Kuanzisha Shule ya Msingi na Sekondari: Utaratibu wa Kiserikali, Ushauri, Changamoto na Faida

nilikuwa na ndoto kama hii kipindi niko Olevel mpaka chou ya kuwa na shule yangu binafsi ila kwa sasa nimejikita kwenye kilimo na ufugaji na kwa kweli imenifanya niheshimike
Safi sana mkuu, banafsi suala la Kilimo ni moja ya malengo makuu makubwa niliyo nayo. Hongera sana mkuu kwa hatua kubwa hiyo, maana unaposema 'Umeheshimika maana yake ni kubwa sana, kwa mtu anayejua"

Hongera sana.
 
Safi sana mkuu, banafsi suala la Kilimo ni moja ya malengo makuu makubwa niliyo nayo. Hongera sana mkuu kwa hatua kubwa hiyo, maana unaposema 'Umeheshimika maana yake ni kubwa sana, kwa mtu anayejua"
Hongera sana.
Kabisa, niko mbali sana kaka...
 
Wadau karibuni basi tu share mawazo
 
Hongera sana mkuu, ndiyo ndoto yangu na mimi siku moja kuwa na shule yangu. Namuomba Mungu anisaidie.
 
Ili uweze anzisha shule vigezo vikubwa kwangu vinavyonipa shida ni

-hati, ofa ya kiwanja chenye ukubwa wa ekari 3 na 1/2 kwa mjini na 7 na nusu kwa kijijini.

-uthibitisho wa uwezo wa fedha ktk akaunti yako, (zaidi ya m.62).

Vingine vyote kwangu naona rahisi.

Wazo zuri mkuu, mimi mwakani nimeapa lazima nianze mchakato mnamo mwezi aprili. Kila la heri nawe pia
 
Nilikuwa na ndoto kama hii kipindi niko Olevel mpaka chou ya kuwa na shule yangu binafsi ila kwa sasa nimejikita kwenye kilimo na ufugaji na kwa kweli imenifanya niheshimike.
mkuu samahani ningependa kufahamu kilimo chako unakifanyaje
 
Shule nyingi zimefeli kipindi hiki cha magu.Ila shule ni uwekezaji endelevu.Cha msingi lazima uwe na business plan nzuri, team nzuri utafikia lengo.Eneo ni dogo, hutakuwa na eneo la viwanja na kota za wafanyakazi.Ukitaka kufanikiwa Fanya yale ambayo wengine hawafanyi.

Mfano shule nyingi hazijawekeza katika matumizi ya teknolojia, shule nyingi hazitoi michezo na Sana'a kwa uzuri kabisa.Fanya kitu ambacho kititofautisha shule yako na nyingine.

Jambo lingine uwe focused. Don't be like technician entrepreneur. Unafanya mambo mengi hafu huyaendelezi.komaa na jambo moja likifanikiwa baadae diversify(This is a principle)
 
Nilikuwa na ndoto kama hii kipindi niko Olevel mpaka chou ya kuwa na shule yangu binafsi ila kwa sasa nimejikita kwenye kilimo na ufugaji na kwa kweli imenifanya niheshimike.
Hongera Sana! Kwa kupata mafanikio kupitia kilimo na ufugaji, labda nasi ungetupa walau A,B,C unalima nn na unafuga nn? Na umewezaje kutoboa tundu kupitia kilimo na ufugaji?

Nasubiria mrejesho kwa furaha kubwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mm sio mahiri saana kwenye kujadili humu ila leo imenibidi nichangie mawili matatu kwa kuwa umegusa kunako.

Binafsi nafanya kazi kwenye taasisis ya kielimu ambayo kazi yake kubwa ni kuendesha mashule na kuanzisha mashule. Na npo dodoma miaka miwili sasa nikiwa kama mratibu wa kanda ya kati wa taasisi hiyo.

Kwa Dodoma hapa tuna project ya ujenzi wa shule wa eneo flani hapa hapa dodoma mjini.

USHAURI WANGU JUU YA WAZO LAKO
1. Kwa eneo lako hilo ni dogo kulingana na vaigezo vya serikali ni vema utafute eneo kubwa zaidi kuanzia hekari 3 mpaka 7. (Tatu kwa mjini na 7 kwa nje ya mji)

2. Kwa uzoefu ulioelezea hapo naona ni bora ungeanza kukodisha shule kwa kuingia mkataba wa kisheria wa uendeshaji wa shule, ili kidgo kidgo uweze kukusanya mtaji kwa ajili ya ujenzi wako binafsi (binafsi taasisi yangu inaendesha shule zaidi ya 30 ila inamiliki shule 1 tu. Ila ina waajiriwa zaidi ya 200)

3. Watu wengi kwa sasa wanashindwa kuendesha kwa changamoto kadhaa wa kadhaa kwa hiyo huo uzoefu ulio nao nahic bado hutoshi. Coz kwa mfano taasisi imeweka waratibu kila mkoa kwa ajili ya kutangaza shule kukusanya wanafunzi.

4. Kuna mbinu nyingi za kupata wanafunzi, kuimarisha matokeo, kupunguza matumizi katika shule ambapo ni tofauti kabisa sehemu au kampuni nyingne.

5. Yaani hr wa kampuni nyingne kuna uwezekano mkubwa akaferi endapo akiingia shuleni. Na hata mwalim wa kawaida, kwenye kuendesha shule binafsi kwenye zama hzi anaweza akaferi kama hana skills na machachari ya kusavaivu kwenye tasnia.

MENGI ZAIDI PM TUNAWEZA KUJUZANA.
 
Habari yako mkuu,

Mm sio mahiri saana kwenye kujadili humu ila leo imenibidi nichangie mawili matatu kwa kuwa umegusa kunako. Binafsi nafanya kazi kwenye taasisis ya kielimu ambayo kazi yake kubwa ni kuendesha mashule na kuanzisha mashule.

Na nipo Dodoma miaka miwili sasa nikiwa kama mratibu wa kanda ya kati wa taasisi hiyo. Kwa Dodoma hapa tuna project ya ujenzi wa shule wa eneo flani hapa hapa Dodoma mjini.

USHAURI WANGU JUU YA WAZO LAKO.
1. Kwa eneo lako hilo ni dogo kulingana na vaigezo vya serikali ni vema utafute eneo kubwa zaidi kuanzia hekari 3 mpaka 7. (Tatu kwa mjini na 7 kwa nje ya mji)

2. Kwa uzoefu ulioelezea hapo naona ni bora ungeanza kukodisha shule kwa kuingia mkataba wa kisheria wa uendeshaji wa shule, ili kidgo kidgo uweze kukusanya mtaji kwa ajili ya ujenzi wako binafsi (binafsi taasisi yangu inaendesha shule zaidi ya 20 ila inamiliki shule 1 tu. Ila ina waajiri zaidi ya 200)

3. Watu wengi kwa sasa wanashindwa kuendesha kwa changamoto kadhaa wa kadhaa kwa hiyo huo uzoefu ulio nao nahic bado hutoshi. Coz kwa mfano taasisi imeweka waratibu kila mkoa kwa ajili ya kutangaza shule kukusanya wanafunzi.

4. Kuna mbinu nyingi za kupata wanafunzi, kuimarisha matokeo, kupunguza matumizi katika shule ambapo ni tofauti kabisa sehemu au kampuni nyingne.

5. Yaani hr wa kampuni nyingne kuna uwezekano mkubwa akaferi endapo akiingia shuleni. Na hata mwalim wa kawaida, kwenye kuendesha shule binafsi kwenye zama hzi anaweza akaferi kama hana skills na machachari ya kusavaivu kwenye tasnia.

MENGI ZAIDI PM TUNAWEZA KUJUZANA
 
Ulikwamia wapi kwenye NGO? Kupitia huko ungepata uzoefu mzuri wa kuanzisha na kusimamia hiyo Shule.
 
Wazo ni zuri, kuhusu shule eneo ulilonalo halitoshi! Waza kupanua eneo! In any school planning enough land is the first to consider.
 
Mkuu anzisha nursery school, then ndo uende kwenye primary au sec. Nursery zinalipa sana. Umechelewa tena. Usitake kusimamisha shule kwa siku moja. Hata Rome haijajengwa kwa siku moja.
 
Daaah hizi mada nazikuta huku zinanihamasisha sana hii ni baada ya Mimi kutamani kumiliki shule yangu binafsi. Jamani, mtu asaidie ilitufikie wapi na tuanzie wapi.
 
MKUU ULISHAANZISHA SHULE AU CHUO?

USHAURI WANGU,

Kama bado hujaanzisha shule au chuo...nakupa.ushauri huu.Anzisha shule ya ufundi na michezo(sijui itaitwaje) ila mawazo yangu natamani iwe shule itakayofundisha ufundi aina zote,kuendeleza vipaji vya watoto wenye vipaji vyote...hasa uimbaji,michezo aina zote...football,netball, volleyball, swimming.. n.k..

Yaani chuo kiwe na uwezo wa kuchukua watoto wote walioshindwa kusoma secondary zao hizi rasmi,wewe chukua fundisha umeme,fundisha udereva,n.k

Mfumo wake uwe kama VETA,Ila sasa chuo chako,kiende zaidi ya chuo cha VETA,naamini ukienda na proposal nzuri serikalini wanakukubalia kukupa kibali cha kufungua chuo cha namna hiyo.

Vingenevyo kama unafungua chuo cha ualimu,sijui secondary,vitu ambavyo jamii imeshaanza kuona havina msaada tena Kwenye maisha halisi...,utawika miaka michache harafu chuo kitakuja kukosa watu.

Huo ndo ukweli mkuu nimekwambia,achana na mawazo hayo ya chuo,shule,sijui...nini...wewe fungua shule ya ufundi na michezo,iwe ya tofauti Tanzania nzima...,inafundisha ufundi wa kila aina,pia michezo aina zote ambazo mtoto anaweza.

Utasaidia sana Taifa letu,na watoto wetu,sasa mtoto kiswahili anapata F,history F,maths F, harafu bado mzazi unatumia gharama tena aanze kurudia sijui masomo apate credits,huko anakoenda ataenda kufanya nini?

Kumbe mtoto alikuwa ni mwanariadha,mwan a masumbwi,mcheza Mpira mahiri,mwimbaji mahiri? Hivi hawa akina rashid matumula,Filbert bayi,samatta,mwakinyo,akina tenga,sade manara,diamond, alikiba,ladyjeey dee,ray kigosi,Stephen kanumba(r.i.p) tungewapata wapi? Bila juhudi zao na kudra tu za mwenyezi Mungu?

Tumekariri vitu vile vile miaka nenda rudi ,havitusaidii ila bado tu tunavifanya...tunaona mfumo wa elimu yetu umekaa vibaya...ila bado tunakomaa nao tu.watu kama nyie wenye maono ya kutoa huduma kubwa hizi za shule ,chuo Kwenye jamii.lazima mje na mawazo mbadala kabisa kuokoa Taifa letu.

Nawasilisha.
Asante
 
Aisee
 
HIYO YA KUFUNGUA CHUO CHA UFUNDI NAKUKUBALIA KWA ASILIMIA ZOTE.
LAKINI HIYO YA KUANZISHA MICHEZO HAINA MAANA KABISA,KWA SABABU WATANZANIA HATUNA HUO UTAMADUNI WA KUSOMEA MICHEZO,HAKUNA MZAZI ATAMLIPIA MTOTO WAKE ADA KWA AJILI YA KWENDA KUCHEZA.
WACHEZAJI WOTE WAKUBWA KAMA AKINA SAMATTA WALIANZIA KUCHEZA MTAANI TU HADI WAKAONEKANA NA CLUB KUBWA.
HIYO YA CHUO CHA UFUNDI NI RAHISI KUTOBOA KWA SABABU VIJANA KARIBU WOTE WALIOFELI SHULE KIMBILIO LAO HUWA NI UFUNDI.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…