbaya usiku ulikuwa umeingia na magari ya kwenda huko hayakuwepo kabisa kwahiyo jamaa alikuwa anahitaji hyo 10k imsaidie kupata sehemu ya kujisitiri ili kesho yake afanye mawasiliano na ndg zake wamtumie nauri na hiyo hela ya kunilipa.

Mwanzoni niligoma kumsaidia ila baada ya kujieleza kwa muda mrefu na ukizingatia ni mwanaume mwenzangu niliamua kumsaidia jamaa akaondoka na Mimi nikafunga ofisi nikaenda zangu nyumbani

Kesho yake akanipigia simu asubuhi na mapema akaniambia kuwa ashafanya mawasiliano Kuna ndg yake anatokea sehemu A hivyo anampitia waendelee na safari ya kwenda nyumbn kwao
Aliendelea kumsubiri hyo ndg Hadi jion hakutokea usiku karudi tena kwangu round hii sikumpatia hela nikaamua kumnunulia chakula na kuambatana nae kwenda nyumbn ili apumzike Kisha kesho aende nyumbn kwake.

Asubuhi ilipofika nikaamka kwenda kazini yeye nikamuacha nyumbn, mchana akaja kazini kwangu akaniaga na kunihaidi kunitumia Ile hela baada ya yeye kuondoka alinipigia simu akiniomba namba ya kuniwekea hela nikamtajia
Baada ya nusu saa nikampigia akapokea akesema anaweka hyo hela Hadi usiku unachukua nafasi hela sikuipata .

Kesho yake namtafuta simu inaita jamaa hapokei nikabadilisha namba nikampigia akapokea aliposikia sauti yangu akakata simu
Hadi nimeishiwa pawa ya kuendelea kumtafuta nikajua tayari jamaa ashaamua kunilipa ubaya😭
Kwa hiyo 10K ndio imekufanya undike uzi. Wenzio tuliwafundisha watu upambanaji, wengine kuwapa elimu na wakatuona mafala. Saidia songa mbele.

wewe inaonekana ulikuwa unamkopesha sio kumsaidia
 
Umesema aliomba msaada ukampa.ten kei,

Akaomba namba akuwekee hela ipi ? Hiyo ten ulitoa sadaka au huku unaumia?

Kwann unambeba mtu usiyemjua mpaka nyumbani kwako ? Huna taarifa zake wala yeye Hana zako?

Ungeibiwa, kuumizwa ?
 
Umeamua kuja kunisema jamiiforum hela yako kausha babu nitakulipaga kwa sasa nataka nitafute kabinti kadogo kanitulize nafis kwanza wewe sio kipaumbele kwa sasa sikilizia utakuja kupata zaidi ya hiyo
 
Mimi ni mtu ambaye kila mara nilijtahidi kwa kadri ya uwezo wangu kumsaidia mtu yeyote aliyehitaji msaada wangu uwe wa muda, mawazo au ata fedha.

Lakini kwa hili lililonikuta naomba Mungu aondoe spirit hii ndani yangu
Juzi nimekaa ofisin kwangu alikuja jamaa mmoja simfahamu yule jamaa nilidhan anahitaji huduma nilimpokea kwa furaha.

Kumbe hakuhitaji huduma yoyote Bali alihitaji msaada wa Tsh 10k hii ni baada ya yeye kuibiwa kiasi Cha fedha alizokuwa nazo na sehemu aliyokuwa anaenda alikuwa bado hajafika na kwa bahati mbaya usiku ulikuwa umeingia na magari ya kwenda huko hayakuwepo kabisa kwahiyo jamaa alikuwa anahitaji hyo 10k imsaidie kupata sehemu ya kujisitiri ili kesho yake afanye mawasiliano na ndg zake wamtumie nauri na hiyo hela ya kunilipa.

Mwanzoni niligoma kumsaidia ila baada ya kujieleza kwa muda mrefu na ukizingatia ni mwanaume mwenzangu niliamua kumsaidia jamaa akaondoka na Mimi nikafunga ofisi nikaenda zangu nyumbani

Kesho yake akanipigia simu asubuhi na mapema akaniambia kuwa ashafanya mawasiliano Kuna ndg yake anatokea sehemu A hivyo anampitia waendelee na safari ya kwenda nyumbn kwao
Aliendelea kumsubiri hyo ndg Hadi jion hakutokea usiku karudi tena kwangu round hii sikumpatia hela nikaamua kumnunulia chakula na kuambatana nae kwenda nyumbn ili apumzike Kisha kesho aende nyumbn kwake.

Asubuhi ilipofika nikaamka kwenda kazini yeye nikamuacha nyumbn, mchana akaja kazini kwangu akaniaga na kunihaidi kunitumia Ile hela baada ya yeye kuondoka alinipigia simu akiniomba namba ya kuniwekea hela nikamtajia
Baada ya nusu saa nikampigia akapokea akesema anaweka hyo hela Hadi usiku unachukua nafasi hela sikuipata .

Kesho yake namtafuta simu inaita jamaa hapokei nikabadilisha namba nikampigia akapokea aliposikia sauti yangu akakata simu
Hadi nimeishiwa pawa ya kuendelea kumtafuta nikajua tayari jamaa ashaamua kunilipa ubaya😭
The best way to avoid disappointment is not to expect anything from anyone. Kilichokufelisha wewe ni kuweka mategemeo. Ulitakiwa kuvunga tu, kama angetuma ni yeye au hata akiacha it's up to him as long umefanya part yako
 
Kwa dunia ilivyo sasa hivi mtu unapataje ujasiri wa kumchukua mtu usiyemfahamu unaenda naye mpaka kwako tena analala kabisa na wewe unapata usingizi, halafu ukaondoka na kumuacha kabisa. Duuh

Kama hujatunga hii habari basi unahitaji kubadilika tena sio kidogo sababu itakuja kukugharimu siku moja.
 
Pole sana mkuu ila usimuamini mtu usiyemjua kumkaribisha nyumbani kwako
 
Nilitegemea kukutana n jambo kubwa ila sio huu upuuzi, kwanza how unampeleka kwako mtu usiyemjua na analala kwako na ww unapata usingizi kabisa how yani how?
 
Back
Top Bottom