Kuanzisha biashara ni jambo gumu sana kuliko kutafuta ajira

Hawa ng'ombe bila shaka ni lazima uwe Kijijini , huku Dar utawalisha Nini?

Mkuu inavyosemekana Darslum kwa Sasa ni moja ya mikoa yenye ng’ombe wengi wa maziwa kwa sasa, fanya utafiti vizuri, vyakula ni aghari lakini watu wanasafirisha na soko lake ni kubwa na bei ya maziwa ni kubwa pia I.e lita moja elfu 2,000
 
Kweli....
 
Mkuu kama uko serious njoo nikupe conection kwa milioni moja
Yani mimi utanipa milioni moja kwa kukupa hilo wazo la biashara na siyo wazo ni kuwa wakala wa bidhaa fulani kwenye kampuni wao wana kiwango chao ambacho watataka uwape ambacho ni milioni 15 alafu eneo la kazi/ofisi watakupa wao kodi hulipi
hiyo 15 watakupa mzigo wa kuendana na hiyo hela
Ukiuza wewe unapeleka hela faida unabaki nayo wanakuletea tena mzigo kadiri utakavyowapa oda
Na uhakika baada ya mda miezi michache tu kuingiza laki mbili kwa siku na kuendelea kama faida itakuwa ni kitu cha kawaida
Utahitaji kuwa na wafanyakazi kama watatu hivi kama wewe mwenyewe hutataka kuwa sehemu ya wafanyakazi kwenye ofisi yako
 
Hiyo bidhaa inatokaa ama ndo unapewa inakufia dukan
 
Hii haina tofauti na biashara ya QNET
 
Naskia harufu ya global alliance na yale mabidhaa yasiyouzika[emoji4][emoji4][emoji4]
 
Kiwanja kipo sehemu gani mkuu,size yake and the price if you don't mind
 
Biashara ni KIPAJI mzee,sio kila mtu anacho!...nilianza na biashara sina mtaji yaan nachukua mzigo kwa “malikauli"
Ndio kanuni ya biashara inavyotaka baadae ukipata pesa utakuwa na uchungu nayo,ila anayeanza na mahela mengi ni ngumu kutoboa kwa sababu hana presha atakuwa analala hadi saa nne asubuhi ndio akafungue biashara
 
Kinachofurahisha kwa wabongo ni kwamba wao hawanaga mitaji ila wana idea za business tu[emoji23][emoji23]
Hata ideas za biashara walizonazo ni za copy & paste.
Ideas za biashara zenye ubunifu halisi zinatakiwa zenyewe ndio zikupe mtaji na zikuvushe na kukupeleka kwenye level zingine.

Sent from my SM-C7000 using JamiiForums mobile app
 
Nani huyo anaekwambia Sumbawanga hakuna mahindi? Mahindi yapo sana serikali inaendelea na manunuzi lakin saiz hakuna hela watu wengi tunadai hatujalipwa kwaiyo huu ni wakati mzuri wa kununua mahindi maana wafanyabiashara wengi hela ziko NFRA hawaendi kununua kwa mkulima hii imepelekea Bei ya mahindi kushuka
 
dah mwamba una pesa mpka sasa umeshindwa kuizungushia dah aisee
 
Mkuu usumize kichwa sana. Hebu nunua treasury bonds halafu ukae usikilizie faida. Utakuja kunikumbuka.
 
Niliwai kufanya biashara ya vinywaji baridi jumla lakini Ile ni kupoteza muda, wanaoweza ni akina mangi wanaoweza kudunduliza, miaka nenda miaka Rudi unamkuta pale pale.
Mkuu biashara yoyote inahitaji commitment, concentration and, most importantly, CONSISTENCE. Hapa ndipo wenzetu wakinga na wachaga wanapotuacha nyuma.
 
Chukua mzigo wa mbao njoo nao Zanzibar maelezo zaidi njoo inbox
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…