Kuanzia Sasa Namuomba Mungu Anipe Moyo Mgumu Wa kutokusaidia Binadamu😭

Kwamba mtoa mada ni mlalahoi mpaka jamaa akakosa cha kuiba ndani?
😂 Ndani ya chumba kwa mtoa mada kuna kiwanja 😂
 
Kesho yake namtafuta simu inaita jamaa hapokei nikabadilisha namba nikampigia akapokea aliposikia sauti yangu akakata simu
Hadi nimeishiwa pawa ya kuendelea kumtafuta nikajua tayari jamaa ashaamua kunilipa ubaya😭
Joshua wewe ni Mwanaume mkuu mara mia ungekua Ester sasa Joshua unalilia 10,000 kweli mkuu 10,000 inakutoa kamasi mkuu?
 
Nilitegemea kukutana n jambo kubwa ila sio huu upuuzi, kwanza how unampeleka kwako mtu usiyemjua na analala kwako na ww unapata usingizi kabisa how yani how?
Mimi siwezi hata kidogo hata niwe na huruma kiasi gani anaweza akalala nje mimi nikalala ndani anilindie geti ila sio kumzamisha ndani
 
Kwa hio unalilia elfu 10 nikadhani alikuibia ulipomuachia nyumba
Bro katika maisha tunatofautiana viwango
Hyo 10k kwako yaweza kuwa hela ya kununuli pumba ya kuku tena kwa siku tu
Lakini hyo hyo 10k kwa mwingne ni bill ya chakula Cha wiki na mtaji juu
 
Mie sio bro. Kingine hio 10k ni ndogo sana kuliko uhai uliorisk kwa kumkaribisha nyumbani kwako na kumuachia nyumba mtu hata haumfahamu
Bro katika maisha tunatofautiana viwango
Hyo 10k kwako yaweza kuwa hela ya kununuli pumba ya kuku tena kwa siku tu
Lakini hyo hyo 10k kwa mwingne ni bill ya chakula Cha wiki na mtaji juu
 
Buku 10 mzee,hiyo ni sadaka mi nilijua kasafisha Gheto
 
Sasa kwa akili yako alikuwa na shida ya 10 k ameipataje kwa haraka hivo
 
Naona kama CHAI vile ya suturungi 😀 😀 😀 😀
 
Una point japo hiyo ten isikulalamishe hivyo. Point ni kila unapotaka kusaidia binadamu zingatia iwe katika mazingira ambayo huwezi kuumizwa pakubwa. Usamaria wema una gharama zake hivyo WEMA uwe na kiasi
 
Bado "li-ten" lako linakuuma sana mkuu?Ukimsaidia au kumkopesha mtu,iambie nafsi yako ulichotoa ndiyo kwa heri ili kupunguza uchungu.
 
Nilivyoanza kusoma nikajitungia story yangu kichwani nakuja kukutana na malalamiko hujalipwa 10k.....mtu humjui halafu unamkaribisha alale na unamwacha kwako kweli???
Inabidi ujitathimini mno
 
Mkuu potezea toka mwanzo uliamua kumsaidia unaweza kumlaumu halafu siku anakuja kukupa misaada zaidi yahuo utajisikia vibaya
 

Nimeona huna akili kumkaribisha mtu kulala kwako. Kuhusu 10,000 fanya umemsadia. Songa mbele. Usije lalamika lalamika humu. Weka namba ya simu nikurudishie kwa niaba yake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…