Kubadilisha gia angani kwa NECTA na maajabu Kemobos

Kubadilisha gia angani kwa NECTA na maajabu Kemobos

Umeshusha tuhuma pasipokuwa na msingi wa ushahidi. Suala la kutoa matokeo bila kutangaza nafasi za shule kitaifa ni matokeo ya utafiti uliofanywa kwa miaka Sasa.

Njoo kivingine lkn walio wengi tunalipongeza baraza kwa uamuzi huu.
 
29.1.2023 Necta imetangaza rasmi matokeo ya kidato cha nne (CSEE) 2022, matokeo haya yamekuja na utaratibu mpya ambapo hakuna kutajwa nafasi ya shule kitaifa na kimkoa maana yake pia hakuna utaratibu wa kutaja shule zilizoongoza kitaifa sanjari na hayo NECTA imefuta utaratibu wa kutaja wanafunzi waliofanya vizuri kitaifa maana yake zile mbwembwe za kwenda kupongezwa bungeni na kuitwa TO zimezikwa rasmi, Vijana wa shule kama Mzumbe, Ilboru , Kibaha na nyinginezo watakuwa hawasomi kwa mzuka tena ili kuibuka kipanga wa TAIFA(TO).Moja ya sababu iliyotajwa ni kuwa NECTA imeona kwa kutangaza shule zinazofanya vizuri inazipa promo la bure shule hizo, hapa sijui wanataka shule zianze kulipia matangazo [emoji1787] anyways ya NECTA tuwaachie wenyewe

Taratibu mpya za utangazaji matokeo za NECTA hazijafanya jitahada za baadhi ya shule zisijulikane, hapa nazungumzia maajabu yaliyofanywa na shule kutoka mkoani BUKOBA ijulikanayo kama KEMOBOS, shule ya KEMOBOS kama ingetokea NECTA imetangaza shule 10 bora za mwaka 2022 bila shaka hii ingeibuka kidedea. Iko hivi ndugu zangu,

KEMOBOS ilikua na watahiniwa 68 katika hao watahiniwa 68, watahiniwa 65 wamepata daraja la kwanza la alama saba(1.7) maana yake wanafunzi 68, 65 wamepata A saba na kuendelea kwenye jumla ya masomo yao.

Watahiniwa wawili ambao kwa shule hiyo tunawachukulia kama watahiniwa wenye uwezo wa wastani wamepata daraja la kwanza la alama nane( 1.8)

Mtahiniwa mmoja ambaye kwa KEMOBOS unaweza sema ndo mtahiniwa mwenye uwezo dhaifu/mdogo au wa chini amepata daraja la kwanza la alama 9 (1.9)

Maajabu hayajaishia hapo katika watahiniwa wote 68 zaidi ya watahiniwa 32 wamenyoosha A kwenye masomo yote waliyoyafanya yani madogo hawa wamekung'uta A kuanzia hesabu hadi Kiswahili.


TETESI: Tetesi Hizi nimezipata kutoka kwa watu wa karibu kabisa wanaohudumu kwenye taasisi hii inayohusika na mitihani ya TAIFA tetesi zinadai matokeo yalikua yatangazwe siku moja baada ya yale ya kidato cha pili 2022 kutangazwa, ila yakasogezwa mbele kwa sababu zifuatazo,

1. Mtihani wa taifa 2022 hakukua na mwanafunzi wa serikali hata mmoja aliyeingia 10 bora. Wote walitoka shule binafsi(private) ambapo watano KEMOBOS, watatu Saint Francis, na wawili Fedha schools.

2.katika mtihani wa taifa 2022 hakuna shule ya serikali imegusa top 10 kinyume chake shule 10 za mwisho zilizoshika mkia ni shule za serikali sasa hii inaweza haribu sifa ya ana upiga mwingi.

Baada ya kujadili haya ambayo yangesababisha ikaonekana shule za umma hazina elimu bora hivyo kuibua mambo kadha kwa kadha kama mafao duni ya waalimu ikiwemo mishahara na nyenzo mbovu za kufundishia serikali ikaona ije na swaga kwamba "kutaja wanafunzi na shule bora hakuna tija"

3. Kuna siasa za kibiashara zimeingia zenye lengo la kuhujumu shule fulani fulani, kuna baadhi ya matajiri wa mashule wamewalipa watendaji wakuu wa Taasisi hii ili kuvuruga utaratibu ambao umeonekana unazipaisha shule fulani kibiashara .


Mtizamo wangu: Serikali isitumie nguvu nyingi kuficha madhaifu ya shule za umma lazima iyakubali ili zitafutwa mbinu za kusaidia mfano shule za private zina kanuni uwepo wa mtumishi unategemea na anavyofaurisha zaidi ya hapo hana kazi ndo sababu waalimu wa private lazima amalize topic zote zinazomhusu na ataoe mitihani mingi kuwaandaa wanafunzi hali hii ni tofauti kabisa na shule za serikali mwalimu kuingia darasani ni ishu, siku mbili bado NECTA unakuta hata nusu topic wanafunzi hawajafika.

Serikali inatakiwa iangalie namna nzuri ya kuhamisha uendeshaji wa shule za private kwenda shule za umma na sio kuficha takwimu.
Wizi tu wa mithani.
Kama wana akili hivyo mbona ni muda mrefu hatujaona wakifanya lolote kwa taifa zaidi ya wizi tu kwenye mabenki na miradi mikubwa ya serikali!

Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app
 
Ukijua maana ya marketing utaondoa huu ujinga hapa. Fungua hii link uone mwenzio anavyobeba wanafunzi wake toka mikoani kila wakifunga na kufungua shule.

Unaumwa sio bure!! Yale matokeo yanatoka walikuwa wanazungushwa kushangalia sio kubeba wanafunzi kwenda likizo rejea ile video ya mwaka Jana.
 
Hakuna cha sifa hapo bali ni ujinga watanzania kuwa na chuki dhidi ya hao watu. Kuzunguka ni kawaida yao kila matokeo yakitoka au wakiwa na matukio yao wanapelekwa kwenye maeneo kuvinjari. Video hii ni januari 2023 na hayo ni magari ya shule yakiwapeleka wanafunzi shule baada ya kufungua shule na kurejea mjini bukoba. Hii siyo sifa

Kwamba wahaya hawana sifa labda huwajui...kila kabila tabia zao zinafanana.
 
.
20230129_121844.jpg
 
ww jamaa sema tu unaipigia upatu hiyo KEMEBOS.........

Huwezi shindanisha watoto wanaolipa ada M10 kwa mwaka na hawa elimu bure kwani wanasoma katika mazingira tofauti ...

Nawapongeza Necta kwa hili ingawaje wamechelewa kustuka kwani tushapiga sana kelele huu utaratibu wa kutangaza top best ni promo ya biashara na kuchochea wizi wa mitihani
Alipie tangazo
 
Wewe ndiye mwenye unaumwa na inawezekana umeijua KEMEBOS na pacha wake Kaizirege mwaka jana. Kwa taarifa yako tu kuzunguka na mabasi yao kwenye viunga vya mji wa bukoba umekuwa utamaduni wao tangu shule hizi zilivyoanzishwa. Kwa wanakaa bukoba wanalijua hilo na linafanyika kuanzia kila matokeo yanapotoka kuanzia darasa la iv mpaka kidato cha sita.
Ushamba toka hapa!!! Kwa sifa Nan asiyewajua ...mbona takwimu za umaskini zikotoka hawashangilii
 
Unajua ada ya FEZA

Haya hiyo M5 unaichukuliaje hafu uje umshindanishe na elimu bure shule za kata kwa kifupi Necta wako sahihi wizi wa mitihani utapungua sana
Kwa nini unasema ELIMU BURE? Sema elimu inayogharimiwa na serikali kwa asilimia 70 (majengo, fenicha, mishahara ya walimu nk) na asilimia 30 mzazi (uniforms, madaftari, Nauli, chakula nk)
 
Cha ajabu sasa, mtaani wanatoboa akina diamond, hamonize, ali kiba, fei toto[emoji23][emoji23],
Huku hao wanaofaulu wakienda kufanya kazi serikalini, na wengi kuishia kuishi kwa kula milungula[emoji2369]
Hoja ya kindezi sana hii jombaaa hivi kwenye watanzania 61 milioni tumeambiwa vijana ni almost 70 % (nearly 43 milioni) hao wakina Diamond, Harmonize etc ni wangapi?? Mimi hapa niki reflect mates wangu kuanzia form 4, form 6 na chuo zaidi ya asilimia 80 wanaendesha maisha yao vizuri tuu kama waajiriwa serikalini, sekta binafsi na nje ya nchi. Wengine kwa elimu yao wamejiajiri na kuajiri wengine (kuna ambao ni madaktari wakubwa, kuna ambao wana mashule nk). Majority ya walioshia darasa la saba wameishia kuwa wakulima, ni wachache sana walioishia std 7 wametoboa na kuwa na maisha ya middle class...
 
Nipe takwimu za umasikini wa KEMEBOS maana hujielewi. Bahati mbaya umejifungia hapo kwenye kiota cha shemeji yako hata hujui kinachoongolewa hapa. Ukitaka kujadili umasikini anzisha mada na utaje kabila na mkoa wako ili tujadili vyema. Inawezekana wahaya walikut ombea dada yako. Naona hata ukiulizwa hao unaosema wana sifa hujui wanapatikana mkoa upi?
Wewe toa ushamba hapo ni wahaya ndo wanakaa kusifia iyo shule behind mkoa wa Kagera ni maskini ..kama hujui jaribu hata kusoma na kufautailia njoo uone status zao huku wanavyojinadi.
 
Hapo shuleni wewe ni mkuu wa shule, mtaaluma au ndio mwenye shule?
 
CCM wanataka kuendelea kutawala watu wajinga ,wanakwepa majukumu Yao waachie ngazi
 
Wewe toa ushamba hapo ni wahaya ndo wanakaa kusifia iyo shule behind mkoa wa Kagera ni maskini ..kama hujui jaribu hata kusoma na kufautailia njoo uone status zao huku wanavyojinadi.
Sasa Tanzania Kuna mkoa husiokuwa maskini....

Mkoa gani huo watu wake wana maendeleo hata kujilinganisha na nchi za dunia ya kwanza...

Tanzania sijaona mkoa unaoweza kusema umeendelea sana hadi waone kagera ni maskini...yote yale yale tu...bora hata huko Bukoba vijijini kuna nyumba bora
 
Back
Top Bottom