Kuanzisha Shule ya Msingi na Sekondari: Utaratibu wa Kiserikali, Ushauri, Changamoto na Faida

Kuanzisha Shule ya Msingi na Sekondari: Utaratibu wa Kiserikali, Ushauri, Changamoto na Faida

mwenye shria ya elimu No. 25 ya 1978 atuwekee hapa tafadhali
 
Kama ni ya awali tafuta pagala karibu na nyumbani kwako uanze kazi. Usisahau kumuajiri Nuru wangu.
 
Nakushauri kodi majengo anzisha tuition-center. Hela ya karanga hiyo, shule sio mchezo
 
Anataka kujua gharama na taratibu NI HILO TU ushauri ungempa baada ya kujibu swali lake
 
Wadau wa Elimu habari zenu! Naomba ufadhili wa kuanzisha shule ya secondary! Naomba wadau.
 
Habari zenu wana-Jamiiforum,
*HISTORIA FUPI*
Nimekuwa na ndoto ya kuanzisha biashara ya kudumu (Ya kitaasisi) kwa muda mrefu sana, na ndoto hii ilianza tangu nikiwa kidato cha sita miaka ya 2000.

Moja ya vitu ambavyo nimewahi kujaribu na kwa sehemu flani nilifika hatua flani ambayo si ya kuita mafanikio, la hasha lakini mchakato (Process) ni kama ifuatavyo;

1. 2009-Nikiwa nimeajiriwa, niliweza kuanzisha NGO pamoja na rafiki na family friend, wakati huo yeye akiwa bado chuoni (Mwenye ndoto za kisiasa pia). Tuliweza kufanya usajili na kupata ofisi maeneo ya Mwanza, tukapata site sehemu ambayo ingetumika kama Project site kulingana na lengo na mipango ya NGO. Hii hatukuweza kwenda mbali sana baada ya rafiki yangu kufanikiwa kupata ubunge na kujikita kwenye siasa, huku mimi nikiwa bado kazini.

2. 2011-Nikiwa na huyu bwana tena, wakati huo akiwa Mbunge, tulianzisha kampuni na malengo makubw aikiwa ni kuingia kwenye biashara mbalimbali ikiwa ni pamoja na kilimo na ufugaji. Tuliweza kununua ekari 100 maeneo ya Mkuranga kwa lengo kufanya kilomo na ufugaji wa kisasa kabisa. Pia tukiwa na usajili wa kampuni, tuliweza kupata ofisi maeneo ya Mkumbusho, kulipia na kufanya designing-Hii nayo haikuwezekana ikaishia njiani.

3. 2015- Niliamua kufungua kampuni yangu binafsi na mke wangu, tulikamilisha usajiri na hatua zote, tulipata frem ya biashara, na tulianza biashara ya Huduma za fedha na baada vipozodi ambalo mpaka sasa linaendelea, ingawa huduma za fedha (M-PESA, TIGO NA HALOPESA) tumesitisha kwa muda. Malengo makubwa ni kuweza kufanya biashara na ofisi binafsi kama NGO na serikali na tunampango wa kujisajili GPSAA ili kuweza kupata fursa hizo.

4. 2015- Niliweza kununua ekari 5 za Shamba maeneo ya Bagamoyo,lengo kuu ikiwa ni kilimo na ufugaji wa kisasa, lakini ambacho kilinikwambisha ni upatikanaji wa maji. Nilipeleka wataalamu wa ku-drill kisima, maji yapo 130m, na gharama ilipaswa kuwa 10,540,000/= Nikashindwa kwa kuwa budget yangu ilikuwa ni only 5m.

5. 2017- Niliweza kununua maeneo kadhaa Dodoma, maeneo mawili tofauti kuna ekari 1 kila eneo, na eneo lingine lina ekari 2. Eneo la ekari 2 na 1 yote yapo nje ya mji kidogo umbali wa 12km toka Dodoma Mjini. Eneo la ekari moja tayari limepimwa kwa ajili ya makazi, bado tunasubiri hati kutolewa.

SHULE KWENYE ENEO LA EKARI 2
Ushauri wenu wana-Jamii.
Kwakuwa Dodoma unakuwa Makao mkuu wa nchi na kwa kukuwa, shughuli nyingi za serikali zimehamia huko, na kwakuwa projection inaonyesha kutakuwa na ongezeko la watu na mahitaji kuongezeka, ikiwa ni pamoja na taasisi za kifedha na shule, kwa kuamini wafanyakazi na wafanyabiashara wakazi na wahamiaji wanalo hitaji hili kwa sababu ya watoto wao.

Na kwakuwa maisha bado yanaendelea na hitaji la shule kwa kikazi ni muhimu sana. Na kwakuwa pia Eneo lipo karibu na barabara kuu ambayo TARURA wapo kwenye mpango wa kui-upgrade kwenye kiwango cha Changarawe na baadae Lami, na kwa kuwa Halimashauri tayari eneo moja yaaani upnde mmoja wa eneo lote umekamika utaraibu wa upimaji, na eneo linalofuata ni eneo ambalo ninazo hizo ekari 2. Na kwakuwa eneo la ekari 2 na hilo la ekari 1 (ambalo upimaji tayari umkamilika), ni maeneo ya makazi tayari, na huduma zote muhimu kama umeme, maji na barabara vipo, na kwakuwa mke wangu kitaaluma ni mwalimu na HR pia (Kwa kuwa amefanya mastaers ya HR-UDBS), na kwakuwa mimi pia ni Administrator mzuri na mwenye uzoefu wa kuongoza watu kwa zaidi ya miaka 13 ambayo nimekuwa kazini.

Hivyo basi nafikiri kuanzisha shule mahali hapo linaweza kuwa ni wazo sahihi sana, ingawa sina uzoefu, sina taarifa za kutosha, wala sijui gharama zipi zitakutakiwa kuweza kufanya hii project to success, hata kama return on investment siitarajii kuipata in less than 5 years, lakini nahitaji kufanya hili kwa kupata msaada wenu.

Naombeni ushauri, mawazo na njia sahihi ya kuwea kulifanya hili.

NB:
Nmeshalifanyia utafiti eneo, bado Halimashauri hawajalipangia matumizi,(Hakuna TP), hivyo niliongea na mtaaramu mmoja wa masuala ya upimaji (Kampuni binafsi), wamenishauri kuweza kulipima na kuweza kupata viwaja. Na gharama ya kufanya hivyo tayari ameshanipati.

Hii inatokana na ukweli kwamba kwa kufanya hivyo itanisaidia hata Halimashauri watakapokuja kufanya upimaji maana yake watakuta tayari eneo langu limeshapimwa na hivyo halitapata changamoto yoyote.
 
Mkuu njoo PM tujadili,naona kuna ndoto kubwa ambayo inahitaji STRATEGIC thinking badili ya Popular Opinion
 
Back
Top Bottom