connections
JF-Expert Member
- Apr 27, 2013
- 2,190
- 3,039
Samahani kutoka kwenye mada. Huu uzi umenifurahisha na kunipa moyo kuwa hapa JF kuna watu wenye hekima ambao wana uwezo wa kufikiria na kuchangia bila kuvuruga mada - kuanzia mtoa mada na wote wachangiaji nyuzi zote ni busara na kwanye nukta. sijaona mchafuzi wa mada. naomba mambo yaendelee kwa njia hi na mleta mada namuombea mafanikio
kaka achana na vyuo vya ualimu maana kwanza ada yao ni ndogo mno maana huko vyuo vya serikali wanalipa 170,000/= kwa mwaka tena hapo ni boarding na nafasi kibao zinabaki kila mwaka maana wengi siku hiz wanakimbilia vyuo vikuu vilivyojaa kama uyoga kila kona. we anzisha kozi zinazovutia wajinga wajinga (BUSINESS MANAGEMENT, IT, TOURISM, HUMAN RESOURCE MGT, LAW (certificate), LOGISTICS, INTERNATIONAL TRADE, COUNSELLING, CUSTOMER SERVICE, MARKETING, TRAVEL & TOURS basi tu kuwavutia watu ili upate pesa. Mjini mipango kaka usipokuwa mjanja unalala njaaa
Nilisha download na nikaanza kushughulikia kibali kutoka wilayani, lakini katika masharti hayo yote haijaeleza kama kuna malipo ya kila mwaka kulipa serikalini,pia sina uzoefu na hawa jamaa wa ukaguzi ambao watatakiwa kuja kukagua na katika suala nzima la uongozi kwani ni lazima kuajiri walimu wawili watatu hivi kuanza nao hivyo nikaona niombe msaada wa ushauri kwa wana Jamii Forum kwa huu ni msitu mnene wenye kila aina ya watu wenye kufanya bishara mbalimbali.mimi sijawahi kuwa kiongozi zaidi ya kuwahi darasani kufundisha.