Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Asante diranqhe. Nitajitahidi, ila umesema shule ina mambo mengi, yapi hayo? Ukitoa gharama za uendeshaji (yaani mishahara ya walimu na walinzi max. 3)
Wewe umemaliza kitu.. asipofuata huu ushauri atakuwa na lake jambo. 8m ni kidogo sana kwa shule ya sekondari. Kama angekuwa na angalau 100m ningesema asonge mbele.Kwa wenye ndoto za kuwa na shule. Please anzia hapa. Sio lazima uanze kujenga shule na kujitanagaza unajenga shule. Jenga vyumba viwili vya ukubwa wa madarasa andikisha watoto wa nursery school waanze kusoma.Then fuatilia usajili wa nursery school ambao hauchukui mda mrefu. Then kupitia hao watoto wa nursery utapata uzoef wa kuendesha shule for one to two years.
Ndani ya hiyo miaka weka tuition ya jioni ya wanafunzi wa msingi na secondari kuendeleza kipato na kukuza kituo.Maana kwa mda huo itakuwq nursery na tuition center. Ukishajipanga ndo uanze kufuatilia taratibu za usajili ujitahidi kiwafuata right people kuwauliza taratibu za usajili. Hasa hawa wanaomiliki shule watakusaidia. Ukipata majibu ya kukatisha tamaa kwa mmoja jaribu kwingine.Hii ni kwa eng medium pri and primary school.
Mimi nasimamia shule amabayo boss wangu alianza hivyo na sasa hivi ndo tupo kwenye hatua za mwesho za uasajili ila tuna hadi darasa la pili wanasomea kule nursery. Cha msingi ni elimu bora ambayo itamfanya mzazi akutangazie shule.
Kwa secondary sina uzoef sana japo tuna mpango wa kujenga. Kama kipato chako ni cha chini anziaha tuition Centre ambayo haihitaji hata kuwa na kabali cha kuendesha. Naomba niishie hapa kwa hiki kidogo mnaotaka kuanzisha shule mtajifuza kitu.
Thanks Quote Reply
Select for moderation Edit History Ban
Asante sana MALILA;
Kwa ujumla nilishapata kama heka 6 nje kidogo ya pale niliponunua heka 1. Kwenye heka moja ni kijijini kabisa ambapo watoto watakuja na kurudi nyumbani kwa miguu (kwa kuanzia).Ninachotakiwa sasa ni kujenga darasa moja ambalo litakuwa multi-purpose kwa chekechea, msingi au hata secondary. Sina uhakika kama hii 8m itatosha kwa darasa hili,maana ninayo kamili. Ninatakiwa kupiga mahesabu kabla ya kuanza ujenzi naogopa kuishia katikati,natamani dara likamilike chekechea ya watoto 70 ianze. Halafu nianze kujipanga kuongeza darasa jingine.
Asante sana, ubarikiwe, maoni yako ni mazuri.
Ungeweza kusema exactly location ulipo ingesaidia kukupa idea zingine za ujenzi...
Nina ndoto kama zako za kuanzisha shule,nimejitahidi kutembelea shule nyingi za binafsi, mashirika ya dini, ngo,na za serikali. Kote huko nilikuwa/ninaendelea kuokoteza vionjo mbali mbali ili nikifika ktk implementation ya ndoto zangu nisilazimike kutoa rushwa au kuingia gharama kubwa kwa mambo yanayoepukika mapema.
Anza na chekechea kwenye hicho kiwanja chako. Ila usijenge shule ktk kiwanja hicho, ni kidogo mno. Chekechea pia inataka vibali na usajiri. Ukipata usajiri wa chekechea, unatumia kibali cha chekechea kuombea shule yako ya msingi na baadae sekondari. Kuna raha kubwa kuwa na wanafunzi unaowajua vizuri tangu wakiwa wadogo. Baadae unaomba A level na hatimaye chuo kikuu au chuo cha kati.
Hiyo pesa, nenda nje ya mji, tafuta eneo kubwa kabisa zuri, liombee kwa Mungu wako. Anza kujenga shule yako hapo kwa kuanza na mazingira kama huna hela, wakati ktk kiwanja chako cha sasa kuna kituo cha chekechea. Utakapoulizwa maabara, utajenga wapi, utakapotakiwa kuwa na uwanja wa michezo utaweka wapi, nyumba ya matron/patron utajenga wapi, vyoo vyako utajenga wapi,arena itakaa wapi.Je hati ya kiwanja unayo?
Muda ni mchache, ningechangia mengi.
Usiache kutimiza ndoto yako,maana yatoka kwa Mungu.
Mkuu nafikiri masharti ya kufungua shule ni lazima uwe na EKA 10 na yenye hati yaani title deed
Kuwa na eneo kubwa ni vizuri.
Nina eneo kubwa lipo msangaMkuu hiyo pesa mbona ndogo snaa bado. .
hujanunua kiwanja. .
Ujenzi bado hapo
Vitabuu , walimu ..
badoo sana. .