Kubali au kataa lakini page ya Mange Kimambi ya instagram ndio talk of the town kwa sasa

Mange tofauti yake na Gigy ni ndogo sana, wote ni watafuta attention kwa kila njia.

Anachofanya mbona muhuni yeyote anaweza, kujificha na kutukana wenzako ukiwa ndani ya chumba nani anashindwa, aje huku awe anafanya press conf ya hizo harakati zake ndio tumuone kweli Mwanaharakati.
 
Zari ondoa hapo sio Mtanzania

Baada ya hapo mie ndio maarufu🙂
 
mkulu mwenyew na mawaziri wake wanamchunguliaga akipost kitu tu wanakanusha fasta
 
Tatizo lake hapendi challenge, ukiwa against nae kidogo tu, block itakuhusu.

Ana Bahati mbaya linapokuja suala la matumizi ya akili.
 
Naamini sote Tumeanza Mwezi Wa December wenye shamrashamshara za kipekee, nikiwa bado niko Arusha nikimalizia kazi, nimeona nirudi tena kwenu kwa salamu za December.

Kwanza nataka CHADEMA na Afisa Habari wenu mnayemheshimu Mange Kimambi mtambue kuwa watoto 1,300 wa Kibiti mnaotangaza kuwa wamepotea na kutaka kuwaaminisha Watanzania kuwa wamekufa sio kweli, Kamanda Simon Sirro anasema alitajiwa idadi hiyo kuwa ni ya watoto watoro wa shule (Absentees).

Na kwa kuwa Afisa Habari wenu anayetumiwa na Wazungu kuivuruga Tanzania na nyie kwa Unyumbu wenu mnamtukuza hajui tatizo la utoro Tanzania basi mmedandia hoja na kuanza kushutumu kuwa wameuawa na Serikali imenyamazisha vyombo vya habari visiripoti .

CHADEMA mchukueni Mange Kimambi wenu mpelekeni wilaya zote za Tanzania akajionee tatizo la utoro.

Mwambie Afisa Habari wenu anayefanya kazi kutokea Marekani kuwa kuna wilaya za Tanzania utoro umefikia hadi wanafunzi 7,000 .

Mwambieni wanaoripotiwa kuwa watoro wengine wamehama shule bila kutoa taarifa shuleni ama mamlaka za Serikali.

Mwambie wengine wanaolewa na kutoroka shule, mwambieni wengine wanaacha kusoma na kwenda kwenye uzalishaji mali na familia .

Na hii sio mara ya kwanza, ilikuwa inaokotwa miili ufukwe wa bahari Dar es Salaam. Afisa Habari wa CHADEMA Mange Kimambi akaanza kutangaza wananchi wanaua, na Viongozi wakuu wa CHADEMA wakadandia lakini mpaka leo hawajaonesha ni ndugu wa nani waliuawa kwa idadi ile.

Nataka kuwatahadharisha Watanzania dhidi ya uchochezi unaofanywa na Mange Kimambi.

Wazungu ni wataalamu sana wa kutengeneza akina Mange Kimambi ili waivuruge nchi. Wanatumia mitandao ya kijamii hivi hivi na wanashabikiwa na wananchi.

Tunayoyaona leo Libya yalianza hivi, Wazungu waliwatumia akina Mange Kimambi wakagombanisha watu na Serikali, wakawatengeneza vijana ili wamuue Ghadafi na walifanikiwa wakamuua Ghadafi.

Leo Libya imevurugika, haikaliki na wananchi wa Libya wamekuwa watumwa wanauzwa kama bidhaa. Wanadhalilishwa, na wanauawa kama kuku, Libya neema haipo tena. Libya imekuwa jehanamu .

Ni hayahaya yalifanyika Syria leo Syria ni balaa. Ni hayahaya yalifanyika Iraq. Yanayotokea Iraq wote tunayaona.

Najua Watanzania wanaakili timamu na wanauwezo wa kutambua upuuzi wa CHADEMA na Mange Kimambi wao ambaye baada ya Watanzania kuwaadhibu kwenye kura za udiwani juzi amejaribu kuhamasisha watu waanze kupambana na Serikali eti wameibiwa kura lakini amekwama.

Mimi naomba Watanzania tukiangalie Chama cha CHADEMA . Tuwaangalie viongozi wake, tuwapime wanaitakia nini nchi hii. Hivi chama Serious kinaweza kufika mahali kinamtukuza mgonjwa wa akili kama Mange Kimambi? Yaani Mwenyekiti Freeman Mbowe anamtaja kabisa kwenye hotuba yake na kumshukuru Mange Kimambi? Anayoyaposti Mange Kimambi yanafaa kwenye nchi ya wastaarabu kama Tanzania? Halafu ndio hawa wanataka wapewe nchi.

Tuonane Machame this Xmass .

Ngariba Mkuu
Arusha, Tanzania
01/12/2017
Nakubaliana na wewe ila sikukuu na wewe karibu Kamachumu
 
Kama wewe ndiye wamekutuma kuzima hasira za wananchi, basis ccm wamebakiza makopo, unaandika uharo tu hakuna point hata moja.
 
Mkuu, Instagram unatumia jina gani ili ni-Mtag halafu niwaache Mutagiane.
 
Hivi Chadema wameridhika kabisa kumpa Mange kimambi umbea wa kuandika Instagram? HawaoniChama kinadhalilika?
Hawaoni. Ndio maana wameambulia kata moja ingawa Mange aliwalisha matango pori kuwa kwenye mikutano ya kampeni ya CCM watu walikuwa hawaji kabisa. Ha ha ha, na Chadema wakaingia mkenge.
 
Mange kaza uzi, myanachama ya "Frastration" inalia huku. Hata wanaharakati dhidi ya ukoloni Afrika walijificha nje ya nchi na mwishowe ushindi ulipatikana. Eh Mungu wa mbinguni angamiza mdudu ccm
 
Laana watapata chadema walio tangaza kwenye Media kuwa Wana uwezo wa kumtibu TL hata kwa kuuza Figo. wafuatwe watoe Fedha Kama walivyoahidi.
Yaani mi ccm yote in "frastration" kama top wao. Poleni sana
Kumbe na wewe ni follower wa Mange[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Ccm wote lazima wapitie page ya Mange kila baada ya dakika kumi, misumali inawachoma balaa.
 
Ccm walifanya kampeni za kisayansi ndo mana walishinda kata nyingi...
Sayansi ya kutumia polisi na mapanga kuwakandamiza watu... Kweli ccm n wanasayansi
Ushindi usio na furaha kwa waliopiga hizo kura zinazoaminisha wananchi tumeshinda ni laana huko tuendako kwani hawatakubali kuendelea kuonekana na majonzi ya Msiba kwani ndo tunakoelekea .Ushindi upatikane waliochagua wawe na furaha
 
Naamini sote Tumeanza Mwezi Wa December wenye shamrashamshara za kipekee, nikiwa bado niko Arusha nikimalizia kazi, nimeona nirudi tena kwenu kwa salamu za December.

Kwanza nataka CHADEMA na Afisa Habari wenu mnayemheshimu Mange Kimambi mtambue kuwa watoto 1,300 wa Kibiti mnaotangaza kuwa wamepotea na kutaka kuwaaminisha Watanzania kuwa wamekufa sio kweli, Kamanda Simon Sirro anasema alitajiwa idadi hiyo kuwa ni ya watoto watoro wa shule (Absentees).

Na kwa kuwa Afisa Habari wenu anayetumiwa na Wazungu kuivuruga Tanzania na nyie kwa Unyumbu wenu mnamtukuza hajui tatizo la utoro Tanzania basi mmedandia hoja na kuanza kushutumu kuwa wameuawa na Serikali imenyamazisha vyombo vya habari visiripoti .

CHADEMA mchukueni Mange Kimambi wenu mpelekeni wilaya zote za Tanzania akajionee tatizo la utoro.

Mwambie Afisa Habari wenu anayefanya kazi kutokea Marekani kuwa kuna wilaya za Tanzania utoro umefikia hadi wanafunzi 7,000 .

Mwambieni wanaoripotiwa kuwa watoro wengine wamehama shule bila kutoa taarifa shuleni ama mamlaka za Serikali.

Mwambie wengine wanaolewa na kutoroka shule, mwambieni wengine wanaacha kusoma na kwenda kwenye uzalishaji mali na familia .

Na hii sio mara ya kwanza, ilikuwa inaokotwa miili ufukwe wa bahari Dar es Salaam. Afisa Habari wa CHADEMA Mange Kimambi akaanza kutangaza wananchi wanaua, na Viongozi wakuu wa CHADEMA wakadandia lakini mpaka leo hawajaonesha ni ndugu wa nani waliuawa kwa idadi ile.

Nataka kuwatahadharisha Watanzania dhidi ya uchochezi unaofanywa na Mange Kimambi.

Wazungu ni wataalamu sana wa kutengeneza akina Mange Kimambi ili waivuruge nchi. Wanatumia mitandao ya kijamii hivi hivi na wanashabikiwa na wananchi.

Tunayoyaona leo Libya yalianza hivi, Wazungu waliwatumia akina Mange Kimambi wakagombanisha watu na Serikali, wakawatengeneza vijana ili wamuue Ghadafi na walifanikiwa wakamuua Ghadafi.

Leo Libya imevurugika, haikaliki na wananchi wa Libya wamekuwa watumwa wanauzwa kama bidhaa. Wanadhalilishwa, na wanauawa kama kuku, Libya neema haipo tena. Libya imekuwa jehanamu .

Ni hayahaya yalifanyika Syria leo Syria ni balaa. Ni hayahaya yalifanyika Iraq. Yanayotokea Iraq wote tunayaona.

Najua Watanzania wanaakili timamu na wanauwezo wa kutambua upuuzi wa CHADEMA na Mange Kimambi wao ambaye baada ya Watanzania kuwaadhibu kwenye kura za udiwani juzi amejaribu kuhamasisha watu waanze kupambana na Serikali eti wameibiwa kura lakini amekwama.

Mimi naomba Watanzania tukiangalie Chama cha CHADEMA . Tuwaangalie viongozi wake, tuwapime wanaitakia nini nchi hii. Hivi chama Serious kinaweza kufika mahali kinamtukuza mgonjwa wa akili kama Mange Kimambi? Yaani Mwenyekiti Freeman Mbowe anamtaja kabisa kwenye hotuba yake na kumshukuru Mange Kimambi? Anayoyaposti Mange Kimambi yanafaa kwenye nchi ya wastaarabu kama Tanzania? Halafu ndio hawa wanataka wapewe nchi.

Tuonane Machame this Xmass .

Ngariba Mkuu
Arusha, Tanzania
01/12/2017
kimambi sio afisa habari,ccm leave the ground open
 
Back
Top Bottom