Mag3
Platinum Member
- May 31, 2008
- 13,413
- 23,592
Ahsante Mkuu kwa kunielewa. Nilipoanzisha hoja hii baadhi ya wanaJF waliishia kunitupia madongo tu bila kutafakari. Sikufanya hivyo kwa kumchukia Kubenea ila kwa sababu mimi ni shabiki wake wa miaka mingi. Sasa nasadiki yote waliyonieleza maana yamejitokeza kwa asilimia 100 kwenye toleo la sasa la MwanaHalisi. Mkono wa Rostam, Lowassa na watu wasio na itikadi ndani na nje ya CCM unaonekana bayana!
Kamaudouilton, nimewahi kusoma upuuzi humu JF lakini huu wa kwako ni babu kubwa. Posti kama hii ya kwako kuna sehemu zake, sana sana kule FB kwa akina Nape, Jakaya na mafisadi wengine .
Wewe kuileta hapa JF ni kutukosea adabu, soma tena hiyo habari kwa makini kama mtu mwenye uelewa - Kubenea anajua fika kwamba hakuna ufisadi bila baraka za Kiongozi Mkuu wa serikali ambaye ndiye pia kiongozi Mkuu wa chama tawala.
Haya madai ya wasaidizi kumwangusha Kikwete anayewateua yamepitwa na wakati, huwezi kuongelea Rostamu, Lowassa na Chenge usimtaje bosi na mshiriki wao Mkuu Kikwete.
Huo mkakati wa kujaribu kumtenga Kikwete na kashfa lukuki zinazoiandama taifa mwenye akili katu hawezi kuzikubali na mbinu hiyo kamwe haitafanikiwa, siyo humu JF.