SoC04 Kuanzishwa kwa Somo la Sheria, kuanzia shule za msingi mpaka Sekondari

SoC04 Kuanzishwa kwa Somo la Sheria, kuanzia shule za msingi mpaka Sekondari

Tanzania Tuitakayo competition threads

Abdulmanafi

New Member
Joined
May 17, 2024
Posts
1
Reaction score
2
Jamii inauhitaji mkubwa wa kujua SHERIA mbalimbali muhimu. Kutojua SHERIA sio sababu ya mtu kujitetea dhidi ya shitaka lolote linalomkabili mbele ya mahakama, hivyo kunauhitaji mkubwa kwa jamaii kujua SHERIA.

Pia kupitia ufundishaji huo wa SHERIA mashureni, utawawezesha pia watoto kujua haki zao na mbinu sahihi za wao katika kujikinga na kujilinda dhidi ya unyanyasaji zidi Yao endapo tu watajua na kuzitambua SHERIA zinazowahusu. Pia tutaweza kupunguza kiasi Cha ualifu kwa kua watu watajua kipi SHERIA chakataza na kipi Cha ruhusu kwani nchi yetu yaongozwa na sheria.

Mfumo mpya wa ufundishaji uanzishwe mashureni katika SOMO Hilo la SHERIA kwa kuzingatia zile sheria muhimu tu kwa jamii kwani ni vigumu kufundishwa Kila sheria kwa ufasaa. Zizingatiwe tu zile sheria muhimu kama haki za binadamu, katiba na uongozi kwa ujumla KUANZIA chini MPAKA juu, sheria za mazingira, makosa ya jinai na madai pia, sheria za miradhi, baadhi ya sheria za ndoa na zinginezo muhimu kwa jamii kuzifahamu.

Kujua huko sheria kutasaidia pia kuchochea hamu kwa vijana kushiriki katika chaguzi za uongozi mbalimbali na hata kushiriki katika mahamuzi mbalimbali katika jamii, pia itasaidia kuongeza uzalendo zidi ya nchi yao. Unyanyasaji pia wa kijinsia utapungua, kwani kupitia sheria za haki za binadamu zitawasaidia kujua njia za kutafuta utetezi zidi ya unyanyasaji huo.
 
Upvote 3
Mfumo mpya wa ufundishaji uanzishwe mashureni katika SOMO Hilo la SHERIA kwa kuzingatia zile sheria muhimu tu kwa jamii kwani ni vigumu kufundishwa Kila sheria kwa ufasaa. Zizingatiwe tu zile sheria muhimu kama haki za binadamu, katiba na uongozi kwa ujumla KUANZIA chini MPAKA juu, sheria za mazingira, makosa ya jinai na madai pia, sheria za miradhi, baadhi ya sheria za ndoa na zinginezo muhimu kwa jamii kuzifahamu.
Nzuri, elimu elimu elimu, watanzania tunahitaji kukubali kujielimisha katika kila nyanja inayogusa maisha yetu.

Subiri hapohapo waje wale wa kusema watoto wapunguziwe masomo, wakupopoe
 
Back
Top Bottom