Kubadilisha gia angani kwa NECTA na maajabu Kemobos

Kubadilisha gia angani kwa NECTA na maajabu Kemobos

ww jamaa sema tu unaipigia upatu hiyo KEMEBOS.........

Huwezi shindanisha watoto wanaolipa ada M10 kwa mwaka na hawa elimu bure kwani wanasoma katika mazingira tofauti ...

Nawapongeza Necta kwa hili ingawaje wamechelewa kustuka kwani tushapiga sana kelele huu utaratibu wa kutangaza top best ni promo ya biashara na kuchochea wizi wa mitihani
Kama mtihani ni mmoja tayari hapo wameshashindanishwa.
Mmoja kutoka kemebos kapata one ya 7.
Mwingine kutoka Nachimeru SS kapata three ya 23.
Mwenye one tayari ana advantage dhidi ya huyo mwenye three.

Kilichofanyika ni kuficha tuu tusione udhaifu, ila udhaifu upo.
 
Ukisema hamna haja ya promotion ya waliofaulu ni kama unawanyima haki ya msingi ya kuwa recognized kutokana na efforts zao.

Hata makazini humo msipopandishwa vyeo huwa mnalalamika sana. Magufuli hakuwaongeza mshahara mkalalamika wee ila hili la wanafunzi wenye juhudi kuwa recognized hamtaki. Eti oh shule itapata umaarufu ni kweli lazma shule ipate umaarufu sababu wamesajili cream.
IST, ISM, Agakhan, Academic, FK, HOPAC lini umesikia zikitangaza wanafunzi bora?
 
Si ndio hapo sasa...Ilboru, Kibaha, Tabora Boyz ilikuwa inazikimbiza hizi shule za private...wakubali tu sasa hivi wamekuwa wazembe
Hujaona matokeo ya hizo shule tajwa?
 
Ndio pesa za wajinga hizo. Mi nawaonaga watanzania wanaotoa mamilioni ya pesa kwa mwaka kusomesha mtot moja O level ni limbukeni na mjinga aiyejielewa. Wenzetu walioendelea hawafanyi ujinga huo. Mnawaibia wajinga, halafu watu wetu wanapenda sana social classes ndiko mnakowapatia wanapenda sifa za kijinga.
Wenzenu kina nani?
 
- muhaya hata kiswahili hujui, eti ' husiokuwa' jifunze kiswahili au Elimu yako STD 7 una kazi ya kusifia wenzio kina Prof mutembei,prof mukandala.
-mkoa wa kagera generally ni mkoa masikini hapa Tanzania, kwenye kuchukua takwimu hatuangalii huko vijijini kwenye magorofa na Nyumba bora, tunachukua Wastani wa mkoa wote umeelewa ww Muhaya.
- Piga picha stendi ya bukoba mjini tuione
Sina muda wa kubishana na small minded people, watu wasiohoji....wew kiswahili unajua?au unafikiri kujua kiswahili ndo kuelimika? Hiv ni mhaya au muhaya? Hebu jifunze nawe kuandika kiswahili au unawaza mimi hapa ninayetoa hoja nikiwa huru ni maskini[emoji23]

So unatumia stendi ya mkoa kupima umaskini[emoji23] na unakataa ubora wa makazi huko vijijini...
 
wezi wakubwa wa mitihani.

hizi shule zipo kibiashara zaidi na hivyo wapo tayari kufanya vyovyote vile ili mradi tu washike top 10 ndio maana wanllalama eti kisa hawajatangazwa!! upuuzi mtupu!
Wamelipa vipindi ili kuonesha kilichofanyika si sahihi
 
Kwa mzazi anayejua kusoma na kuandika hahitaji NECTA kujua shule bora. kwani zile wanazolipa 78M ada ya mwaka hua zinatangazwa na NECTA? Mnashindana form 4 na form 6 then watoto mnawarunika UDOM sawa na wale waliopata daraja la 3.
Wanaolalamika ni wamiliki wa shule, wanafunzi
 
Ndo maamuzi yametoka. Na Kuanzia 2024 Serikali itakuwa na English Medium zake kwa bei ya kawaida,
Hivi hii imeshapitishwa mkuu ama bado. Hebu usiniambie. Hilo suala namie nilikuwa naliwaza mno. Ujue ntt inabidi azoee lugha akiwa mdogo so anakuwa nayo baadaye iyo Hali inakuwa Ile automatic kwake kuongea bila ya kuwaza
 
Nchi zilizoendelea zimefuta mitihani ya machujio zamani sana

USA ukianza la kwanza hakuna mchujo wowote mpaka unafika HIGH SCHOOL.

hata kama kilaza namna gani una uhakika wa kufika high school
Hawa wetu wakiachiwa waende tutaandaa janga kubwa.

Marekani grading ipo vizuri tu.

Mitihani inafanyika kawaida
 
Ilboru na Kibaha zimejaribujaribu, ila kemebos moto mwingine kabisa
Hizo shule wanafunzi hawasimamiwi kama kemebos, kemebos hadi muda wa kuoga mbapangiwa.

Kibaha iko open, ni rahisi mtu kwenda mail moja kufanya mambo yake
 
Hivi hii imeshapitishwa mkuu ama bado. Hebu usiniambie. Hilo suala namie nilikuwa naliwaza mno. Ujue ntt inabidi azoee lugha akiwa mdogo so anakuwa nayo baadaye iyo Hali inakuwa Ile automatic kwake kuongea bila ya kuwaza
Kila halmashauri itatenga shule kadhaa za English medium za kulipia.
 
Kumbe unaajenda yako ya kuitangaza hiyo kemobos.. Tv na redio si zipo shida wapi
 
Nchi nyingi zilizoendelea hakunaga cha kutangaza sijui best student or school. Wanaamini kila mwanafunzi ana uwezo tofauti ,so kuwashindanisha haina tija. Halafu huwezi wapima wanafunzi kwa mtihani mmoja tu.
 
Pia kuna shule za ndugu wale huwa zinashika mkia tangu zianzishwe ni aibu tupu. Wanaajiri walimu wenye itikadi yao hata kama ni empty set vichwani mwao. Kwa huu mtindo mpya wa kutotaja shule bora kutaficha udhaifu wa shule za hao ndugu
Kama wewe upeleki watoto wako kwenye shule za hao ndugu unawashwa washwa na nini?
 
Cha ajabu sasa, mtaani wanatoboa akina diamond, hamonize, ali kiba, fei toto😂😂,
Huku hao wanaofaulu wakienda kufanya kazi serikalini, na wengi kuishia kuishi kwa kula milungula🤷‍♂️
Huu huwa ni upotoshaji ukichukua middle class yote Tanzania utagundua waliosema ni wengi kuliko wasiosoma na walio chini ya Pato la Dola 1 kwa siku utakuta Zaidi ya 70% Wana elimu ndogo yaani la saba mpaka iliteracy!!

Sample ya Harmonize mmoja tu kati ya illiterates million 10 inakua outlier tu sio hali halisi. Embu niambie nani ana PhD hii Tanzania alafu anaishi chini ya dollar 1 kwa siku? Then nitafutie wote ambao hawajasoma niambie wangapi wanaishi juu ya dollar kwa siku?

Takwimu za ILO ziko wazi kabisa kwa umaskini una correlation na elimu so usipotoshe wengine wakidhani ukiwa hujasoma basi utatoboa kama harmonize!!!
 
29.1.2023 Necta imetangaza rasmi matokeo ya kidato cha nne (CSEE) 2022, matokeo haya yamekuja na utaratibu mpya ambapo hakuna kutajwa nafasi ya shule kitaifa na kimkoa maana yake pia hakuna utaratibu wa kutaja shule zilizoongoza kitaifa sanjari na hayo NECTA imefuta utaratibu wa kutaja wanafunzi waliofanya vizuri kitaifa maana yake zile mbwembwe za kwenda kupongezwa bungeni na kuitwa TO zimezikwa rasmi.

Vijana wa shule kama Mzumbe, Ilboru, Kibaha na nyinginezo watakuwa hawasomi kwa mzuka tena ili kuibuka kipanga wa TAIFA(TO). Moja ya sababu iliyotajwa ni kuwa NECTA imeona kwa kutangaza shule zinazofanya vizuri inazipa promo la bure shule hizo, hapa sijui wanataka shule zianze kulipia matangazo 🤣 anyways ya NECTA tuwaachie wenyewe.

Taratibu mpya za utangazaji matokeo za NECTA hazijafanya jitahada za baadhi ya shule zisijulikane, hapa nazungumzia maajabu yaliyofanywa na shule kutoka mkoani BUKOBA ijulikanayo kama KEMOBOS, shule ya KEMOBOS kama ingetokea NECTA imetangaza shule 10 bora za mwaka 2022 bila shaka hii ingeibuka kidedea. Iko hivi ndugu zangu.

KEMOBOS ilikua na watahiniwa 68 katika hao watahiniwa 68, watahiniwa 65 wamepata daraja la kwanza la alama saba(1.7) maana yake wanafunzi 68, 65 wamepata A saba na kuendelea kwenye jumla ya masomo yao.

Watahiniwa wawili ambao kwa shule hiyo tunawachukulia kama watahiniwa wenye uwezo wa wastani wamepata daraja la kwanza la alama nane( 1.8)

Mtahiniwa mmoja ambaye kwa KEMOBOS unaweza sema ndo mtahiniwa mwenye uwezo dhaifu/mdogo au wa chini amepata daraja la kwanza la alama 9 (1.9)

Maajabu hayajaishia hapo katika watahiniwa wote 68 zaidi ya watahiniwa 32 wamenyoosha A kwenye masomo yote waliyoyafanya yani madogo hawa wamekung'uta A kuanzia hesabu hadi Kiswahili.

TETESI: Tetesi Hizi nimezipata kutoka kwa watu wa karibu kabisa wanaohudumu kwenye taasisi hii inayohusika na mitihani ya TAIFA tetesi zinadai matokeo yalikua yatangazwe siku moja baada ya yale ya kidato cha pili 2022 kutangazwa, ila yakasogezwa mbele kwa sababu zifuatazo,

1. Mtihani wa taifa 2022 hakukua na mwanafunzi wa serikali hata mmoja aliyeingia 10 bora. Wote walitoka shule binafsi(private) ambapo watano KEMOBOS, watatu Saint Francis, na wawili Fedha schools.

2. Katika mtihani wa taifa 2022 hakuna shule ya serikali imegusa top 10 kinyume chake shule 10 za mwisho zilizoshika mkia ni shule za serikali sasa hii inaweza haribu sifa ya ana upiga mwingi.

Baada ya kujadili haya ambayo yangesababisha ikaonekana shule za umma hazina elimu bora hivyo kuibua mambo kadha kwa kadha kama mafao duni ya waalimu ikiwemo mishahara na nyenzo mbovu za kufundishia serikali ikaona ije na swaga kwamba "kutaja wanafunzi na shule bora hakuna tija"

3. Kuna siasa za kibiashara zimeingia zenye lengo la kuhujumu shule fulani fulani, kuna baadhi ya matajiri wa mashule wamewalipa watendaji wakuu wa Taasisi hii ili kuvuruga utaratibu ambao umeonekana unazipaisha shule fulani kibiashara .

Mtizamo wangu: Serikali isitumie nguvu nyingi kuficha madhaifu ya shule za umma lazima iyakubali ili zitafutwa mbinu za kusaidia mfano shule za private zina kanuni uwepo wa mtumishi unategemea na anavyofaurisha zaidi ya hapo hana kazi ndo sababu waalimu wa private lazima amalize topic zote zinazomhusu na ataoe mitihani mingi kuwaandaa wanafunzi hali hii ni tofauti kabisa na shule za serikali mwalimu kuingia darasani ni ishu, siku mbili bado NECTA unakuta hata nusu topic wanafunzi hawajafika.

Serikali inatakiwa iangalie namna nzuri ya kuhamisha uendeshaji wa shule za private kwenda shule za umma na sio kuficha takwimu.

View attachment 2499268View attachment 2499269View attachment 2499270
Hivi hawa watu mwishowe wanaishiaga wap?
 
Back
Top Bottom