Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Elimu bure imebadilika kuwa bure elimu.....Vya bure siyo.
Siungi mkono elimu bure.
Hivi kwa nini waga tunachukiwa...tuna majanga kibao ila tukifurahia machache tuliyofanikiwa watu wanamaind [emoji38]...shule za kemebos zipo bukoba sehemu gani? One day nisafiri nikapige hata picha..[emoji16]Hakuna cha sifa hapo bali ni ujinga watanzania kuwa na chuki dhidi ya hao watu. Kuzunguka ni kawaida yao kila matokeo yakitoka au wakiwa na matukio yao wanapelekwa kwenye maeneo kuvinjari. Video hii ni januari 2023 na hayo ni magari ya shule yakiwapeleka wanafunzi shule baada ya kufungua shule na kurejea mjini bukoba. Hii siyo sifa
Sasa wakishangilia wewe unaumia roho? Du bongo watu bado kushika mtutu, tuna chuki za kifalaUnaumwa sio bure!! Yale matokeo yanatoka walikuwa wanazungushwa kushangalia sio kubeba wanafunzi kwenda likizo rejea ile video ya mwaka Jana.
Ni ya mtu binafsi tena hata hakubahatika kusoma sana ila anapenda Elimu hatari...Yeye ni dereva...mara moja moja anaendeshaga school buses za shule yake..Ni ya kanisa gani mkuu? Maana Loyola wameanza kutoa zero
29.1.2023 Necta imetangaza rasmi matokeo ya kidato cha nne (CSEE) 2022, matokeo haya yamekuja na utaratibu mpya ambapo hakuna kutajwa nafasi ya shule kitaifa na kimkoa maana yake pia hakuna utaratibu wa kutaja shule zilizoongoza kitaifa sanjari na hayo NECTA imefuta utaratibu wa kutaja wanafunzi waliofanya vizuri kitaifa maana yake zile mbwembwe za kwenda kupongezwa bungeni na kuitwa TO zimezikwa rasmi.
Vijana wa shule kama Mzumbe, Ilboru, Kibaha na nyinginezo watakuwa hawasomi kwa mzuka tena ili kuibuka kipanga wa TAIFA(TO). Moja ya sababu iliyotajwa ni kuwa NECTA imeona kwa kutangaza shule zinazofanya vizuri inazipa promo la bure shule hizo, hapa sijui wanataka shule zianze kulipia matangazo 🤣 anyways ya NECTA tuwaachie wenyewe.
Taratibu mpya za utangazaji matokeo za NECTA hazijafanya jitahada za baadhi ya shule zisijulikane, hapa nazungumzia maajabu yaliyofanywa na shule kutoka mkoani BUKOBA ijulikanayo kama KEMOBOS, shule ya KEMOBOS kama ingetokea NECTA imetangaza shule 10 bora za mwaka 2022 bila shaka hii ingeibuka kidedea. Iko hivi ndugu zangu.
KEMOBOS ilikua na watahiniwa 68 katika hao watahiniwa 68, watahiniwa 65 wamepata daraja la kwanza la alama saba(1.7) maana yake wanafunzi 68, 65 wamepata A saba na kuendelea kwenye jumla ya masomo yao.
Watahiniwa wawili ambao kwa shule hiyo tunawachukulia kama watahiniwa wenye uwezo wa wastani wamepata daraja la kwanza la alama nane( 1.8)
Mtahiniwa mmoja ambaye kwa KEMOBOS unaweza sema ndo mtahiniwa mwenye uwezo dhaifu/mdogo au wa chini amepata daraja la kwanza la alama 9 (1.9)
Maajabu hayajaishia hapo katika watahiniwa wote 68 zaidi ya watahiniwa 32 wamenyoosha A kwenye masomo yote waliyoyafanya yani madogo hawa wamekung'uta A kuanzia hesabu hadi Kiswahili.
TETESI: Tetesi Hizi nimezipata kutoka kwa watu wa karibu kabisa wanaohudumu kwenye taasisi hii inayohusika na mitihani ya TAIFA tetesi zinadai matokeo yalikua yatangazwe siku moja baada ya yale ya kidato cha pili 2022 kutangazwa, ila yakasogezwa mbele kwa sababu zifuatazo,
1. Mtihani wa taifa 2022 hakukua na mwanafunzi wa serikali hata mmoja aliyeingia 10 bora. Wote walitoka shule binafsi(private) ambapo watano KEMOBOS, watatu Saint Francis, na wawili Fedha schools.
2. Katika mtihani wa taifa 2022 hakuna shule ya serikali imegusa top 10 kinyume chake shule 10 za mwisho zilizoshika mkia ni shule za serikali sasa hii inaweza haribu sifa ya ana upiga mwingi.
Baada ya kujadili haya ambayo yangesababisha ikaonekana shule za umma hazina elimu bora hivyo kuibua mambo kadha kwa kadha kama mafao duni ya waalimu ikiwemo mishahara na nyenzo mbovu za kufundishia serikali ikaona ije na swaga kwamba "kutaja wanafunzi na shule bora hakuna tija"
3. Kuna siasa za kibiashara zimeingia zenye lengo la kuhujumu shule fulani fulani, kuna baadhi ya matajiri wa mashule wamewalipa watendaji wakuu wa Taasisi hii ili kuvuruga utaratibu ambao umeonekana unazipaisha shule fulani kibiashara .
Mtizamo wangu: Serikali isitumie nguvu nyingi kuficha madhaifu ya shule za umma lazima iyakubali ili zitafutwa mbinu za kusaidia mfano shule za private zina kanuni uwepo wa mtumishi unategemea na anavyofaurisha zaidi ya hapo hana kazi ndo sababu waalimu wa private lazima amalize topic zote zinazomhusu na ataoe mitihani mingi kuwaandaa wanafunzi hali hii ni tofauti kabisa na shule za serikali mwalimu kuingia darasani ni ishu, siku mbili bado NECTA unakuta hata nusu topic wanafunzi hawajafika.
Serikali inatakiwa iangalie namna nzuri ya kuhamisha uendeshaji wa shule za private kwenda shule za umma na sio kuficha takwimu.
View attachment 2499268View attachment 2499269View attachment 2499270Katangazeni biashara zenu wenyewe, mnahaha nini km wanafunzi wa hiyo shule wamefaulu siwaendelee form 5 baadaye University matangazo ya nini? Mmezoea kula upepo siyo? Soma kwa faida yako siyo matangazo. Mmewakaririsha majibu watoto wa watu ili mtangaze biashara yenu muwapige ada kubwa hakuna asiyejua maujanja yenu. Hao wanafunzi wenu university wanakuwa wameishiwa pumzi wanapigwagwa vibaya nao hao mnaowaita wa st. Kayumba. Elimu ni mchakato siyo hiyo zima moto ya shule km za kwenu.
Si ndio hapo sasa...Ilboru, Kibaha, Tabora Boyz ilikuwa inazikimbiza hizi shule za private...wakubali tu sasa hivi wamekuwa wazembeHamna ki2 tulize tuliosoma shule kama ilboru tulichokuwa tunawafanya waliotoka shule kama izo.
Ndio pesa za wajinga hizo. Mi nawaonaga watanzania wanaotoa mamilioni ya pesa kwa mwaka kusomesha mtot moja O level ni limbukeni na mjinga aiyejielewa. Wenzetu walioendelea hawafanyi ujinga huo. Mnawaibia wajinga, halafu watu wetu wanapenda sana social classes ndiko mnakowapatia wanapenda sifa za kijinga.
Km wewe tayari ni mjingax2Eti kutangaza Top 10 hakuna tija.....hahahaha
Hivi hawa jamaa wanafikiri kila mtu mjinga mjinga sio....
Mficha maradhi kifo humuumbua....
Mzee wa msoga na Kemebos wap na wap[emoji28]Hyo shule naskia ni ya Mzee wetu wa mzoga.....sema wamejipanga haswaa ....skull buses zao ni yutong kama mabasi ya mkoani
Watu hawapend kujulikana mkuu...ila ndo ivo inajulikana kwamba ni ya mzee....mitihan inavujishwa sanaa pale ila hawafuatiliwiMzee wa msoga na Kemebos wap na wap[emoji28]
Ingia YouTube millardayo kamhoji mmiliki wa shule
Takwimu zinatolewa kilichokatailwa safari hii ni kutangaza top best.Hakuna cha ushindani hapo. Takwimu ni muhimu.
Sema chief hangaya anaogopwa kuumbuka na mikopo Yake ya madarasa.
Analeta habari za kizenji huju Sisi tumeshaziea ligi katika Kila kitu.
Elimu inapoteza morali kabisaa.
- muhaya hata kiswahili hujui, eti ' husiokuwa' jifunze kiswahili au Elimu yako STD 7 una kazi ya kusifia wenzio kina Prof mutembei,prof mukandala.Sasa Tanzania Kuna mkoa husiokuwa maskini....
Mkoa gani huo watu wake wana maendeleo hata kujilinganisha na nchi za dunia ya kwanza...
Tanzania sijaona mkoa unaoweza kusema umeendelea sana hadi waone kagera ni maskini...yote yale yale tu...bora hata huko Bukoba vijijini kuna nyumba bora
Sasa haya ni matatizo ya serikaliNecta walisema mapema sana mwaka 2022 kwamba kuanzia mwaka huu matokeo hayatatoa 10 bora. Walisema hivo kabla hata mitihani haijasahishishwa inawezekana hata iuanza ilikuwa haijaanza.
Point waliyotoa NECTA iko sahihi na serikali inatakiwa kuona ukweli huo. Hivi una akili timamua hata wewe unayeandika kunfananisha mtoto wa private na serikali? Mtoto anaamka asubuhi hajui kama atakula mchana, hana nauli, kwenye daladala anasukumwa sukumwa tu, njiani anakoswa koswa na bodaboda, akifika home wazazi wanaoigana au anapewa ubuyu na maandazi akauze, akirudi apike na kufanya kazi za ndani na wakqti huo umeme uneishq haqwzi kujisomea au anaishi nyumba haina uneme, bado hana madaftari na vitabu vya kusoma kwa sababu serikali haijapeleka vitabu mashuleni kwa ratio hata ya 1:2 ubakuta labda ration ni 1:10😐 na haviendi kila mwaka, je kama kuna mtoto kapoteza kitabu kitakuwa replaced vipi? Bado huyo mzazi hawezi afford vitabu kwa mtoto.Mtoro anarudi home anakuta hata chakula hamna. Mtoto wa tandale ubamfabanisha na mtoto wa Masaki uko sawa kichwani au ni USHABIKI NA MIHEMKO????😳🤔.
Na serikali hili waliangalie ndo maana walimu wanakuwa wakali kuoitikoza kwa sababu serikali inalazimisha wakimu wa serikali kufaulisha katika mazingira yasiyowezekana kabisa wanaguka mbogo kwa wanafunzi katika kutekeleza yasiyo wezekana
Tunapoekekea Serikali itafuta kabisa mitihani.
Kufeli kwa watoto wa shule zaserikali kutaongezeka maradufu.
Hiki kitendo cha kuondoa chujio darasa la saba mpaka sasa haijaleta matokeo chanya.
Mtoto asiye na uwezo anaonekana tangu shule ya msingi sasa unamlazimisha amalize form four ili iweje? Tena kwenye shule ambayo darasa lina watoto 200 walimu wawili.
Kwanini hizo pesa Serikali isiwekeze kwenye kitu ambacho kitaleta tija kwa huyo mtoto ndani ya hiyo miaka minne?
Mfano elimu ya ufundi na ujasiliamali iwe ni lazima kwa watoto ambao hawajafanya vizuri shule ya msingi.
Elimu yetu imejaa siasa hakuna anaejali wanasiasa wanaichezea watakavyo.