Kuanzisha biashara ni jambo gumu sana kuliko kutafuta ajira

Kuanzisha biashara ni jambo gumu sana kuliko kutafuta ajira

Ni muda wa miezi kadhaa,sasa Niko na mtaji mkononi wa zaidi ya 40m nimejitahidi kutafuta biashara ya kufanya nimegonga mwamba.

Nimetafuta frame ili nianze biashara ya uwakala wa pesa ,Bank Wakala,na Mitandao ya simu. Nimekumbana na Kodi kubwa ya frame lakini pia location ya frame Kwa biashara husika haziendani kabisa, nimewaza kuuza nafaka Nako NILIFANYA analysis naona kama mtajinunaenda kudidimia huko, Nikawaza kilimo nikakumbuka kilishanizamisha mwaka juzi, Nikawaza nifungue duka la jumla Nikawaza nani akae pale na faida yake uwa ni kidogo sana hii biashara nikiangalia wanaofanya hawaendelei

Nimejaribu kutoa mtaji kidogo nikampeleka mtu anunue mahindi sumbawanga lakini wapi siku hizi mahidi hamna kule, serikali imeingia hadi wilayani kukusanya mahindi.

Mpaka sasa naona mtaji kila siku unazidi kupungua, kila baada ya week naona milioni inaondoka hata sijui nafanyia Nini.

Kimsingi kwa Africa hasa TZ kutunzia hela unaangalia si mchezo zinaisha bila kujua ulichofanya.

Na hii ikiisha sijui nitakuwa mtoto wa nani,juzi nilienda bank wakaniambia imebaki 33m.

Hapa sielewi kabisa.
Zipo njia nzuri tu , Huna haja ya kuumiza kichwa tena kuhusu mkataba

Nina tatizo kama lako ila mimi nataka kubadilisha tu biashara. Nilifanya biashara nimapata ziaid ya milion 21.

Kwa sasa nataka kubadilisha biashara. Amini usiamini huu ni mwezi wa 7 sijajua biashara nyingine ya kufanya.

Nipo tu, mzigo ulikuwa milion 21 kwa sasa nimebakiza 16.
Unataka kutoka kwenye biashara gani?
 
Wewe jamaa ni masikini wa kiroho. Huu ndio umasikini hatari kuliko wowote ule .Leo una million 30 unashindwa, ukiitafuna yote ikaisha utaweza kusimama kweli?

Anyway hizo pesa huja tolea jasho kuzipata hata shilingi 1, pengine za urithi, mkopo au bahati nasibu.

Kitendo cha kupukutisha hiyo pesa hadi kufika million 33 bila kufanya lolote wewe ni wakuhurumiwa. Yaani nikama maiti ambayo iko mochwari inasubiri sanda ikafukiwe.

Inaonekana hata elimu ya fedha huna. Pesa hailindwi kwa kuificha ndani bila kuizalisha itaisha. Utaitumia kidogo kidogo Yaani itapukutika hata usiamini tena ndio unafamilia . Kama huamini njoo hapa January tupige hesabu utakuwa umebaki na ngapi.

Ushauri wangu kabla mambo hayajawa mabaya tafuta kazi ya ofisini ufanye utakayo kuwa unaingiza pato kila mwisho wa mwezi .

Kuna mfanya biashara sasa hivi ana mtaji wa 5M kwa macho ya kawaida ni ndogo kuliko hiyi milion 33 yako. Ila kibiashara ana mtaji mkubwa kukuliko jaribu kutafakari uchukue hatua.

Sent from my SM-A025U using JamiiForums mobile app
Akili ya biashara atapata baada ya kubaki na 2M na hapo ndio atakapoanza kuinuka tena.Hela ikiwa nyingi mkononi kunakua na ideas nyingi sana na mara nyingi zinakua chenga.Pesa ikibaki kidogo atapata akili tu
 
Ni uhakika mkuu, unanunua ng'ombe akiwa na mimba mkuu, mimi mpaka sasa sina passion ya kufuga kabisa ila inabidi kufuga maana pesa ipo nyingi, ukiwa na ng'ombe watano tu wa maziwa pure breeding wanakuzalishia shilingi milioni 5 kila mwezi.
Mkuu running costs zake zikoje

Shusha gharama za kuwahudumia hao ng'ombe wa5 Kwa mwezi.
 
Ni muda wa miezi kadhaa, sasa niko na mtaji mkononi wa zaidi ya 40m nimejitahidi kutafuta biashara ya kufanya nimegonga mwamba.

Nimetafuta frame ili nianze biashara ya uwakala wa pesa, Bank Wakala na Mitandao ya simu. Nimekumbana na Kodi kubwa ya frame lakini pia location ya frame Kwa biashara husika haziendani kabisa, nimewaza kuuza nafaka Nako NILIFANYA analysis naona kama mtaji unaenda kudidimia huko, Nikawaza kilimo nikakumbuka kilishanizamisha mwaka juzi, Nikawaza nifungue duka la jumla nikawaza nani akae pale na faida yake huwa ni kidogo sana hii biashara, nikiangalia wanaofanya hawaendelei.

Nimejaribu kutoa mtaji kidogo nikampeleka mtu anunue mahindi Sumbawanga lakini wapi siku hizi mahindi hamna kule, Serikali imeingia hadi wilayani kukusanya mahindi.

Mpaka sasa naona mtaji kila siku unazidi kupungua, kila baada ya week naona milioni inaondoka hata sijui nafanyia Nini.

Kimsingi kwa Afrika hasa TZ kutunzia hela unaangalia si mchezo zinaisha bila kujua ulichofanya.

Na hii ikiisha sijui nitakuwa mtoto wa nani, juzi nilienda bank wakaniambia imebaki 33m.

Hapa sielewi kabisa.
Biashara unatakiwa kuianza kidogo. Ilitakiwa uanze na mtaji mdogo then mazingira na soko ndo litakufundisha jinsi ya kuiendeleza au kuikuza. Hautakiwi kuanza na mtaji mkubwa.
 
Ni muda wa miezi kadhaa, sasa niko na mtaji mkononi wa zaidi ya 40m nimejitahidi kutafuta biashara ya kufanya nimegonga mwamba.

Nimetafuta frame ili nianze biashara ya uwakala wa pesa, Bank Wakala na Mitandao ya simu. Nimekumbana na Kodi kubwa ya frame lakini pia location ya frame Kwa biashara husika haziendani kabisa, nimewaza kuuza nafaka Nako NILIFANYA analysis naona kama mtaji unaenda kudidimia huko, Nikawaza kilimo nikakumbuka kilishanizamisha mwaka juzi, Nikawaza nifungue duka la jumla nikawaza nani akae pale na faida yake huwa ni kidogo sana hii biashara, nikiangalia wanaofanya hawaendelei.

Nimejaribu kutoa mtaji kidogo nikampeleka mtu anunue mahindi Sumbawanga lakini wapi siku hizi mahindi hamna kule, Serikali imeingia hadi wilayani kukusanya mahindi.

Mpaka sasa naona mtaji kila siku unazidi kupungua, kila baada ya week naona milioni inaondoka hata sijui nafanyia Nini.

Kimsingi kwa Afrika hasa TZ kutunzia hela unaangalia si mchezo zinaisha bila kujua ulichofanya.

Na hii ikiisha sijui nitakuwa mtoto wa nani, juzi nilienda bank wakaniambia imebaki 33m.

Hapa sielewi kabisa.
pharmacy
 
Kiongozi, nunua Kirikuu/Carry then tafuta eneo la kutosha na likiwa fenced itapendeza zaidi, ukipata mashine ya kuchakata plastic anza hiyo biashara ya maplastiki.

Unazunguka na Carry yako unachukua mzigo kwa wale wanaonunua plastic kutoka kwa mateja ili wapeleke wakauze kiwandani, nunua kwa hao unazichakata vizuri mzigo ukiwa wa kutosha unapeleka kwa mchina unauza bei ya juu coz tayari umeshazichakata.

Unaweza ukawa unatafuta na oil chafu pamoja na chuma chakavu unanunua mtaani unaenda kuuza viwandani, utakuja kuleta mrejesho hapa.

Kila la heri ndugu...!

Oil chafu inatumika kwaajil ya nini na wateja wako wapi ?
 
Nina kiwanja sehemu huko kigamboni nimetafuta wateja mwaka wa tano huu sipati yaani Ardhi inahitaji uwe na hela usiyoitegemea ili uzamishe uko isahau utauza siku pakichangamka. Lakini hizi za kwetu tunazotegemea tuzalishe ili tupanuke haraka maisha yaendelee si mchezo

Brother ni Kigamboni sehemu gani ambapo una plot na imekosa soko? Unless kiwanja kipo eneo ambalo halifikiki kirahisi, this can not be any further from the truth.

Japo nakubali ni kweli kwamba biashara ya ardhi inahitaji uwe na hela ambayo hauitegemei kwenye mzunguko wa kila siku ila it's the most ideal kwako kwakua umeshatanabaisha kwamba una wasiwasi na kila wazo la biashara unalopata kuhusu uhakika wa return yake. Biashara ya ardhi odds zote zikibaki constant, basi uhakika wa kupata faida ni 100% guaranteed.

Naungana na member mmoja hapo juu kukushauri hiyo hela ujengee nyumba ya kupanga. Ukishirikisha wataalamu na ukasimamia vizuri, million 35 inatosha kabisa kupata nyumba ya kupangisha.

Kuhusu aina ya nyumba, kama eneo lako lipo karibu na ferry (kwaajili ya urahisi wa wanachuo ambao ndo wengi)basi jenga zile nyumba kama hall (tranka) kisha uigawe kwa vyumba self-contained. Hapo uhakika kupata kodi 100k - 120k per month kwa idadi ya vyumba vilivyopo. Kama eneo liko mbali kidogo na ferry basi jenga nyumba ndogo tu iwe classy kwaajili ya kupangisha mtu mmoja na familia yake halafu uchukue angalau 250k kwa mwezi. Baada ya mwaka unaanza harakati za kutafuta mteja wa nyumba yote.

Niko Kigamboni mwaka wa 4 huu hivyo kwa ufahamu wangu, naiona kabisa hela yako ikirudi.
 
Jambo zuri zaidi ni kutafuta experience katika biashara yoyote ile,then after experience pesa inakujaga baadae.

Ndio maana biashara nyingi huwa zinakufa mwanzoni kwa sababu zinahitaji experience,na experience huja kwenye changamoto,na wengi wakipata changamoto wanapotea.

Ndio maana tunasema kwamba biashara mpya ni kama mtoto,anahitaji kutunzwa na kufuatiliwa.
.biashara mpya inatakiwa uingize pesa ambayo UPO TAYARI KUIPOTEZA kwa sababu biashara mpya inachangamoto nyingi ambazo hujazijua.

Solution ya haya yote ni kutafuta mtu ambaye ana experience na biashara husika mkafanya ili kwenye changamoto yeye ajue anazipitaje kwa sababu tayari ni mzoefu.

You've said it all.
 
Ni uhakika mkuu, unanunua ng'ombe akiwa na mimba mkuu, mimi mpaka sasa sina passion ya kufuga kabisa ila inabidi kufuga maana pesa ipo nyingi, ukiwa na ng'ombe watano tu wa maziwa pure breeding wanakuzalishia shilingi milioni 5 kila mwezi.

Hakika mkuu! Mimi nishajenga passion ya ufugaji kwa muda sasa ni kitu nitafanya hata nikistaafu kazi ya Jamhuri! So far mwezi ujao Nitaanza ujenzi wa sehemu ya kufugia ng’ombe hao na soko lipo la uhakika eneo nilipopata kiwanja kwa hesabu zangu ng’ombe wa maziwa Wana faida ukiweka management vizuri ukipanda na malisho.
 
Back
Top Bottom