Mimi ni mtu ambaye kila mara nilijtahidi kwa kadri ya uwezo wangu kumsaidia mtu yeyote aliyehitaji msaada wangu uwe wa muda, mawazo au ata fedha.
Lakini kwa hili lililonikuta naomba Mungu aondoe spirit hii ndani yangu
Juzi nimekaa ofisin kwangu alikuja jamaa mmoja simfahamu yule jamaa nilidhan anahitaji huduma nilimpokea kwa furaha.
Kumbe hakuhitaji huduma yoyote Bali alihitaji msaada wa Tsh 10k hii ni baada ya yeye kuibiwa kiasi Cha fedha alizokuwa nazo na sehemu aliyokuwa anaenda alikuwa bado hajafika na kwa bahati mbaya usiku ulikuwa umeingia na magari ya kwenda huko hayakuwepo kabisa kwahiyo jamaa alikuwa anahitaji hyo 10k imsaidie kupata sehemu ya kujisitiri ili kesho yake afanye mawasiliano na ndg zake wamtumie nauri na hiyo hela ya kunilipa.
Mwanzoni niligoma kumsaidia ila baada ya kujieleza kwa muda mrefu na ukizingatia ni mwanaume mwenzangu niliamua kumsaidia jamaa akaondoka na Mimi nikafunga ofisi nikaenda zangu nyumbani
Kesho yake akanipigia simu asubuhi na mapema akaniambia kuwa ashafanya mawasiliano Kuna ndg yake anatokea sehemu A hivyo anampitia waendelee na safari ya kwenda nyumbn kwao
Aliendelea kumsubiri hyo ndg Hadi jion hakutokea usiku karudi tena kwangu round hii sikumpatia hela nikaamua kumnunulia chakula na kuambatana nae kwenda nyumbn ili apumzike Kisha kesho aende nyumbn kwake.
Asubuhi ilipofika nikaamka kwenda kazini yeye nikamuacha nyumbn, mchana akaja kazini kwangu akaniaga na kunihaidi kunitumia Ile hela baada ya yeye kuondoka alinipigia simu akiniomba namba ya kuniwekea hela nikamtajia
Baada ya nusu saa nikampigia akapokea akesema anaweka hyo hela Hadi usiku unachukua nafasi hela sikuipata .
Kesho yake namtafuta simu inaita jamaa hapokei nikabadilisha namba nikampigia akapokea aliposikia sauti yangu akakata simu
Hadi nimeishiwa pawa ya kuendelea kumtafuta nikajua tayari jamaa ashaamua kunilipa ubayağŸ˜